Kazi ya jeshi la polisi ni kulinda raia na mali zao na wala si jeshi la kupigana na raia. Polisi wanatakiwa watumie weredi tu. Maandamano na migomo ni haki ya kikatiba ya wananchi katika kuwasilisha sauti zao pale ambapo lugha za midomoni na kalamuni zimedunda. Polisi kuapigana na raia wema kwa maslahi yao binafisi ni kuvunja sheria. Wanatakiwa wawe walinzi wa amani ambao kazi yao ni kuhakikisha maandamano hayo yanafanyika kwa amani na usalama wa waandanaji na waandamaniwaji.
Nguvu ile ambayo wanapanga kuitumia kuua raia kwa sababu tu wanaandamana kwa amani, waitumie kuzuia uharifu wowote ambao intellingencia yao itawaambia. Hiyo ndiyo kazi yao. Vinginevyo, hawataweza kuuzima moto watakao uwasha kwa unyanyasaji na mwendelezo wa umwagaji damu za raia wema.
Wakumbuke kwamba wanaishi na kufanyia kazi kati kati ya raia. Wakumbuke kwamba wana ndugu zao wa damu ambao wanaishi uraiani na kwa vile ni maandamano ya nchi nzima, yamkini hao ndugu zao pia watakuwa miongoni mwa watakao uawa na polisi kwa vile hawatakuwa na nembo kama red cross kwamba hawa ni ndugu wa polisi.
Sioni askari yeyote atafurahia kulinda ccm huku akipoteza ndugu zake wote kwa mkono wa ccm hiyo hiyo. Sioni furaha yoyote wataipata Chagonja na mumiani wowote pale jeshi la polisi likiasi seriakali mikononi mwao. Wfahamu jeshi la leo siyo la zamani la utii kwanza akili baadaye.
Askari wa sasa wana reason na ni wasomi wanaoelewa. Na watakapochoka, ndipo uvamizi wa vituo na wizi wa sialaha magharani utashika kasi huku askari wengi waki resign ili kuepuka amri dharimu za kina chagonja ambazo zitawalazimisha kuua ndugu zao.
Chagonja, muda wa ubabe ukwisha. Tumia akili hata kama huna, azima kwa wasaidizi wako ambao wana akili na weledi kuliko wewe.