Bedroom yako ndio ikulu yako

Bedroom yako ndio ikulu yako

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
361,112
Reaction score
831,782
Kwanza nipende kuwapongeza mno na kuwasifia sana wale woote ambao huzifanya bedroom zao sehemu za kuvutia mno, ambapo hata mwenzi wako aingiapo pamoja na uchovu wote hupata mandhari tofauti na uchovu wote hupotea. hakika kuna watu ni wataalqm katika hili
bedroom kwa asilimia 99 unakuwa wewe na mwenzi wako tu,ni sehemu ya mazungumzo ya faragha, ni bustani yenu ya eden,ni mahali ambapo watoto au kizazi huendelezwa

Bedroom ni mahali ambapo uumbaji wa Mungu hujidhihirisha kwakuwa ni hapo tu mnaweza kuwa watupu kwa hiari yenu, bila kuoneana aibu wala haya, ni mahali ambapo mnajitenga na dunia na kubaki nyie tu wwawili, wa tatu akiwa MUNGU na wanne akiwa shetani
hivyo basi kutokana na unyeti huu bedroom yapaswa kupewa kipaumbele kikubwa mno, kuanzia kwenye usafi, rangi za mashuka na mito, aina ya godoro na mito, aina ya kitanda mapambo ya ndani nk

kama kuna sehemu tunapaswa kuwekeza sana ni bedroom, jitahidi iwe kubwa , yenye rangi zilizotulia, hewa ya kutosha na mpangilio wa vitu ndani, bedroom inapopendeza na kuvutia huleta very wonderful sensation ya mahaba na hata kama kuna shida mahali fulani hujikuta wote mmeisahau.

bedroom si ya kumpa mdada akusaidie kutandika au kusafisha,.bedroom haiachwi wazi ni sehemu maalum kwa nyie wawili tu, ni kama ikulu ilivyo strict kwa watu wengine
 
Bathi ni getto langu tu, linalo.........
Linalonipa......!
 
Na kama wakina sisi tumepanga chumba kimoja inakuwaje.
 
Na kama wakina sisi tumepanga chumba kimoja inakuwaje.

still u can make it, kuna mageto yanavutia mno, kwa usafi na mpangilio wake wa ndani wa vitu vyake, na wala si vitu vya gharama ni vya kawaida tu
 
still u can make it, kuna mageto yanavutia mno, kwa usafi na mpangilio wake wa ndani wa vitu vyake, na wala si vitu vya gharama ni vya kawaida tu
very trueeee.
So fresh so clean.
 
Back
Top Bottom