Mimi mchango wangu, siwezi kuchangia kama hao wengi walio tangulia, inaonekana wanafanya ushabiki Zaidi kuliko kutumia akili zao vizuri, najua ni akili ndogo lakini mlipaswa kujiongeza kidogo
Nani kati yenu asiejua ubabaishaji wa jeshi letu polisi ?
Mtu kama Gwajima na utajili alionao kuna ubaya gani kmiliki bastola, kwani mpaka tushangae hilo wanao toa kibali cha kumiliki bastola kuna mipaka kwa wachungaji ?
Which means idea 'ya kumtorosha' ilisukwa kwa polisi...kwa ajenda isiyojulikana. Then hapo ndio naanza kuamini kuwa kuna zaidi ya 'matusi kwa Pengo' kwenye sakata hili.
Kwamba idea imesukwa na police
Kwa upande wangu bado nina maswali mengi kuliko majibu kuhusiana na taarifa ya polisi. Kwanza ninachojiuliza ni kuwa polisi wanawezaje kudhibitisha kuwa hao wanaoitwa wafuasi wa Gwajima walikuwa na nia ya kumtorosha? Labda kama wakisema walikuwa wameishambeba na kutoka naye nje ya hospitali. Kinyume cha hapo kwa kuonesha bastola na paspoti haidhibitishi nia ya kumtorosha. Vinginevyo jamaa wanaweza kusema walikuwa wameenda kumfanyia maombi mgonjwa.
Pili: Nashindwa kuelewa uharaka wa polisi kutoa taarifa kwa vyombo vya habari huku mambo mengine ambayo yalikuwa ni rahisi kabisa kupatiwa majibu kabla ya taarifa hiyo yakiiacha bila majibu. Hivi najiuliza: Inaichukua polisi masaa mangapi kujua iwapo bastora iliyokamatwa ilikuwa ikimilikiwa kihalali ama vinginevyo!!!? Kwa nini wameshindwa kufanya hivyo na wamekimbilia kutoa taarifa kwa umma!!!!?
Tuisadiane kutafakali hayo machache kwa sasa!
hUNA LOLOLTE ,BIBILIA HAINUKULIWI HIVO ,WAHUNI NYIE ,MANABII WA UONGO ! YALE SIO MAHUBIRI YA ASKOFU HATA KAMA PENGO ALIKOSEA!
Kwamba idea imesukwa na police
Jungle Warrior nawaheshimu sana watumishi na watu wa kada zote pia lakini sio gwajima n the like, sijui mzee wa upako nkMkuu unatafuta laana kwa kumdhalilisha mtumishi.
Pengo alishamsamehe, naamini na polisi watamuachia huru pindi akipona.
Ipo hivi mbinu za kutafuta habari kiitelijensia ziko nyingi, mko vijana kwa mfano kumi na zaidi mnapanga kuandamana siku fulani kwa sababu yeyote ile mnakutana mara mbili tatu lakini kukiwa na wengine wameongezeka msiowafahamu lakini wakiwa mbele kwa kuongea na kupanga mikakati, siku inafika mnaandamana mnakamatwa wote lakini mkifika selo wale wengine hawaonekani wameyeyuka! Ni mapandikizi
Kwa ishu hii iko hivi wanajitokeza watu mnaodhani mko nao pamoja wanaanzisha mada ya kumtor
inaitwa ENTRAPMENT,ama STING,
hii mbinu inatumika sana kwa vyombo vya usalama.kwahiyo wachungaji wakaingia mkenge hadi kufuata na begi la jamaa kwake,huh?
Jungle Warrior nawaheshimu sana watumishi na watu wa kada zote pia lakini sio gwajima n the like, sijui mzee wa upako nk
Gwjima ni muongo na tapeli mkubwa hilo liko wazi
- Yuko wapi Amina Chifupa aliyedai atamfufua? Ndugu na familia yake walijisikiaje kuona ndugu yao anadhalishishwa kwa malengo binafsi.?
- Iko wapi misukule yoote aliyoifufua? Unamfahamu yeyote kati yao walau mmoja tu?
- Anafanya biashara gani mpaka awe na utajiri na ukwasi wrote ule? Sadaka? Ni zake au ni kwa ajili ya kuhudumia wajane yatima na wenye shida?
-Alishirikiana na jeshi la polisi kuuhadaa umma kuwa mtesi was ulimboka alienda kwake kutubu! Kiongozi mkuu wa imani unashiriki uongo? Kwa ahadi ya kulindwa na utawala?
-Na hizi kashfa za kila siku za ngono nazo anasingiziwa?
Mpendeni na kumwogopa lakini pia yatafakarini maneno yahusuyo manabii na mitume was uongo katika Bible
Ulimi umemponza
Hilo la kijani ni buku au passport book?
Kova banaa!!!Kwa tamthilia za kusadikika ndiye mwenyewe hapo bado hajaingia kubwa la maadui Chagonja.
Does God exist?1. Gwajima amekosa heshima basic na hivyo anatupa shaka kama ni mtumishi wa mungu.
Lakini
2. Tutajuaje hiyo picha ni ya begi la Gwajima na si picha isiyohusika naye au iliyopandikizwa kwake?
Dogo huoni hiyo picha imepigwa baada ya polisi kupekua begi...inaonyesha wewe ni muhuni na jambazi na huo ndio mpangilio wa nguo katika bag lako
Jamaa mhuni tu hakuna cha kupoteza fahamu wala nini mhuni tu huyu jamaa hiyo pistol hospitali ya nini.Kumbe wala hakuwa amepoteza fahamu,hilo bag lisingeenda hospital bila maelezo yake kamili kwa walinzi wake.
Nadhani huyu Gwajima ni tapeli la kimataifa na inawezekana ana biashara nyingine haramu anafanya kwa mgongo wa kanisa. Lazima kuna kitu polisi wamemshtukia ndio sababu wanajaribu kumhoji na lazima tu ukweli utajulikana.
Usifikiri kila anayejiita nabii au mtume aliyetumwa na Bwana kama mtumishi wak na mwenye waumini wengi ni kweli ana nia ya kuhubiri neno la bwana na kuchunga kondoo wake. Wengine na matapeli, majambazi, Malaya na mafisadi wakubwa ktk nchi hii. Inabidi Polisi kuwa nao makini sina kufuatilia mienendo yao na vianzo vyao ya mapato maana sio sadaka tu inayowaingiza fedha nyingi hivyo kwa mara moja.