BBS ya mwaka 2012 imepooza sana.

BBS ya mwaka 2012 imepooza sana.

katika wote Walter ndiye wa ukweli kuliko hata sifa anazobebeshwa Wababa. Walter anaimba ametulia na hata uchaguzi wa nyimbo zake ni kiboko lakini mtindo wa kupanga matokeo unawafanya wampigie upatu Wababa zaidi na ni katika mtindo huo huo Norman aliondolewa.

Pili Husna kaondoka lakini nakwambia alikuwa mzuri kuliko Nsami aliyeimba kizembe wimbo wa kuboa sana na matumizi yake ya steji ni zero. Husna pia alimpiga fimbo Salma (kipenzi chao anayeandaliwa kuchukuwa hiyo 50M). Ni kweli kabisa kuwa Huyu Salma ni mbovu hata Salama leo kamkataa. Ni binti anashindwa hata kutamka maneno yanavyotakiwa ana'kithembe' na anaimbia puani. Kila siku anajificha nyuma ya gitaa. Yaani akiambwia kuimba live hata top 20 hakustahili kabisa! Hamna noma mchagueni tu huyo binti wenu wa EPIC ili mgawane naye hizo 50.



Kama nilivyosema hapo mwanzo hakuna zaidi ya Walter Chilambo; haya tunasubiri walete upuuzi kwamba kura hazikutosha. Yaani watu wamevamia jukwaani mpaka hapatoshi!! Huyu guitar girl kaaribu kabisa na wimbo wa mwisho ndio umemuonesha alivyo hana kitu zaidi ya kubebwa na upigaji wa guitar. Madam rita mpe walter hela yake basi ili urejeshe imani kwa watu vinginevyo BSS mtaaibika sana leo Hakuna ubishi hata kwa mtu asiyejua mziki. The decision is as clear as anyone can see!!
 
Back
Top Bottom