Be Forward wamekuwa wajanja na waongo, magari yanaletwa mabovu

Papatu-Papatu

Member
Mar 19, 2024
33
168
Wakuu natumai mu wazima!

Kuna wimbi la Be Forward kuleta magari mabovu ambayo yanasabibisha usumbufu mkubwa kwetu sisi wateja.

Nimenunua Alphard- nikaambiwa imefanyiwa mpaka na Inspection, na tena Be Forward Tanzania ndio walifanya clearance. Sasa cha ajabu gari imefika inavuja oil, pia imepigwa rangi nyeusi kumbe Original color ilikuwa ni Nyeupe, ikabidi tena ifanyiwe service hapa Tanzania kwenye yard ya Be Forward ndio TBS wakaipitisha.

Lakini gari bado ina matatizo mengi sana ya check engine, rejeta, masega na Engine box. Nimejaribu kufuatilia Be forward Tanzania wananijibu sababu niliagiza moja kwa moja Japan na Singapore hiyo haiwahusu. Nimefuatilia ilipotoka wananizungusha bila majibu ya kueleweka. Sasa nimeishia kupaki gari sababu haina nguvu na injini inachemsha.

Naomba mnisaidie kama kuna mwenye ushauri wa nini cha kufanya.

Asanteni wakuu.
 
Kuna siku mtu alileta uzi akasema: Kabla haujalipia gari kutoka Japan (mfano Beforward) omba upewe zile karatasi mbili, (1) Auction Sheet na (2) Condition Report/Form.

Matatizo yoote uliyoyasema yapo Alphard inamaanisha yangekuwepo yametajwa kwenye izo documents.

Kama haukuomba sasa iyo issue nyingine.

Hafu, kwanini TBS wanapitisha gari huku, si uwa wanamaliza inspection Japan? Au umeagiza from Singapore.?
 
Ilikuwa Singapore Mkuu ila kupitia ofisi yao ya Japan na Tanzania.
 
Weka na gharama ulizotumia ili tujie bureghali au huduma yao mbovu ?
Gari mpaka kufika 26M, mbali ya ushuru. Ilipofika tu service kwenye yard ya Be Forward ilikwenda zaidi ya 250,000 maana TBS walikataa kurelease gari. Baada ya gari kutoka nimelipeleka gereji nyingi sana na nimetumia zaidi ya 10,000,000 kujaribu kulirepair lakini wapi. Mpaka nilinunua Gear Box mpya lakini wapi.!
 
Back
Top Bottom