Bedroom diplomacy is urgently needed!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bedroom diplomacy is urgently needed!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Dark City, Mar 5, 2010.

 1. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Katika baadhi ya mijadala nimeshawishika kuamini kuwa watu wengi kwenye mahusiano wana mapungufu ya jinsi ya kuwasiliana. Kwa hiyo kuna ulazima wa kuwa na kungwi au wataalamu wa kutusaidia katika hili. Mimi siyo mmoja wao lakini naamini naweza kuwa na ushuhuda wa maisha yangu!

  Inaeleweka kabisa katika jamii zetu kwamba wanaume hunogesha maongezi yao wakati wanapata moja baridi na moja ya moto. Katika kikao cha namna hiyo hata mambo makubwa yanaweza kujadiliwa bila kuzua jazba. Je wanawake hongea mambo yao wapi na lini? Je mambo ya ndani (katika mahusiano) yanaweza kuongelewa wakati wowote na kwa lugha (pamoja na tune) yoyote?
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,231
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Wanawake wanaongelea mambo yao kwenye saluni za nywele, na huwa si kwa nia ya kujenga, bali kuweka petroli kwenye moto!...

  Pamoja na juhudi zote za kuandaliwa wakati wa kuyaingia maisha ya unyumba, hii haisaidii kitu, maana shughuli hizo(kitchen party, send-off etc etc) pia zinakuwa na dalili zote za kimeta!

  Kwa wanaume, ndugu yangu DarkCity, si wote wanahudhuria kwenye maeneo uliyotaja, labda tuseme tu kuwa wanaume wamejaliwa kipawa hicho cha uongozi toka mwanzo, na wanaweza kumaliza mambo mengi pasipo kucharurana.
   
 3. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,292
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  haya wazoefu!TWENDE KAZI...!mi nikichangia hapo nitakuwa mzushi
   
 4. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  [


  Itabidi waje wenyewe watueleze. Kwa nini wanaendekeza hicho kimeta!!


  Hapo ndugu yangu umeongea kama Bishop. Naamini mjadala haujafungwa.
   
 5. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 15,241
  Likes Received: 2,328
  Trophy Points: 280
  Unajua hii breakdown ya communication kwenye ndoa inaanzia wapi, nyingine ni hapa JF watu wamezoea kuambiwa asante hata kwa jambo la kipumbavu kabisa kwahiyo akienda nyumbani anataka mke au mume ammpe treatment kama za uku kwenye mtandao ambako unapewa asante saa nyingine hata na ibilisi maaanake bwana tusidanganyane hii ni mitandao tu kwahiyo chukua yale bora ya kipuuzi achana nayo na wengine comments zao za kifreemasons na watu wengine kwa upofu wao wa kuwaza wanazichukua hizo na kwenda kuziapply makwao, imekula kwenu.

  Kwa walionielewa wamenielewa kwa wasionielewa ooh! ooh! kidedea
   
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Nimejaribu kukuelewa lakini bado naona vinyota nyota. Bahati mbaya wadau wameshaanza mipango ya week end. Ngoja tusubiri labda tutapata mtu wa kutusaidia.
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Hebu rudi basi, mbona umetokomea? Bado tunahitaji vitu vyako, hata kama ni theory, uwanja wa kwenda kufanyia mazoezi siku hizi hulipii!!
   
 8. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #8
  Mar 5, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 15,241
  Likes Received: 2,328
  Trophy Points: 280
  uko mnjini ndio mnaanza weekend sio kwahiyo brain zimekaa kiweekend pia, ni jambo jema pia kwa afya ya mwili na akili
   
 9. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,776
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Ah mie wangu tunaongelea popote jikoni, bafuni na hata tukiwa tunacheza wenywe! hihi ihiih ihiihi
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...