BAVICHA watoa tamko kuhusu maandamano

BAVICHA watoa tamko kuhusu maandamano

Mwenyekiti wa baraza la vijana BAVICHA bw PATROBAS KATAMBI akizungumza na wanahabari muda huu hapa katika mkutano wa chadema unaoendelea
-Kufwatia jeshi la polisi Tanzania jana kupiga marufuku maandamano yaliyotangazwa kufanyika na chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA,umoja wa vijana wa chama hicho BAVICHA umeibuka na kusema kamwe hawatishiki na kauli ya jeshi hilo na wapo tayari kwa lolote.
---------
Akizungumza na wanahabari muda huu nje ya mkutano wa kamati kuu ya chama hicho mwenyekiti wa vijana taifa PATROBAS KATAMBI amesema kuwa kauli iliyotolewa na mwenyekiti wao sio kauli yake kwani ni kauli ya chama na wanachama wote hivyo polisi wasihangaike kumkamata mwenyekiti wao na badala yake wajiandae kulinda amani wakati wa maandamano- hayo.
---
“tumezoea kusikia kauli za vitisho vya jeshi la polisi wakati chadema inapotaka kufanya kitu cha kuwatetea wananchi wao,ila siku ccm ikitangaza kufanya maandamano ya amani huwezi kusikia kauli kama hizo,sasa tumechoka na mambo hayo na tupo tayari kwa lolote lile”amesema mwenyekiti wa BAVICHA TAIFA
------
Aidha amesema kuwa ofisi yake imeitisha kikao cha dharura kwa ajili ya kupanga mikakati imara ya kuanza maandamano hayo ambapo amesema kuwa yatafanyika nchi nzima bila kikomohuku akisema -yataanza muda wowote kuanzia sasa.
Nyie BAVICHA msiponze Watoto wa wenzenu. Tokeni nyie na Watoto, wake, wajomba, wakwe n.k. Mkaandamane mubondwe nyiye na si kuchochea Watoto wa Watu wengine nyie mnajificha. Watanzania hatudanganyiki. Tunaona mataifa mengine yaliyowafika. Siku hizi hata Sisi wa Vijijini tunayaona kwenye TV baada ya kuwezeshwa kupatikana Umeme hata Vijijini kulikowezeshwa na Serikali ya CCM.
 
Kama huna kitu unachokiamini kiasi cha kutoa maisha yako kukitetea huna sababu ya kuishi!!
 
Mwanzo nilifikiri ana utimamu kumbe sivyo! Yani anajidai nae mtoa matamko!
Chadema katika hili itawaponza vijana wengi sana!
 
Safi sana Kamanda tupo pamoja hakuna kulala mpaka kieleweke tukicheka na hawa interahamwe watoto wa watoto wetu wataishi maisha magumu zaidi yetu.
 
Kama huna kitu unachokiamini kiasi cha kutoa maisha yako kukitetea huna sababu ya kuishi!!
WE,yaani niache dunia ajili ya kutetea ukoo wa mbowe au slaa wakaishi magogoni,aah wapi?,maisha matamu bana na ukishakwenda umekwenda hakuna kwamba utarudi mbowe akupe hata umesenja wa ikulu.
 
Nyie BAVICHA msiponze Watoto wa wenzenu. Tokeni nyie na Watoto, wake, wajomba, wakwe n.k. Mkaandamane mubondwe nyiye na si kuchochea Watoto wa Watu wengine nyie mnajificha. Watanzania hatudanganyiki. Tunaona mataifa mengine yaliyowafika. Siku hizi hata Sisi wa Vijijini tunayaona kwenye TV baada ya kuwezeshwa kupatikana Umeme hata Vijijini kulikowezeshwa na Serikali ya CCM.

acha kupinga mayowe.kuandama tunaandama sisi.
 
Maandamano ndo hayo maradhi menyewe.syria walianza maandamano tukasema chondechonde syria msijaribu mtakuja kulia,leo wanalia.

libya vilevile,ncha ya upanga haijasaidia kitu.sasa unadhani wanazuia maandamano kwasababu gani.maandamano yasiyo kikomo tena nchi nzima lengo lake ni kuiangusha serikali,nani atakubali hiyo?

Hufahamu yaliyoko nyuma ya Pazia.Je Libya walioifikisha pale ni Walibya wenyewe? Fuatilia siasa za Syria utajua kinachoendelea.anayeonewa akichoka kuonewa akifanya maamuzi huwa harudi nyuma.Tafuta upeo wa mbali na si kutazama karibu.kama wanajali wananchi nipe sababu kwa nini wamesigina kpengele cha maadili ya viongozi,ukomo wa madaraka kwa wabunge na suala la elimu,kwa haraka utaniambia Katiba inatoa Uhuru,swali Je walioko kule mjengoni wote hawajui haki za wananchi.NIMESHANGAZWA NA HAO MP WANAODAI WALIOKO NJE HAWAWATISHI LAKINI LIKIONGELEWA NJE WALIOKO NDANI WANAJIBU.NINI MAANA YAKE?
 
Cku zote yanapofanyika maandamano ya amani polisi ndio wanaoanzisha fujo. Ole wenu polisi mnaopinga chadema wakati wanatetea katiba itakayo wahusu.

Narudia tena plz polisi msiingie haya maandamano sababu tutawaboko haramu.

Huku arusha tupo tayari kwa mchaka mchaka tunasubiri raisi wetu lema apulize kipenga.
 
Mwanzo mzuri Patrobas!
Yaani unasifia ujinga! Maandamano ya nini kama BMK liko kisheria na mwisho wake ni october 4, 2014; kura ya maoni juu ya katiba mpya 2016; maandamano ya nini? wacha wale hizo hela halafu watakutana na wananchi baadaye na watawaadhibu sana hawa maccm.
 
WE,yaani niache dunia ajili ya kutetea ukoo wa mbowe au slaa wakaishi magogoni,aah wapi?,maisha matamu bana na ukishakwenda umekwenda hakuna kwamba utarudi mbowe akupe hata umesenja wa ikulu.

huo ndio uwezo wako wa kufikiri?
 
Hufahamu yaliyoko nyuma ya Pazia.Je Libya walioifikisha pale ni Walibya wenyewe? Fuatilia siasa za Syria utajua kinachoendelea.anayeonewa akichoka kuonewa akifanya maamuzi huwa harudi nyuma.Tafuta upeo wa mbali na si kutazama karibu.kama wanajali wananchi nipe sababu kwa nini wamesigina kpengele cha maadili ya viongozi,ukomo wa madaraka kwa wabunge na suala la elimu,kwa haraka utaniambia Katiba inatoa Uhuru,swali Je walioko kule mjengoni wote hawajui haki za wananchi.NIMESHANGAZWA NA HAO MP WANAODAI WALIOKO NJE HAWAWATISHI LAKINI LIKIONGELEWA NJE WALIOKO NDANI WANAJIBU.NINI MAANA YAKE?
Mh..wewe ndo wakuniambia mambo ya syria na libya kweli?..

yaliyoko nyuma ya pazia ni watu kuhongwa na wamagharibi na kuanzisha maandamano eti papatikane demokrasia,na demokrasia ndo hiyo wanaipata sasa.
tatizo la cdm ni kutaka kuiga mambo ya kwenye luninga badala ya kufanya siasa za kistaarabu.
 
Chadema wanaume ,Pamoja sana ikibidi mpaka ikulu.

Mkuu ratiba ya chakula itakuwaje ? au tunaandamana tu kula kwetu?
chama inabidi kifikirie na chakula muda wa maandamano hatuwez kuandamana huku tuna njaa!
nawakilisha tu.
 
Kwa mwenye akili timamu sidhani kama atashabikia maandamano, ukivunjwa mguu au kiuno wenzako wanaendelea kula bata na hakua atakayekujali.:hail:
 
Wakuu egypt walikuwa wanahawa mikate na maji kwa waandamanaji vipi kwa upande wetu sie makamanda?
 
Back
Top Bottom