Usishangae ndugu polisi kutoa vitisho unavyoviona. Wengi wa polisi ni wala rushwa na wamepata maisha mazuri na vyeo vyao kwa kubebwa na wala wajibu wao hawaujui. Usishangae akina Chagonja nk ukimpa kitabu cha sheria za jeshi la polisi au hata katiba aishie kusoma page moja ama mbili. Yeye anachojua ni kuangalia kiongozi gani wa ccm anasema nini wanajua ndio sheria zinavyosema. Lakini hawajui maandamano ni haki ya kikatiba. Lakini kwa polisi ambao .wana mafanikio kwa rushwa na kutegemea vyeo vya mfumo huu mbovu sio rahisi wakubali maandamano maana ndio mwanzo wa utawala mbovu kutoka madarakani na wao waishie kuaibika.
Nasema hivyo kama ni kweli ni polisi wenye uwezo na weledi wa kazi yao, walipaswa kutoa mwongozo maandamano hayo kama ni ya amani yafinyike wapi na kuyaonyesha maeneo ya kupita ili iweze kuwa rahisi kwa polisi kuyadhibiti kama yana lengo baya. Ila polisi hawa wanapatikana kwa rushwa, kujipendekeza na mifumo mibovu ya uteuzi wanahakikisha raia hawana sauti ya kutoa hisia zao tofauti kwa njia ya amani tena ya kikatiba kwani wao ni sehemu ya mfumo huo mbovu, na wanajua mfumo mbovu ukibadilika ajira zao zitakuwa hatarini kwani wengi hawana uwezo wa kazi hiyo na wanamiliki mali nyingi zisizo za halali, wanaendesha biashara bila kulipa kodi nk. Ndio maana chunguza sana viongozi wakuu wa polisi ndio wanaunga mkono viongozi wengi wabadhirifu wa serekali kwani wote wanasaidiana kwenye kuibia wananchi. Na ukienda kwa undani sana wote wanamiliki biashara, majumba, magari nk kwa majina ya watu wengine.
Mimi ninawaomba viongozi wote wanaochagiza wananchi tuandamane, waende polisi na barua wawaeleze polisi njia watakazotumia kwa maandamano yao, na eneo watakaloishia na ujumbe utakaotolewa na barua hiyo isomwe kwenye vyombo vya habari kama ushahidi na iwapo polisi watagoma nguvu ya umma ifanyike. Na pia wakati wa tangazo hilo la vyama vinavyotaka maandamo lazima watoe angalizo kwa watu wote watakaondamana waje na majani ama vitambaa vyeupe na kila mtu awe mlinzi wa mwenziwe ili wenye lengo ovu wachuliwe hatua. Na ikiwezekana kuwe na madaftari ya wananchi watakaofika kwenye maandamano waandike majina yao na kusaini kutokukubaliana na wizi unaoendelea hapo Dodoma tena kwa njia ya amani tu. Hapo ndio mtajua tuna polisi wa aina gani, lakini ukiona polisi anayesimama na kusema hatutaki maandamano, sijui watu watapoteza maisha yao sio kweli, mbona ajali zinatokea za mabasi lakini hawasimamishi watu kusafiri bali wanawabana zaidi madereva na wamiliki kuwa makini ajali zisitokee. Maandamano ni lazima na ole wao polisi waue raia mwema ni lazima tuwafungulie mashitaka hawa wezi na watu wanaopata madaraka bila uwezo wa kazi stahiki ama rushwa na kujipendekeza.