HIVI NDIVYO NYUKI ANAVYOTENGENEZA GUNDI YAKE (PROPOLIS).

Fred Katulanda

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
374
509
rawpropolis-2017a_711x.jpg
Wengi tumesikia watu wakisema au kutaja Gundi ya Nyuki, ambayo kwa ufugaji wa Kisasa imeanza kuvunwa Kama zao la Nyuki pia tofauti na Asali.

Ili kutambua gundi hii hupatikanaje tunapaswa kujua kutokana na nyuki kuwajibika kuitunza asali au kulinda makazi yao, Mungu amewajalia uwezo wa kuzalisha gundi kujilinda.

Katika mfumo wa maisha yao nyuki wafanyakazi (majike) uhakikisha hakuna mdudu yoyote au kitu chochote kinaingia katika nyumba yao kuiharibu asali au kuwaua wao, watoto hata Malkia. Iwapo ikitokea kuwa kuna mdudu au kitu chochote kile, kimeingia kwenye mzinga au asali, basi nyuki watashirikiana kukishambulia kwa kudunga miba yao yenye sumu, lakini jitihada hiyo ikishindikana na kama adui mwenyewe ni mdogo basi watakitoa nje.

Lakini ikiwa kitu hicho au mdudu huyo ni mkubwa kiasi kwamba wao kwa uwezo wao wanashindwa kumtoa/kukitoa nje ya makazi yao, basi watatumia njia nyingine ya kuilinda asali na makazi yao. Kwa hatua hii watatengeneza ute (Bee Resin) na kuuchanganya na utomvu unaotokana na miti au baadhi ya mimea hivyo wataunda kitu kinachoitwa Gundi ambayo inatambulika kama #Propolis.
51XXU8slz5L.jpg

Propolis hii huwasaidia kuzuia maadui aina yoyote ile wasiharibu asali au kuvamia makazi yao. Sasa baada ya kutengeneza Propolis umzungushia mdudu huyo ute huo ambao ni gundi ngumu yenye rangi nyekundu, bila ya kubakisha upenyo hata mmoja, kwa unene wa milimita moja na nusu (1.5mm) ili kumkinga asitoke hapo na kufanya uharibifu wowote. Vilevile kama kutakuwa na nyufa katika mzinga wao, basi hutumia ute huo kuziba na ute huo, hivyo mara baada yaa kuuweka Ute huo unapokutana na hewa ya nje huganda mara moja na kuwa mgumu sana hivyo kuzuia baadhi ya wadudu wadogo au maadui wasiweze kuingia ndani ya mzinga.

Hivyo kwa ufugaji wa kisasa Propolis (Ngundi) huvunwa na kuuzwa kama bidhaa na hutumika kutengenezea dawa ya kutibu vidonda ijulikanayo kama Tincture.

Gundi hii imekuwa biashara kubwa kwa sasa kutokana na kuhusika kutengenezea dawa za ngozi za bunadamu au kuhusika kuongezwa kwenye mafuta ya kujipaka ikiwa ni pamoja na dawa za kupunguza msongo wa akili.
 
Back
Top Bottom