Beating the Drum on One Side: Confusing the People on Both Sides

Sharif,

Bwa bayana kama hii,

Mimi nadhani mtu wa kwanza kupanga FOLENI KUNAKO MALIWATO NI HUYU MSAMBAA Nguruvi3...

Teh teh teh

Hebu mpatie kata ya kujitawazia kabla hajachafua hali ya hewa

Niwia radhi Kakangu,

Narakabisha kiduchu...Professor Nguruvi3 ni Mbondei wa Kicheba!

Tafadhali kifurusika, basi watake radhi ndugu zetu wa Kisambaa kwa kuwanasibisha na huyo Nguru wa Kicheba!

Ahsanta sana.
 
Hajat faiza Fox, al maarufu punjab Sing, Shariif Ritz ,Al akly THE BIG SHOW, na Al Alma Mohamed Said. Ahadi ni deni, na huwa sitoi kauli bila kuwa na msingi wa kauli hiyo.
Nipo tayari, nimekusanya makabrasha, panya wameyaparaza kidogo lakini sehemu za MS zipo intact. Ninakuja tuongee. Kabla sijamwaga kinachoitwa takwimu za Mohamed, napenda niwape kionjo kuwa mambo yamekaa uzuri, halafu jioni nawapa data zake. Zipo ili nina udhuru kidogo, nakwenda kuchukua madafu sehemu, jua kali
Niwaonyeshe kuwa Ms kafanya makosa mengi zaidi si ya logic bali ya upotoshaji. Nashangaa mnaposema Hirji ambaye amekiri kukosea mau mau na maji maji ametenda dhambi kuu. Hii ya Mohamed saidi si kuwa ni dhambi tu…

  1. Nilimuuliza Mohamed Said mwaka 2011, kutokana na kauli yake kuwa EAMWS iliuawa na wakatoliki na Nyerere, je ana ushahidi wowote.

Mohamed Saidi akajibu hivi: Ukisoma ukursa huo hakuna mahali paliposema Wakatoliki walishirikiana na Nyerere kuua EAMWS. Hii maana yake ni kuwa Mohamed Said ametunga hadithi kama kawaida, kaiweka kwa lugha nzuri akijua anapotosha. Sikuwa alighafilikiwa kwa maneno, bali alisema maneno yasiyo na ukweli na ukurasa ni shahdi.

Nitaendelea maana niliwaonya kuwa mzee atakaa karibu na uani


Sikuweza kuupload ukurasa, ninao hapa





Mkuu kuna vitu vingine viko open kabisa huhitaji kuambiwa ili uelewe au ujue.


EAMWS ilivunjwa na Nyerere na haihitaji elimu ya chuo kikuu kuelewa hilo.
 
Alhabiby G.S

Mantahofu nimeipata bayana yako,

Labda nikubali nasaha yako na niwaombe radhi ndug zangu WASAMBAA kwa kuwanasibisha na huyu Mbondei wa kicheba teh teh teh
Nguruvi3 mbondei huyu ana visa wallahi,,mwaka huu atakufa zake na kijiba chake cha roho,

Maskin alidhan anaweza safaria nyota ya Profesa Maji marefu wake kumbe looh ndiyo kajivua nguo moja kwa moja,

BILA SHAKA HIVI SASA YUKO MALIWATONI HUYU MIDA HII

TEH TEH TEH

Niwia radhi Kakangu,

Narakabisha kiduchu...Professor Nguruvi3 ni Mbondei wa Kicheba!

Tafadhali kifurusika, basi watake radhi ndugu zetu wa Kisambaa kwa kuwanasibisha na huyo Nguru wa Kicheba!

Ahsanta sana.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kuna vitu vingine viko open kabisa huhitaji kuambiwa ili uelewe au ujue.


EAMWS ilivunjwa na Nyerere na haihitaji elimu ya chuo kikuu kuelewa hilo.

Usiishie tu kusema vitu vipo open. Ingalikuwa ni vyema ukaja na facts za kukusuport kwamba EAMWS ilivunjwa na Nyerere. Lete vivid evidences usikurupuke.

Punguza mihemko mkuu hapa tunajadili kitaalam kwa facts, sio kilevi otherwise na wewe ubaki mshabiki.
 
Mkuu kuna vitu vingine viko open kabisa huhitaji kuambiwa ili uelewe au ujue.


EAMWS ilivunjwa na Nyerere na haihitaji elimu ya chuo kikuu kuelewa hilo.

CC Nguruvi3

Unaskia maneno hayo??

Sema wewe Lusungo,

Maaana tukisema sisi tunasemangwa kwamba ni VIJANA WA Mtalaam Mohamed Said teh teh teh

TUNAULIZA KWANI KUNA UBAYA??

SISI BINAFSI TUNAJISKIA FAHARI KUITWA VIJANA WA MTAALM KAMA HUYU,

WAO SIJUI WANAONA NI KEJELI??teh teh teh

KEJELI GANI TENA KUNASIBISHWA NA WASOMI JAMANI...

ha ha ha ha

BURDAN SANA.
Mohamed Said Mtaalam wetu Naona Profesa kakimbia moja kwa moja.
 
Last edited by a moderator:
Usiishie tu kusema vitu vipo open. Ingalikuwa ni vyema ukaja na facts za kukusuport kwamba EAMWS ilivunjwa na Nyerere. Lete vivid evidences usikurupuke.

Punguza mihemko mkuu hapa tunajadili kitaalam kwa facts, sio kilevi otherwise na wewe ubaki mshabiki.

Basi umepitwa na mengi Mkuu.

Huu sio mnaksha wa kwanza kufanywa humu JF kuhusu masuala kama haya,

Kma hujui sema ujuzwe usiishie kumshambulia mwenzako kwa ghilba na chuki zako.
 
Mkuu,

Nchi hii hivi sasa imeshakufa

Wasomi na wazalendo kama Kina Warioba wanapigwa na wachumia tumbo,

Wasomi wetu tuliowategemea kama Kina Hijr ndiyo hawa wanaomba radhi kwa kufanya kwao UTOTO,

Waandishi wa habari tulionao ndiyo kama hao Kina MANYENYERE JACKTON

YAANI NI BALAA JUU YA BALAA.
Kama ni mwaandishi wa habari BASI NI MAJANGA HAYO kwa jamii.

Mtu wa namna hii mwenye dhima ya KUIILIMISHA JAMII, na KUIHABARISHA jamii mambo ya kweli bila CHUKI wala Ushabiki anaandika bila kufanya utafiti japo kiduchu.

Inna Lillahi wainna ilaihi rajihunna.

 
Basi umepitwa na mengi Mkuu.

Huu sio mnaksha wa kwanza kufanywa humu JF kuhusu masuala kama haya,

Kma hujui sema ujuzwe usiishie kumshambulia mwenzako kwa ghilba na chuki zako.

Mkuu big show sina chuki wala ghilba kwa yeyote umu. Coz sina nnayemfahamu .

Inawezekana kweli mimi ni mgeni umu, ila sioni ubaya wa kutaka facts ili nijifunze.

Kama ata wewe unazo sio mbaya ukizileta.
 
Wanabarza,
Kuna mtu hapa yeye kaamua kuwa Launcelot Gobbo,
Ikiwa hamjui huyu ni nani aingie "Merchant of Venice," William Shakespeare.

Ananikejeli "name calling" ati mimi ni Mzee wa Boston.
Ugomvi hauko kwenye uzee.

By the way leo nimetimiza miaka 63.
Alhamdulilah.

Ugomvi uko hapo kwenye, "Boston."
Sasa namuongezea mji mwingine na atizame hii picha:

DSC03077.JPG


DSC03074.JPG


Hapo juu nipo UN Geneva.
Hiyo picha ni mashuhuri inaitwa "Broken Leg Chair."

Akipenda sasa na aniite Mzee wa Geneva au UN Geneva
au vyovyote vile.

Tutandendelea hivi In Sha Allah kila akitoa jina na mimi nampa mji mpya.
Nimepata kumuonya nikamwambia husda ni maradhi mabaya ya nafsi.

Mnakasha umenoga Faiza anadarsisha,
Mashaallah.

Angekuwa mwanamme ningempiga kilemba.

Kwa kuwa ni mama yetu namvisha ushungi wa hariri.
Allah amuongozee ilm na amjaalie umri tawil.


mimi mohammed ni kaka yangu sana kwa umri, elimu na ufikiri, lakini bado mimi hoja yangu iko pale pale, huwezi kuringa na maisha ya mfumo kristo na upande wa pili unaulanni mfumo huo huo nyumbani, mimi naona huu ni unafiki wa fikira unaokuja na dini, nasema dini siyo kisomo, kama picha hii ingekuwa saudia au yemen, au misri, kweli ningekubali kuwa huo mfumo kristo unamatatizo, mimi kwa kweli nashindwa, na ninashindwa kwa sababu mara zote wenzangu hawaja niconvince kuwa utawala wa wakristo na wazungu ni mbaya kiivyo, wao hawakai arabuni au nchi zenye uislamu wa kutukuta, na wakaringa kuwa oneni uislamu huo, imagine utajiri waote saudia, hata wakimbizi wa kiisilamu hawaendi. leo vita iko somalia, sudan nchi ya kiisalamu haina vita , lakini wasomali waote wanakimbilia kenya, tanzania , southa africa na kutafuta njia ya kwenda sweden , norway nk, siyo njia ya kwenda saudia. same na vita vya syria, wote italy, uingereza, ujerumani, saudia ata, hawataki, lakini kucha wakristo na wazungu wabaya, makafiri nk. mimi nilikuwa na kaka yangu marehemu sasa mungu amrehemu, yeye alikuwa engineer wa kutukuta, na akakaa sweden miaka ya 70, na akaajiriwa na kampuni ya pripps, hii kampuni ndiyo ilikuwa imepewa tenda ya kutengeneza mecca, mind you wa kristo ndiyo walifanya kazi hiyo , majengo , tiling, ablution facilities , air conditioning , sanitation nk, lakini kutwa hawa makafiri , hawa makafiri. ahsanteni, picha mumeiona kaka yangu yuko boston, kamkumbuka sana dada yake na anamlaani kwa nguvu zote mwanamke wa kizungu, ambaye baba na babu zake wametngeneza mazingara ya kumhifadhi, shukurani ya punda , mateke. hongera kaka, keep it up
 
Ni kweli banian mbaya kiatu chake dawa.

Huyu ndio mwasisi wa TANU, baba wa taifa letu Mwl JK Nyerere aliyemwezesha ata Mohammed Said kwenda shule aloitaifisha akafute tongotongo. Bila hivyo Sydney, ata Boston angeisikia kwenye bomba.

Kibandiko vipi? au hujakiona?
 
Usiishie tu kusema vitu vipo open. Ingalikuwa ni vyema ukaja na facts za kukusuport kwamba EAMWS ilivunjwa na Nyerere. Lete vivid evidences usikurupuke.

Punguza mihemko mkuu hapa tunajadili kitaalam kwa facts, sio kilevi otherwise na wewe ubaki mshabiki.

Then tell

Vivid eveidences? Facts or hypothesis from your so called learned Karim Bhai?

Vivid = intense, powerful

Prof. M.Said has given the vivid proof non hypothetical research.
 
Huu ni upotoshaji mwingine wa Mohamed Said. Kama kunaanyebisha kuwa si upotoshaji basi aje hapa tuongee naye. MS alishakubali kuwaalitetereka, sasa nasubiri dagaa Ndugu zangu, mumefungua pandora box,nitahangaika na MS machweo na mawio

Huna ujanja huo, wewe payuka tu, mara "makabrasha" mara "panya" mara "udhuru" mara "nimeyapata" mara "nitahangaika"...

Vipi takwimu za "hypothetical" za Mohamed Said ulizoahidi jana? au zimeliwa na panya?

Amma kwa hakika mfa maji haishi kutapatapa.
 
Usiishie tu kusema vitu vipo open. Ingalikuwa ni vyema ukaja na facts za kukusuport kwamba EAMWS ilivunjwa na Nyerere. Lete vivid evidences usikurupuke.

Punguza mihemko mkuu hapa tunajadili kitaalam kwa facts, sio kilevi otherwise na wewe ubaki mshabiki.

Hebu tupe zako japo kiduchu basi, naona unahororoja tu bila kuwa na chochote zaidi ya porojo.
 
hakuna kitu kibaya kama uwongo, kwani hata mimi ni mngoni, mama yangu kasoma kichwele, babu yangu alikuwa medical supertendent sewa haji (ocean road) kuanzia mwaka 1948, na kuna vitu vitatu ambavyo ni uwongo mtupu, kwanza kuna historia kubwa sana ya wakristo kwenye kupigania uhuru, pamoja na michango ya hela na vitumbua ya babu na bibi zetu, hata mission quarter kwenyewe kuna wazee wengi ambao walishiriki kwa nafasi zao , kwani ni eneo amablo wakristo wengi walikuwepo. hili kama linatakiwa kunadikwa litaandikwa kwani watu wako canada , uingereza na hata tanzania wanakumbuka vitu vingi, pili wangoni ni accomplinces wa vita vya maji maji, kwa matazamo wangu ni kama babu zangu waliingia kichwa kichwa vita vilivyoanzia kilwa na maeneo ya liwale has kutokana na mpango wa wajerumani kutaka kulima karanga na pamba, uwongo huu mnaoleta leo unakinai na haulipeleki taifa hili mbele, nimesoma shule hapa dsm na kwa macho yangu nimeona watoto wa kike wakiisilamu waki tolewa shuleni na baba zao kwenda kuolewa, na wengine waume kwa wake kukatazwa kwenda shule kwani "mtalishwa nguruwe" leo miaka hamsini lawama zimetoka bila hata kuangalia waliokataa kusoma kwa hiyari yao ni % ngapi na wanaonewa kwa utashi wa wakristo ni % ngapi, other waise nchi hii tunaipeleka kubaya. you may think you know everything, but dont be surprised tukikuambia you know nothing

Sasa si uilete hiyo historia ya babu zako na wazee wako tuisome, yanini unaandikia mate a wino unao?

You know everything, lakini tatizo linakuja pale unapoambiwa tuletee historia yako, unashindwa.

"Master of all trades, jack of none".

Hapo sasa.
 
Mkuu Nguruvi3 ikiwa African Assocition kilianzishwa na Bwana Abdulwahid Sykes mwaka 1929 kumbukumbu zangu zinaonyesha wakati huo alikuwa na miaka 5 tu je hili liliwezakana vipi ?.Kweli nimeamini Ustadhi Mohamed Said yupo daraja ya juu ya uongo.
Prof Ngongo.

Naona umeamua kwa makusudi kujitosa kwenye tope la maji taka bila kujali chochote.

Haya pata dasra hapa kiduchu.



Mohammed SaidBaada ya vita kuu ya pili (1938-1945) nchi nyingi zilizokuwa chini ya ukoloni hasa barani Afrika zilianzisha harakati za kudai uhuru.Uongozi uliokuwepo Tanganyika wa chama cha Waafrika kilichojulikana kama African Association wakati ule ulishindwa kabisa kubuni mbinu mpya za kupambana na utawala wa kigeni.Ili Tanganyika iende mbele ilikuwa ni lazima uongozi ule uondolewe madarakani. Sababu kuu za kuung’oa madarakani uongozi ni kule kushindwa kwake kupambana na mabadiliko ya siasa yaliyokuwa yakitokea dunia nzima.Harakati za Waziri Dossa Aziz na kuweka wazi mali yake ili kupambana na dhuluma za Serikali ya Kiingereza katika Tanganyika zinaanza wakati huu. Dossa wakati ule alikuwa kijana mdogo wa miaka 25.Ili aweze kupata picha halisi ya siasa katika mji wa Dar es Salaam ni lazima msomaji afahamishwe hali iliyokuwepo Dar es Salaam katika miaka ya 1950.Katika mji wa Dar es Salaam ya miaka 1950 kulikuwa na koo mbili maarufu. Ukoo wa Azizi Ali baba yake Dossa, Ramadhani na Hamza Azizi na ukoo wa Kleist Sykes baba yao Abdul-wahid (1924-1968), Ally na Abbas Sykes.Wazee hawa wawili walikuwa marafiki na urafiki huu ulienea hadi kwa watoto wao. Watoto wao wakafanya mengi pamoja katika harakati za kudai uhuru wa Tanganyika; na ndiyo maana haiwezekani ikaelezwa habari za Dossa bila kugusa habari za akina Sykes.Halikadhalika haiwezekani yakaandikwa maisha ya Nyerere au historia ya uhuru wa Tanganyika na mwandishi akapuuza mchango wa watu hawa. Watoto wa koo mbili hizi, Dossa akiwakilisha ukoo wa Azizi Ally na Abdulwahid na Ally Sykes wakiwakilisha ukoo wa Sykes ndiyo mwaka 1950 waliohusika na mapinduzi ya kuung’oa madarakani uongozi wa African Association wa wazee uliodumu kuanzia mwaka 1929 hadi 1950 rais wake wa mwisho akiwa Mwalimu Thomas Sauti Plantan.Muhimu katika mazingira ya siasa za wakati ule ni kuwa hakuna chochote ambacho kingeliweza kufanyika Dar es Salaam katika jitihada ya kupambana na Serikali ya kikoloni bila ya msaada wa Dossa na watoto wa Kleist Sykes kwa sababu hawa walikuwa kwanza na elimu ya kutosha na pili walikuwa na hazina ya kuendesha harakati za siasa.Kleist Sykes (1894-1949) alikuwa mwajiriwa wa Tanganyika Railway kama mhasibu. Kleist alikuwa mwanasiasa muasisi wa African Association (1929) na Al Jamiatul Islamiyya (Muslim Association) (1933) katika miaka ya mwisho ya uhai wake Kleist akawa mfanyabiashara maarufu.Azizi Ally alikuwa mkandarasi wa kujenga majumba. Lakini kwa kuwa Azizi Ali alikuwa Mwafrika wakoloni walimbagua wakakataa kumpa leseni ya ukandarasi wa daraja la juu ambayo ingelimwezesha kujenga majumba makubwa ya ghorofa. Leseni hizo walipewa Wahindi na Wazungu. Juu ya ubaguzi huu wote baba yake Dossa alifanya kazi ya ujenzi na akatajirika katika biashara kama alivyotajirika rafiki yake Kleist. Mali hii ndiyo iliyokuja kuwa mtaji wa kwanza waliotumia Waafrika wa Tanganyika katika miaka ya mwanzo kuanzia harakati za kudai uhuru.Wakati ule mtu hakujiingiza katika siasa ili anufaike binafsi. Nafasi hiyo haikuwepo kwa kuwa hakukuwa na fedha katika siasa. Kila aliyeingia katika harakati aliingia kwa uchungu na mapenzi ya nchi. Kama alikuwa na mali basi aliingia ili atoe mali yake kuikomboa nchi. Kama hana mali basi alijitolea chochote katika vipawa alivyojaaliwa.Dossa aliingia katika harakati za siasa mwaka 1950 siasa ikiwa katika hali hii. Aliingia katika African Association na uongozi mpya wa vijana miongoni mwao akiwa Abdulwahid na Ally Sykes, Hamza Mwapachu (1918-1962), Tewa Said Tewa (1924-1998), Dk. Vedast Kyaruzi, Dk. William Mwanjisi, Dk. Luciano Tsere, na vijana wengine ambao ingawa hawakuwa Watanganyika walishiriki kikamilifu katika harakati za kudai uhuru. Hawa walikuwa Dennis Phombeah kijana wa Kinyasa kutoka Nyasaland (Malawi), Patrick Aoko na Dome Budohi kutoka Kenya na vijana wengine wengi.Dossa aliguswa na madhila ya ukoloni kwa dhahiri yake mwaka 1947. Dossa pamoja na mtoto mmoja wa Mwarabu tajiri aliyekuwa akiishi Dar es Salaam, Ali Mmanga walichaguliwa kuhudhuria mahojiano Nairobi kwa ajili ya kozi ya urubani wa ndege. Walipowasili Nairobi wakoloni walikataa kumfanyia usaili Dossa kwa sababu alikuwa Mwafrika. Dossa alifahamishwa kuwa yeye kama Mwafrika hastahili kupewa ujuzi wa kurusha ndege. Dossa alifadhahika sana na alimweleza mwandishi wa makala hii kuwa alipiga simu kwa baba yake na akawa analia machozi kwa uchungu. Kwa kumuonea huruma baba yake alimtumia fedha ili anunue gari pale Nairobi kama zawadi ya kumfajiri. Hii ndiyo ilikuwa gari ya kwanza kuwa nayo Dossa na aliitumia hadi 1955 alipoitoa kwa TANU ili itumike kwa ajili ya kudai uhuru.Lakini Dossa alipokwenda Nairobi alimkuta Ally Sykes yupo mjini hapo na tayari alikuwa akifahamiana na wanaharakati wa Kenya kama Jomo Kenyatta, W.W. Awori, Tom Mboya na wengineo. Ally alikuwa akihudhuria mikutano ya siasa ya Wakikuyu iliyokuwa ikifanyika kwa siri Limuru.Ally Sykes alimchukua Dossa katika moja ya mikutano ya hadhara ambao Kenyatta alikuwa anahutubia katikati ya Nairobi sehemu moja ijulikanyo kama River Road. Aliyoyaona pale yalimtosheleza kabisa Dossa kujua kuwa Tanganyika ilikuwa imechelewa katika harakati za kudai haki yake. Waafrika wa Kenya walikuwa wamefikia hali ya kuzungumza siasa kwenye majukwaa wakati Waafrika wa Tanganyika walikuwa bado wakifanya mikutano yao ndani ya kiofisi kile kidogo cha African Association chini ya uongozi dhaifu wa Thomas Plantan akiwa kama Rais na Clemet Mtamila kama Katibu. Dossa alifikisha yote aliyoyaona Kenya kwa wenzake.Mzee Dossa alimfahamisha mwandishi wa makala hii kuwa ni katika kipindi hiki kati ya mwaka 1947-1950 ndipo njama za kupindua uongozi wa Africa Association zilipoanza washiriki wakuu wakiwa yeye mwenyewe Dossa, Abdulwahid na mdogo wake Ally na rafiki yao Hamza Kibwana Mwapachu. Huku akicheka Mzee Dossa alimfahamisha mwandishi kuwa:"Ilikuwa kutokea Tanga Club, Club mahsusi ya vijana wasomi Waafrika iliyokuwepo New Street (hivi sasa Lumumba Str.) si mbali sana na ofisi ya African Association ndipo Abdulwahid na Hamza Mwapachu walipoivamia kwa nguvu ofisi ya African Association na kufanya mapigano ambayo yalimfanya Katibu Mzee Mtamila apigwe na kutupwa nje ya ofisi".Dossa anasema yeye ingawa alikuwa anauchukia ule uongozi wa wazee hakuwa na moyo wa kuwatoa wazee wale kwa nguvu na kwa taadhira, kwa ajili hii basi alibaki nje akawa anaangalia sakata ile kwa mbali. Uchaguzi ulifanyika na wazee wakang’olewa madarakani. Dk. Kyaruzi akachaguliwa Rais na Abdulwahid akiwa Katibu wake.Kuanzia wakati huu mikutano ya siasa ikaanza kufanyika Ilala Commuity Centre ambako Hamza Mwapachu alikuwa akifanya kazi kama Assistant Welfare Officer. Nyakati za jioni mijadala hii ikawa inahamia nyumbani kwa Dossa Mtaa wa Mbaruku Gerezani au Tanga Club, Agenda kuu ikiwa namna ya kuwaunganisha Watanganyika chini ya chama cha siasa ili kudai uhuru.Mwaka wa 1950 Gavana Edward Twining alipoteua Kamati ya Katiba (Consitutional Development Committee) ili kukusanya mapendekezo ya Waafrika ni vipi wangependa katiba ya nchi iwe, Dossa alisema kuwa hapo ndipo Waingereza walipopata kwa mara ya kwanza kuhisi kuwa uongozi mpya wa vijana katika African Association ulikuwa umepania kuleta mabadiliko katika nchi. Uongozi wa akina Dossa uliihimiza Serikali ya kikoloni kuhusu umuhimu wa kuwa na uwakilishi wa Waafrika katika Baraza la Kutunga Sheria, uwakilishi wa kuchaguliwa na wananchi wenyewe badala ya ule uwakilishi wa kuchaguliwa na Gavana rangi ya mtu zaidi kuliko sifa nyingine yoyote.Kipindi hiki cha mwaka 1950-1954 kilikuwa kipindi kigumu sana kwa kuwa kwanza chama kilikuwa hakina fedha kikitegemea sana msaada wa Dossa. Wakati ule chama kilitegemea sana fedha za Dossa katika shughuli za kuendesha ofisi na gari yake katika kutimiza majukumu yake ya kila siku.


Prof haya tuwekee hizo kumbukumbu zako.
 
Last edited by a moderator:
naamini wakati umefika, bahati mbaya itachukua muda lakini tutafanya juhudi kubwa kuanza kuweka vitu sawa, najua wakati mwing umepita lakini archives ziko, wazee wachache wapo, watoto wasikivu na simulizi wapo. Lakini natoa angalizo ambalo lina methali moja , its an early bird who enjoy the fruits, Historia ya ku repeat inakuwa na matatizo makubwa sana ni heri kusahihisha historia iliyopo kulioko kuanza kufanya review ya mambo ya miaka ya hamsini au arobaini, hatari zake na athari zake wakati mwingine huwa hazifutiki.

Ungana na Yericko Nyerere na Mzee Mwanakijiji na Nguruvi3 na Mag3 na wengineo waliosema kama usemavyo wewe na wakaahidi watajumuika kuja na ukweli kuupinga na kuugaragaza huu "uongo" wa Mohamed Said.

Leo takriban miaka mitatu, kimyaaaaaaa. Wengine hata kupitia minakasha ya Mohamed Said wanaogopa kwani wanajuwa wataulizwa, vipiiiii?

Nakuuliza swali moja, umewahi kumsikia Mshume Kiyate?
 
Last edited by a moderator:
Maneno hayo unayema wewe,

WE NANI KAKUAMBIA MOHAMED SAID AU HATA WAISLAM WANASEMA MAKAFIRI NI WATU WABAYA??

NANI KAKUAMBIA??AFTER ALL KAFIRI SIYO TUSI NI NENO TUH LA KAWAIDA LINALOMAANISHA MTU ASIEAMINI KWAMBA ALLAH NI MUNGU NA MUHAMMAD NI MTUME WAKE HUYO NI KAFIRI..WALA SIYO TUSI,

MIMI BINAFSI NINA RAFIKI ZANGU WAKRISTO NA WA IMAN ZINGINE AMBAO SIYO WAISLAM NA TUNAISH NAO VIZUR SANA,,

KWA UPENDO NA AMANI

WAPO BAADHI YAO WABAYA NA WAPO BAADHI YAO WAZURI MNOO KITABIA TENA HATA KUSHINDA BAADHI YA WANAOJINASIBU NA UISLAM, NA WAISLAM

USITUWEKEE MANENO YAKO MDOMONI MKUU

HATUPO HAPA KUHUBIRI CHUKI AU KUBEZA WATU WA IMAN ZINGINE,,KAMA UTAKUWA UNAWAZA HIVYO BASI UTAKUWA UMEPOTEA SANA KIFIKRA

SISI NI WATANZANIA NA HAPA TUNADISCUSS KUHUSU HISTORIA YA NCHI HII,,HAKUNA LA ZAIDI

KAMA UNAWAZA SISI TUNADISCUSS CHUKI UMEPOTEA SANA
mimi mohammed ni kaka yangu sana kwa umri, elimu na ufikiri, lakini bado mimi hoja yangu iko pale pale, huwezi kuringa na maisha ya mfumo kristo na upande wa pili unaulanni mfumo huo huo nyumbani, mimi naona huu ni unafiki wa fikira unaokuja na dini, nasema dini siyo kisomo, kama picha hii ingekuwa saudia au yemen, au misri, kweli ningekubali kuwa huo mfumo kristo unamatatizo, mimi kwa kweli nashindwa, na ninashindwa kwa sababu mara zote wenzangu hawaja niconvince kuwa utawala wa wakristo na wazungu ni mbaya kiivyo, wao hawakai arabuni au nchi zenye uislamu wa kutukuta, na wakaringa kuwa oneni uislamu huo, imagine utajiri waote saudia, hata wakimbizi wa kiisilamu hawaendi. leo vita iko somalia, sudan nchi ya kiisalamu haina vita , lakini wasomali waote wanakimbilia kenya, tanzania , southa africa na kutafuta njia ya kwenda sweden , norway nk, siyo njia ya kwenda saudia. same na vita vya syria, wote italy, uingereza, ujerumani, saudia ata, hawataki, lakini kucha wakristo na wazungu wabaya, makafiri nk. mimi nilikuwa na kaka yangu marehemu sasa mungu amrehemu, yeye alikuwa engineer wa kutukuta, na akakaa sweden miaka ya 70, na akaajiriwa na kampuni ya pripps, hii kampuni ndiyo ilikuwa imepewa tenda ya kutengeneza mecca, mind you wa kristo ndiyo walifanya kazi hiyo , majengo , tiling, ablution facilities , air conditioning , sanitation nk, lakini kutwa hawa makafiri , hawa makafiri. ahsanteni, picha mumeiona kaka yangu yuko boston, kamkumbuka sana dada yake na anamlaani kwa nguvu zote mwanamke wa kizungu, ambaye baba na babu zake wametngeneza mazingara ya kumhifadhi, shukurani ya punda , mateke. hongera kaka, keep it up
 
Back
Top Bottom