Jamani utabiri wa Mtumishi wa Mungu(hata kama hamtaki) T.B.Joshua zote huwa ziko wazi na recorded, ukizihitaji unazipata, sasa hiyo ya EL kutabiriwa uraisi 'live' mwenye nayo aweke humu! Ninachojua humu huyo mbunge mwanamke ndiye huwa anasimulia hilo, aweke clip yake basi! Lkn nikuambie kitu kingine, ili Mungu afanye muujiza wake kwako kuna masharti yake lazima uyakubali, uyaishi na kuyatenda pasi kupunguza hata kidogo. Mbili tatu kati ys hizo ni:1-Utakatifu,2-Kumtegemea yeye tu,3-Utauwa etc na mengine mengi. Huwezi(hata kama umetabiriwa) kupata kile ulichotamkiwa huku ukitegemea akili zako mwenyewe Mfano Jemedari Naaman,Mfalme Sauli, Sensa ya Mfalme Daudi na wengine wengi. Kwa hiyo, huyo EL mambo ya kutegemea akili, uwezo, mtandao,rupia etc kama amejihusisha lile tamko la baraka linakuwa kinyume chake! Mungu ni yeye yule Jana,Leo na Siku zote. Naongeza; Mungu hadhihakiwi.