Bei ya mafuta inatisha

itabidi tuwapelekee malalamiko yetu wazee wa maandamano kwani kwenye sukari wamefanikiwa na sasa ni mafuta na ninajua itawezekana, kwani kuna uzi fulani nilisoma unasema ccm inaongozwa na cdm nazani litawezekana...
 
Mbona foleni barabarani hazipungui? au kuna mahala watu wanapata mafuta ya bei poa?

Hapana uchumi unatuambia kuwa kunabidhaa ambazo lazima zitanunuliwa tuuu... we call it demand elasticity??? isipokuwa kuna kitu wanasema ni copying mechanism.... kama mwnzo ulikuwa unakula milo mitatu sasa inafikia watu wanakula mara mbili au mara moja (skipping meal). Kwenye mafuta kama ulikuwa unajaza lita 10 kwa 20,000/= the same amount utanunua lita 8. Kwa hivo unakuta ndo kufunga mkanda na kujaribu kupunguza movement. Mfano kwa hivi sasa serikari ikechukua uamzi mzito wa kuyasimamisha mashangingi yote yanayo zunguka hapa Masaki Posta.....na hizo peza kwenda kutumika kwingineko. Habari ndo hiyo bro.
Mfano mzuri waangalie watu nyuso zao wanaoendesha midude mikubwa....utamwona kama ni binafsi basi kakunja sura na ukijaribu kumchomekea ndo utaona hasira za kuangalia geji zina amishiwa kwako. Siku hizi hata wale ambao walikuwa hawashushi vioo wamerudi kwetu sie na wanajua hadha ya kuendesha mchana na jua kali na joto ndani yake. Hii ndo copying MECHANISM!!!
Hitimisho....Its not true that all CCMs are stupid people but most stupid people are CCMs... MAGAMBA HOYEEEE.
 
haiwezekan kupunguza bei ya bidhaa mbalimbali kam bei ya mafuta ipo juu, hapa tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu, serikal inapaswa kubeba lawama juu ya suala hili, kwani katika hali ya kawaida tu hakuna jitihada zozote zile zinazofanywa na serikali katika kuhakikisha maisha ya Watanzania yanakuwa bora kama wanagamba walivyoahidi katika kampeni zao zisizotekelezeka. mfno ni kwamba wakati hii serikal inapandisha kima cha chini cha mishahara ya watumishi wake mwaka jana sukari ilikuwa 800-1000 lakini leo hii sukari ni kuanzia 1600-2000 imeapanda kwa 1000% lakini serikali bado ipo ipo tu, huyu mtu atamudu vip maisha yake. Viongozi wa serikali wanalipa posho tu kuptia kodi za hawa watanzania ambao inawadhulumu, zaidi ya nusu ya bajet ni kuendesha serikali tu, sasa kweli hapa kuna maisha gan ambayo ni bora zaidi ya kuchoshana tu. Watanzania wana kila sababu ya kuilaumu serikal ya Kikwete na wangamba wenzie. wao wanakula maisha sisi tunateseka tu, kwa kweli tumefika wakati tuwakatae hadharani kwani watanzania walalahoi wamechoshwa na matuimiz mabovu ya rasilimali zao. MH. kikwete Tambua kwamba Watanzania walitegemea maisha bora na sio maisha bora. Lawama zote zinaelekezwa kwako kwa kuwa wewe ndo kiongozi uliyepewa dhamana ya kuongoza nchi hii. Usipoamua kufanya maamuzi amgumu na mazito sio siri hii inaweza kukupa wakati mgumu sana katika kutekeleza majukumu yako. Watanzania tunaomba utekeleze yale uliyoahidi watanzania. Vua gamba Mh. chinjilia baharini hawa mafisadi ili urejeshe imani na matumaini kwa Watanzania, sikiliza maoni ya Watanzania bila kujali itikadi za kisiasa. ni hayo tu kwa leo!
 
Jamani Mimi nadhani naumia zaidi, maana kwa siku nina ratiba ya zaidi ya KM 78, Yaani Home-office-Shule-Home, bado hawa Trafif nao wanatusimamisha humu barabarani sijui huwa wanaongea lugha gani, Maisha ya Dar imekuwa Kero.


Serikali Oneni hili , wanawa Kindimba Juu tunaumia sana, wote hatuwezi Jenga City Center so toka Gongs mpaka Masaki ni mateso.













Ningekuwa na Macho mengi ningetumia kutazama wengine wanapata wapi mafuta ya Dili
 
Back
Top Bottom