Bei ya mafuta inatisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bei ya mafuta inatisha

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Benno, May 22, 2011.

 1. B

  Benno JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2011
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 332
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tutaendesha magari kweli kwa Bei hii ya mafuta? Bei inapanda sana. What next
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Serikali nyingine kama Ulaya na Marekani bei za mafuta zimeshaanza kupungua tangu wili mbili zilizopita. Nasikia Marekani bei ya mafuta imepungua kwa Cts 10-15 na itaendelea kupungua zaidi. Sasa iweje bongo bei isipungue wakati nchi zinazotoa mafuta ni zile zile zinazouzia Uyala na Marekani?
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Ndo tulivyoamua kuiingiza madarakani serikali isowajali wananchi wake, juzi Bunge la Kenya limesitisha shughuli zake ili kujadili mfumuko wa bei, bongo hii sijawahi kuisikia halafu mtu anavaa linguo la ccm na kuimba kipuuzi tu huku maisha yake magumu balaa.

  Anyways, MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO!
   
 4. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Hivi tatizo haswa ni nini? mbona Rwanda na Malawi bei iko chini kidogo na yanapita hapa kwetu? what is behind all these? hapa nahisi kuna hidden agenda kuhusu hii
   
 5. Habdavi

  Habdavi JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 393
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  kwani hamjui wenye biashara za mafuta ndiyo hao hao waliopo madarakani? Haya yote ni kutokana na sera za magamba. Kukamua jasho la mwananchi mpaka aanguke kwa dehydration.
   
 6. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  It is true kwamba Bunge la Kenya lilijadili suala la kupanda kwa gharama za maisha lakini ilipokuja kwenye suala la hatua zinazopaswa kuchukuliwa, hakuna chochote tangible kilichofikiwa ambacho kinatoa nafuu kwa mwananchi wa kawaida. Survey yangu ndogo katika suala hili accross east africa nimegundua kwamba malalamiko haya yanafanana na kote huko serikali zinalaumiwa kwamba hazijafanya lolote au hazijafanya la maana kuondoa hali hii. Wakati nakubali kwamba viongozi wanapaswa kuwa concerned na hali hii na kuonekana kwamba wanachukua hatua, tunatakiwa kufahamu kwamba mengi ya matatizo haya (hasa hili la mafuta) ni tatizo kubwa zaidi ambalo serikali haiwezi kulimaliza kirahisi. Kenya walishusha kodi na hiyo ingeshusha mafuta angalau kwa shilingi 6 kwa lita lakini baada ya siku sita bei ikapande tena kwa shilingi sita na senti. Hata huko Marekani bei ya mafuta bado iko juu hata kama kuna kupungua huko kidogo. Hata hivyo nakubali kwamba EWURA na wizara wanapaswa kuendelea kutafuta namna bora ya kudhibiti hali hii inayowamaliza watanzania kwa namna ya ajabu sana.

  Mimi nafikiri eneo ambalo serikali inaweza kufanya vizuri zaidi kuliko inavyofanya sasa ni kwenye suala la bei za vyakula na hasa kwa kuwadhibiti hawa wafanyabiashara ambao wakati mwingine wanapata nafuu nyingi za kodi lakini bado bei ziko juu na unafika wakati hujui kama huu ni wakati wa mavuno au la! Lakini suluhisho la tatizo hili siyo mikutano na maandamano maana ingekuwa ni hivyo basi Spain ambako watu wanaendelea kuandamana hali ingekuwa tofauti. Hata walk to work ya Besigye ilishachemsha kule Uganda.
   
 7. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,645
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  nafasi ya kubadilisha mfumo wa utawala tulikua nayo tukakubali kuchakachuliwa!!!

  tusilalamike kwa lolote.. tuwaachie watukamue mpaka utumbo mwembamba, they don care and why should they?
   
 8. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  sahau kupungua kwa bei ya mafuta kwanini mafuta tunanunua kwa pesa za kigeni..sasa kama usd inapanda kwa wastani wa tzs 5 kwasiku kweli unategemea mafuta ya shuke bei..
   
 9. M

  Maimai Senior Member

  #9
  May 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 174
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  masebu ajiuzulu basi
   
 10. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #10
  May 22, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Mbopo acha siasa, tunaongelea kupanda kta bei za mafuta bila udhibita. Ni jukumu la serikali kupunguza ukali huu wa maisha. Sio kazi ya upinzani. Naona umekimbilia kwenye maandamano. Ulikuwa unataka cdm ambao ndo unawazungumzia wafanye nini au wasifanye nini ili shlingi iimarike na mafuta yashuke bei?

  Usiukimbie ukweli.
   
 11. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #11
  May 22, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwa bahati mbaya sana hata ukiulizwa kwa nini shilingi yetu inashuka thamani hutakuwa na majibu ya kisayansi (kiuchumi) zaidi ya kulaumu tu serikali. Ukweli ni kwamba pamoja na kwamba serikali inatakiwa kufanya juhudi kama nilivyodokeza (na kitaalam zaidi kwa weledi wao) lakini matatizo haya hayawezi kumalizwa wala mwananchi hawezi kupata nafuu kwa kuchochewa kwenye maandamano.
   
 12. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #12
  May 22, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,520
  Likes Received: 19,943
  Trophy Points: 280
  kwa mawazo yako ni kuwa politics has nothing to do with Tanzanians life?
  use your brain tupe hayo majibu ya kisayansi hapa,
  mya take: politics ina interfere life la watanzania kwa 100%
   
 13. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #13
  May 22, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  I
  Bado hujasema chochote, kama mwananchi wa kawaida sihitaji kujua sababu za kisayansi wala kihistoria, tumewaajiri ccm waiendeshe nchi, hatutaki visingizio tunataka mabadiliko.

  Sasa sema wewe unaridhika na hali ya maisha kwa maana ya gharama za bidhaa ikiwemo fuel na gas? Ukilinganisha na kipato cha mtanzania? Kama wewe ulipwa vialowance vya kifisadi usivihesabu.

  Haya, nini kifanyike/kifanywe na cdm au kisifanywe ili gharama za maisha zibadilike?
   
 14. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #14
  May 22, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Mkuu, hawa akina mbopo ndo think tanks wa ccm na serikali yake.
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  May 22, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo Mkuu tukae tu na kusubiri kufa?
   
 16. T

  Twasila JF-Expert Member

  #16
  May 22, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,913
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  Niambie mchumi uliyebobea serkaii itumie njia gani kupunguza bei ya chakula! Kama wewe ni mchumi Serikalini basi toa ushauri interventions ambazo zinatakiwa ili thamani ya shilingi isishuke na uchumi usiporomoke. Haitoshi kulalamikia maandamano. Ni haki ya watz kuilalamikia serikali. Wao ndio wameiweka. Kutegemea upinzani wapite mitaani kuishangilia ni kutaka wapinzani wawe jumuiya xa ya ccm. kufiki serikali
   
 17. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #17
  May 22, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Yaani kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta misele yote imekufa, duuuuh na serikali ndiyo kwanza hailisemei hili. Hii limeenda mbali mpaka kupanda kwa bei ya vyakula.
   
 18. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #18
  May 22, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Mbona foleni barabarani hazipungui? au kuna mahala watu wanapata mafuta ya bei poa?
   
 19. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #19
  May 22, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  <br />
  Ni kweli kwa takribani miaka mitatu sasa thamani ya shs imepungua saana kwa shs km 300-400. Sasa wewe wastani wa shs 5 kwa siku unautoa wapi au unaanzia wapi. Tuache uongo pale takwimu zinapoweza kutumika.
   
 20. Kajuni

  Kajuni JF-Expert Member

  #20
  May 22, 2011
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  Mbopo unajichanganya mwenyewe how can the government control the food price while the fuel price is high!!! naona umefikiria tu kwenye maandamano. Let think on the food chain.. Toka chakula kinalimwa mpaka kinafika MEZANI. Kila hatua inaitaji sana mafuta. Mfano tukianzia na pembejeo ili zimfikie mkulima lazima zisafirishwe... njoo kwenye kuvuna kunatumia mashine abazo zinaitaji mafuta usifikirie kilimo cha jembe la mkono Mpobo. Hayo ni mawazo mgando ya sera mbovu za Chama cha Magamba. From kuvuna njoo kwenye storage kuna vyakula kama nyanya vinaitaji cold room.. huu ni umeme ambao unataji mafuta. Njoo sasa kwenye transportation kutoka ruvuma mpaka sokoni kariakoo mafuta yataitajika. In short mafuta ndo kila kitu.. na hapo nimejaribu kufupisha tu. Serikari kupanga bei ya mazao kwa mkulima ni kumtwisha mzigo mkulima ambao haustaili.
  Je wenzetu wanafanya nini? ndo tunakuja na ishu za ruzuku (SUBSIDIES) serikari lazima itoe ruzuku kwa wakulima... kuanzia pembejeo nakadhalika. Pia bei ya mazao inaweza ikabaki vile vile lakini ni jukumu la serikari kuyanunua mazao kwa bei ya sokoni na kuwapunguzia wananchi kwa bei kubalika. Tusidanganyane hapa kama serikari ina nia kuna vyanzo vingi tu vya mapato ambavyo serikari ina weza kutumia ku cushion the increasing fuel price. Sema kwa vile chama chetu kina wazee ambao bado wanamawazo ya ANALOG hawawezi kwenda sambaba na Digital era. Hii kusema hili ni tatizo la ulimwengu mzima au Afrika mashariki ni ukosefu wa kufikiri kama tuna taka tunaweza kuwa wa kwanza na wengine wakatufuata kwamba mbona TZ wameweza? Bwana bwana tatizo ni kwamba ukiwa mwana MAGAMBA hata kufikiri tu akiri inakuwa na Magamba na kitakacho toka ni MAGAMBA TUUUUUUUUUUUUUUU.
   
Loading...