Mcheza Karate
JF-Expert Member
- Jun 30, 2011
- 690
- 350
Sijapata bahati ya kukutana na mbunge wa Kilindi, Beatrice matumbo shellukindo lakini anastahili sifa hasa kwa kutafuta, kushughulikia na kutafutia suluhu matatizo ya wana kilindi.nimekuwa mtumishi hapa kilindi kwa miezi kadhaa lakini wenyeji wamenieleza mambo yalivyobadilika ndani ya uwakilishi wa shellukindo. Ametoa umeme kutoka wilaya ya Handeni hadi Songe(makao makuu ya wilaya ya kilindi), amepandisha hadhi barabara kadhaa na sasa ni barabara za mkoa sambamba na kuzifanyia matengenezo kwa kiwango kikubwa. Hayo ni machache sana, ameboresha michezo, kwa ushahidi kuna wakati aliniahidi vifaa vya michezo lakini kwa Bahati mbaya nikawa nimepatwa na msiba wa marehemu baba. Hivyo namba zake nikapoteza nikiwa safarini kuelekea nyumbani songea kwenye mazishi. Hivyo kushindwa kunipatia kwa kukosa mawasiliano. Shellukindo ni msikivu, hana dharau. Hivi wanaotaka kumchafua kwa kumwingiza kwenye makundi ni wanafiki na wauza magazeti tu. Waje kilindi waone aliyoyafanya. Kama kuna mtu anamfahamu zaidi yangu aeleze leo pasipo unafiki. Ila kwa ninavyomfahamu shellukindo, ikatokea kwa bahati mbaya leo atangulie mbele ya haki na nikapewa niandike tanzia naweza nikajaza hata kurasa 10.