BAVICHA Watikisa Majiji Matatu Tanzania

BAVICHA Watikisa Majiji Matatu Tanzania

Chademakwanza

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2014
Posts
6,346
Reaction score
1,873
BAVICHA Watikisa Majiji Matatu.

Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA ) Wamezidi kudhihirisha umahiri wao katika,kuhakikisha wanaipoteza na kuifuta Ccm katika medani za siasa ya Tanzania.

BAVICHA wamefanya mashambulizi makali katika Jiji la Mbeya,Mwanza na Musoma.Kama ambavyo,lengo kuu la BAVICHA nikuona CHADEMA kwa kushirikiana na UKAWA wanakwenda Ikulu mwaka huu, wa uchaguzi 2015 wameamua kutumia fursa hii kuendelea kuisambaratisha Ccm kila kona ya nchi hii.

Mashambulizi haya yameendelea kuongozwa na Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa PATROBAS KATAMBI,ambae yeye alikuwa Mwanza kwaajili ya kuhakikisha matawi ya CHASO yanafunguliwa katika CHUO CHA MIPANGO Mwanza,jambo ambalo limefanikiwa na kuzaa matunda makubwa kwani alifanikiwa kuvuna wanachama wapya miatatu kutoka CCM.

Huku katika Mji wa Musoma...,Katibu Mkuu wa BAVICHA Julius MWITA aliwashamoto,na kuwahutubia maelfu ya wananchi waliokusanyika kumsikiliza na kumshangilia kwa kila hoja aliyokuwa akiizungumzia kwakuwa alisema kweli tupu.

Katibu Mkuu huyo hakusita kugusia swala la ukosefu wa ajira kwa vijana na jinsi Serikali ya CCM ilivyoshindwa kuzalisha ajira kwa vijana,badala yake wasomi wanaomaliza vyuo vikuu wapo mtaani hawana kazi za kufanya.

Julius Mwita...,alihoji juu ya Upungufu mkubwa wa Askari katika vituo vya Polisi jambo ambalo,haliingii akilini wakati vijana wapo mitaani wamemaliza Sekondari na Vyuo hawana ajira.

Huko nako katika Jiji la Mbeya...,M/kiti wa Mkoa wa BAVICHA George Tito amezidi kutishia uhai wa Ccm katika Jiji hilo,baada ya kufanya ziara vijijini ilikuimarisha Chama upande huo.Akiwa katika Kata ya Ushirika alipokelewa kwa Maandamano makubwa na vijana waliokuwa wakimsubiri kwa hamu tokea saa1 Asubuhi.

Akizungumza katika mkutano huo George Tito,aliweka wazi jinsi Serikali ya Ccm imewasahau wananchi wanaoishi vijijini,nakuwaona hawanathamani mara baada ya kuiweka madarakani.

"Serikali ya Ccm imeshindwa kuona thamani yenu,wana wa Ushirika imewasahu na kuona hamna maana tena.Sasa uchaguzi umefika watarudi tena kwenu kuomba kura kama walivyokuja mwaka 2010, mka wapa kura zenu sasa wanakuja kwa style ilele ya Vilemba,Kapelo,Kanga na Tirshet kuwahonga tafadhali msikubali hata kidogo.
 
Attachments

  • IMG-20150417-WA0015.jpg
    IMG-20150417-WA0015.jpg
    131.4 KB · Views: 2,610
  • IMG-20150417-WA0014.jpg
    IMG-20150417-WA0014.jpg
    187.9 KB · Views: 2,601
  • IMG-20150417-WA0012.jpg
    IMG-20150417-WA0012.jpg
    194 KB · Views: 2,413
  • IMG-20150417-WA0011.jpg
    IMG-20150417-WA0011.jpg
    88.6 KB · Views: 2,261
Mwaka huu magamba yanahemea kwa machine na bado twenden kaz makamanda hakuna kulala oct tunaingia Ikulu, tunahakikisha tunawakaba kila kona hakuna kulala hadi kieleweke.
 
CHADEMA kimekuwa kama teja. kikiona kina arosto kinaenda kwenye strongholds zake kinalalamika na kukashifu na kuridhika kuwa kinajenga chama. nendeni mkajenge chama huko ambako hamna wafuasi.
 
CHADEMA kimekuwa kama teja. kikiona kina arosto kinaenda kwenye strongholds zake kinalalamika na kukashifu na kuridhika kuwa kinajenga chama. nendeni mkajenge chama huko ambako hamna wafuasi.

Hatutaacha hata masalia hizi ni rasharasha mvua inakuja
 
Hatutaacha hata masalia hizi ni rasharasha mvua inakuja
kwanini nguvu kubwa ya ujenzi wa chama mnaelekeza kwenye ngome zenu tu? mtu aliyeokoka haitaji kuhubiriwa sana. kwanini hampeleki nguvu kubwa pwani, lindi, mtwara, zanzibar,katavi etc. au hamna cha kuwaambia?
 
CHADEMA kimekuwa kama teja. kikiona kina arosto kinaenda kwenye strongholds zake kinalalamika na kukashifu na kuridhika kuwa kinajenga chama. nendeni mkajenge chama huko ambako hamna wafuasi.

Wewe mbona umekuwa gasho kwa tamaa za bu7 acha mawazo finyu ya kigamba
 
kwannini nguvu kubwa ya ujenzi wa chama mnaelekeza kwenye ngome zenu tu? mtu aliyeokoka haitaji kuhubiriwa sana. kwanini hampeleki nguvu kubwa pwani, lindi, mtwara, zanzibar,katavi etc. au hamna cha kuwaambia?
Naomba nikuhabarishe Chadema ipo Tanzania nzima na kama unafwatilia habari za chama pamoja na Bavicha tunaenda maeneo yote mfano mdogo tu juzi Myika alikua wapi?
 
kwanini nguvu kubwa ya ujenzi wa chama mnaelekeza kwenye ngome zenu tu? mtu aliyeokoka haitaji kuhubiriwa sana. kwanini hampeleki nguvu kubwa pwani, lindi, mtwara, zanzibar,katavi etc. au hamna cha kuwaambia?

Acha wivu wakike juzi Mh Mnyika alikuwa wap? Sio mtwara kama ujui hata macho huna kweli ugamba kaz mwaka huu mpaka mnene kwa lukha
 
Acha wivu wakike juzi Mh Mnyika alikuwa wap? Sio mtwara kama ujui hata macho huna kweli ugamba kaz mwaka huu mpaka mnene kwa lukha
nguvu wanazotumia huko hazilingani na mwanza, Arusha, klm au Mbeya.
 
CHADEMA kimekuwa kama teja. kikiona kina arosto kinaenda kwenye strongholds zake kinalalamika na kukashifu na kuridhika kuwa kinajenga chama. nendeni mkajenge chama huko ambako hamna wafuasi.
unagegedwa
 
Naomba nikuhabarishe Chadema ipo Tanzania nzima na kama unafwatilia habari za chama pamoja na Bavicha tunaenda maeneo yote mfano mdogo tu juzi Myika alikua wapi?
ssasa ilitakiwa isiwe juzi tu. ilitakiwa mikutano huko iwe mingi kuliko arusha na mwanza. hivi zanzibar na mafia mnaendaga?
 
Big up saaaana Bavicha, huu ni mwaka wa ukombozi na Bavicha lazima iwe game changer
 
Vijana ndio kundi linaloweza kufanya mabadiliko ya kweli ya kutosha kuiondoa ccm... Endeleeni kupambana tu...
 
kazi kwenda mbele mpaka kieleweke ,bavicha nganganga tupo pamoja wapambanaji.
 
BAVICHA safi sana...fanyeni kazi...kazi kama hizi inatakiwa nchi nzima inakuwa active kila weekend...si mpo nchi nzima bana

Point ya muhimu fanyeni kampeni ya mtu kwa mtu.....tuna viongozi wa msingi watumieni hao
 
Sasa hao si wavuta bangi kabisa hao katika picha hizo nani anafanana na uongozi? Tusifanyane watoto wadogo.
 
Back
Top Bottom