NATTA WITO
JF-Expert Member
- Jun 5, 2013
- 228
- 97
Haya ni matokeo ya sera za kipuuzi za hao hao waingereza na mabepari wenzake. Walituhadaa tukaamini ubepari ndiyo jibu. Kwa mtindo huu, kama mtoto, ama hana wazazi na qalezi, au anao lakini hawana uwezo, lazima aingie kwenyw hii mnayoona ni child labour. Hali si mbaya kama bbc wanavyouaminisha ulimwengu. Hili ni la dunia nzima.
Manyerere Jackton vp? Unatafuta fungu la TanzaniteOne nini?
Manyerere Jackton inaonesha ameumizwa na habar ya BBC ila hajaumizwa na vile watoto wanavyotumikishwa,kila jambo likitangazwa na medi za nje zinaitwa propaganda,kuna ujangil hapa,ila watu wa uingereza walivyoripot tukaambiwa propaganda,sasa kama waandishi wa ndan wamefeli si waandishi wote wamefeli,waandishi wanaojua wajibu wao wameripot,na huu ndo uwandishi,na hizi ndizo habar zinazopaswa kuibuliwa,ili watu wachunguze sera na mianya ya sheria
Haya sasa matusi! Suala la ajira mererani kwa watoto si kubwa wala la kulazimishwa. Kuna watoto nilibaini wamefiwa wazazi wote. Hao wanaingia pale kuchakuachakua kama ilivyo sehemu nyingine. Ninachokataa ni kile cha kuonesha kama child labour ya pale ni jambo lililobarikiwa na vyombo husika au na matajiri wa migodi.
Ndo yale yale ya Darwin's Nightmare ya mapanki, watu wanaandamana hawali mapanki kumbe watu tunakula balaa kisa mtoa filamu ni mfaransa.Hao BBC wasichoke kuumbua maana waandishi wetu wengi ni makanjanja kama alivyosema Ridhiwani.
Mkuu hbii mambo ya sera mbaya tuliletewa na kama hayo ni old stories tangu enzi za SAP yaani tunalalama kama vile sisi ni "tabula rasa" kabisaaaa.......hatuna ubongo wala akili......????!!!!
Haya tumegundua mbaya nini kinafanyika kurekebisha!!!?????
Hilo la mzazi kukosa uwezo nalo ni la kulalamikia watu wa nje wakati wazazi wengine wanachukua posho ya siku kubwa kuliko mshahara wa mzazi mwingine kwa mwezi....huu nao ni ushauri wa nje!!!?????
Hali ya ustawi wa watoto yaweza kuwa mbaya kuliko ilivyooneshwa na BBC mkuu, kama hatukubali uwepo wa shida ni vipi tutaanza kushughulikia???????!!!!!
jana nimeiona hiyo habar,kwanza tusianze kuwasingizia makaburu,bbc wameonesha kinachoendelea,la pili ajira kwa watoto hapa Tanzania zipo,mashamban,migodini,mbona kila jambo tunakimbilia kusingizia?kwa sababu suala la NYOKA kule mereran ni la muda,a ILO imeshawai kutoa ripot za child labor in Tanzania,kwa miaka ya nyuma,me nnayo hiyo report ukipenda nipe e-mail nikutumie leo,ifike wakat tusisake mchawi jaman,
Mererani we huijui,The Boss, hujui kitu. Watoto wapo nje wanaokota tu. Hakuna anayeingia shimoni. Nimekaa miezi miwili pale sikuona mtoto "nyoka" akizama chini. Wanaozama ni wana-apollo.
nHivi kwa maono yako kuna serikali ya kuwasaidia hawa watoto? Nani awapeleke shule? Hata marekani haijaweza na ndiyo maana inao wasiojua kusoma wala kuandika. Kama kujifungua tu hatuwezi kugharimia, hiyo shule na chakula serikali itaweza? Wale watoto wanatafuta kuishi. Hawawezi kufia ndani ilhalu kuna kuchakuachakua mchanga ili wapate kula.