Inawezekanaje anang'atwa na nyuki waliokuwa wamemzunguka? Kuna siri gani??

Jchris14

JF-Expert Member
Aug 15, 2019
261
545
Habari za mida hii wanagenzi natumaini wote muko powa kabisa, kwa wale ambao afya si njema mkapate nafuu na kupona kabisa kwa uwezo wa mwenyezi Mungu.

Asubuhi nilipata wasaa wa kwenda kuangalia shamba kutokana na malalamiko mengi ya watu wakisema panya wamevamia mashamba kiufupi wanaharibu vibaya mnoo na ni wengi sana wanakula mahindi sehemu zote si yale ambayo bado yapo chini ya ardhi wanapita nayo kwa kuchimba na haya yanayoanza kuchomoza wanakula vibaya mnoo. Kwenye shamba la anko yangu wameacha visiki vya mahindi tu.

Na hadi muda huu hakuna anaejua hawa viumbe wametoka wapi, maana ni tatizo. Ok nirudi kwenye lengo la uzi, wakati napita kuelekea shambani kwangu nilimwona jamaa akiwa anavuna asali ya hawa nyuki wakubwa.

Sasa cha kushangaza huyu bwana alikuwa kavua na shati yaani kifuani yupo mtupu kabisa kabaki na suruali yake tu. Nikashangaa huyu jamaa nyuki hawamung'ati?? Maana kwa mbali kidogo niliona kabisa wakiwa wamemzonga kifuani na baadhi kichwani, ikabidi nipaze sauti kumuuliza kaka unahitaji msaada?

Cha kushangaza jamaa akasema hapana, hakuna shida kabisa na hao nyuki hawamung'ati. Sehemu ambapo alikuwa anavuna hio asali ilikuwa ni kakilima kadogo ivi na vichaka vichaka ivi japo sio vikubwa. Na hao nyuki walikuwa wametengeneza mzinga wao sehemu kama shimo ivi kubwa kubwa.

Sasa ikabidi nisimame kidogo kuangalia, jamaa akatoa likipande la mzinga likiwa limezongwa na nyuki, jamaa aliwafagia hao nyuki kwa mkono tu tena kirahisi tu kwenye hilo likipande la mzinga.

Sasa nauliza kwa wajuzi wa haya mambo inawezekanaje huyu jamaa hakuwa anang'atwa na hao nyuki?? Kuna namna ya kuwapoza au ni vipi maana nilimuuliza akasema hakutumia kitu chochote eti, na kingine cha kushangaza ni kwamba kuwa angevaa shati ndo wangemung'ata hahaaa!.
 
Nyuki anaweza akatua usoni kwako asifanye kitu mpaka pale unapoanza rusha mikono,they sense heat,they sense fear hivyo Jamaa kazoea anajua kuwa control.
 
Back
Top Bottom