(Be forward) Bei hizi za magari mitandaoni zipo sahihi kweli?

PureView zeiss

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
9,092
29,857
Yapata miezi 3 sasa nimekuwa nafatilia bei za magari hasa mitandaoni pamoja na kwenye yards mbalimbali ili kujua uhalisia wa bei.

Kitu ambacho kimenishangaza kidogo mitandaoni ni namna bei zake zilivyokuwa cheap,mwezi iliopita nilienda yard moja pale manyanya kinondoni ili kujua tu bei ya athletes crown nikaambiwa ni tsh milioni 18 hadi 22.

Baada ya kuingia online kucheki bei zao hasa kwenye site ya BE FORWARD nimekuta bei za crown ni USD 1500,1700,1900 hapa nilishangaa hizi bei nikajiuliza inakuaje haya magari kwenye yards yanauzwa bei ya kufa mtu? Kwa wale wenye uzoefu wa manunuzi ya online kuanzia magari na vitu vingine watanisaidia juu ya hizi bei je zipo sahihi?

Ukiachilia mbali ushuru bandarini pamoja na tra inakuaje gari hizi kwenye yards zetu zinapigwa sana bei ya juu?je magari haya kwenye mitandao yanauzwa bei chee kwasababu ya mileage kubwa?
 
Screenshot_2018-08-18-09-56-18.png
 
Unapoona bei ya gari mtandaoni ongeza na usafiri mpaka Dar halafu uangalie na ushuru wa serikali hapo ndio utapata picha kamili kwanini bei zinakuwa juu hivyo zikiwa showrooms

Kodi ni nyingi mno especially gari linapokuwa limetumika zaidi ya miaka 10

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Nenda Kwenye Kodi Utalia Mwenyewe...kujua Kodi,hiyo Bei zidisha mara 2
Wakati $ni Approximately Tsh 2280.

2280*2858=kama 13million hivi, Sasa Wewe unaona ni Rahisi na Hiyo Kodi? Unless wewe uwe ni Marketing officers, executives,wa Be forward JP Tanzania, hivyo unawapa Promo kiaina!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unapoona bei ya gari mtandaoni ongeza na usafiri mpaka Dar halafu uangalie na ushuru wa serikali hapo ndio utapata picha kamili kwanini bei zinakuwa juu hivyo zikiwa showrooms

Kodi ni nyingi mno especially gari linapokuwa limetumika zaidi ya miaka 10

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
Hizo habari za kusema eti gari iliyotumika miaka zaidi ya 10 inakua na kodi kubwa si kweli kabisaaa.

Jaribu kwa mfano: toyota rav 4 2006 vs toyota rav 4 2015 zenye same specifications utapata jibu.,jaribu na other brands ujionee. Calculator ya TRA itakupa majibu mpk utashangaa.

Inshort,kodi ya gari za miaka ya karibuni ni kubwa mara dufu kuliko kodi ya magari ya zamani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nenda Kwenye Kodi Utalia Mwenyewe...kujua Kodi,hiyo Bei zidisha mara 2
Wakati $ni Approximately Tsh 2280.
2280*2858=kama 13million hivi,
Sasa Wewe unaona ni Rahisi na Hiyo Kodi?
Unless wewe uwe ni Marketing officers, executives,wa Be forward JP Tanzania, hivyo unawapa Promo kiaina!

Sent using Jamii Forums mobile app
Si kweli hio crown iliyotajwa hapo juu na mtoa mada kodi yake kwa mujibu wa TRA ni 6.8mil uki plus gharama za clearing na nyingine tu-assume ifike hata 8.5mil.

8.5mil + CIF ya $1500 haiwezi kufika huko kwny bei za yard za mil18-20

Inshort yard ni maumivu matupu na ni kwa ajili labda ya watu waoga/wasiojua habari za ku-order online na watu wanaotaka magari fasta(uvumilivu wa kusubiri gari toka japs hawana.)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mng'ato,
hiyo USD 1500 sio CIF (cost, insurance and freight) bali ni bei ya gari pekee (cost). CIF itakua juu inaweza kufika hata mara mbili ya hiyo cost, na TRA ndio wanayoitumia kukokotoa kodi.
 
Ukitaka kujua gharama halisi ya gari kama unaagiza kutoka nje. Ingia mwenye website ya TRA ingina sehemu imeiandikwa calculators kisha used motor vehicles calculators kisha ingiza details za gari unayotaka kuagiza pale utapata hesabu za kodi unayotakiwa kulipa.

Hiyo total jumlisha na gharama ya gari huko unapoagiza ndio jumla ya hela itakayokutoka mpaka uimiliki hiyo gari.

Usione gari mtandaoni inauzwa USD 1500 ukajua umeula.

Link hii hapa

Used Motor Vehicle Valuation System - Used Motor Vehicle Valuation System
 
mng'ato,
yap yap hayo mambo sijui ya miaka 10 ndo bei kali haya exist kwa TRA according to navyotumia calculator yao kila siku bei ya kodi huwa kubwa navyosogea miaka ya karibuni na sio unavyoshuka chini mfano prado4th ya kwanza 2009 kodi ni 30m na unavyopanda karbu kodi inakuwa maradufu mfano la 2014 ni kama mil 38-39 almost 40m as a kodi
 
Nenda Kwenye Kodi Utalia Mwenyewe...kujua Kodi,hiyo Bei zidisha mara 2
Wakati $ni Approximately Tsh 2280.
2280*2858=kama 13million hivi,
Sasa Wewe unaona ni Rahisi na Hiyo Kodi?
Unless wewe uwe ni Marketing officers, executives,wa Be forward JP Tanzania, hivyo unawapa Promo kiaina!

Sent using Jamii Forums mobile app
sio kweli kwanza kodi haizidishi mara mbili hata hayo magari yenye miaka 10 + mfano ka ist cha 2003 unaweza kukipata kwa 5.3m had bandarin then kodi 4.5

na hata hayo ma crown bei ya kawaida 12-14M za 2006 kurud nyuma
 
Hapo kwny web ya be forward kuna Crown mpk CIF yake ni $1682 mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtoa mada ahakikishe hiyo bei ya gari mtandaoni ni CIF na sio FOB. Hiyo dola 1500 iliyotajwa ya Crown yenye namba ya utambulisho BF936053, gharama yake (kabla ya freight, bima na inspection) ni $1525. Ukiweka hizo gharama nyingine, bei yake (CIF) ni $2979, roughly sawa na Tsh 6.8mil.

Ushuru wake TRA ni Tsh 6,802,593/-. Ukiangalia bei kwa njia ya simu (smartphone) kwenye site ya Beforward, huwa unaona FOB pekee. Ili kupata bei halisi, ni hadi uombe quotation. Mimi nitamshauri mtoa mada, aagize gari toka Japan. Nilishafanya hivyo na huu ni mwaka wa 4 nalitumia. Ingawa atalisubiri kwa wiki 4-6, bado ataokoa milioni kadhaa. Hiyo ya $1600 nimeiona pia.
 
Nakubaliana na vitu vingi hapa kwny bandiko lako mkuu lkn hapo uliposema ukitumia smartphone kwny site ya be forward unaona FOB pekee sio sahihi mkuu.

Kuna sehemu ya ku select nchi inakuletea mpk CIF Mkuu(hata kama unatumia smartphone kwny hio web ya be forward).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
yap yap hayo mambo sijui ya miaka 10 ndo bei kali haya exist kwa TRA according to navyotumia calculator yao kila siku bei ya kodi huwa kubwa navyosogea miaka ya karibuni na sio unavyoshuka chini mfano prado4th ya kwanza 2009 kodi ni 30m na unavyopanda karbu kodi inakuwa maradufu mfano la 2014 ni kama mil 38-39 almost 40m as a kodi
Swadakta kabisaa mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakubaliana na vitu vingi hapa kwny bandiko lako mkuu lkn hapo uliposema ukitumia smartphone kwny site ya be forward unaona FOB pekee sio sahihi mkuu.

Kuna sehemu ya ku select nchi inakuletea mpk CIF Mkuu(hata kama unatumia smartphone kwny hio web ya be forward).

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimeona mabadiliko. Kipindi cha nyuma walikuwa wanaonesha FOB pekee. Imebidi niangalie tena naona sasa wanaonesha vyote.
 
Back
Top Bottom