Habari zilizoanza kusambaa duniani jan usiku zinaonyesha kuwa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) watakuwa wenyeji wa mkutano wa bodi ya umoja wa vijana wa vyama vya kidemokrasia Duniani (Internationa Young Democrat Union, IYDU) mwezi July.
Taarifa hizo zinaeleza kuwa hii itakuwa mara ya kwanza kwa umoja huo unaoshirikisha nchi zaidi ya 120 ikiwemo BAVICHA kufanya mkutano wake Kusini mwa Jangwa la Sahara na Tanzania chini ya BAVICHA kuwa kichocheo cha kuleta mkutano huo nchini.
IYDU inahusiasha vijana wa vyama vikubwa duniani kama Republican ya Marekani, Consevrative ya Uingereza, CDU ya Ujerumani, kile Chama cha Sarkozi cha Ufaransa. Nchi nyingine zinazoonekana kwenye umoja huo ni Hispania, Denmark, Uswis, Italy, Austarlia Argentina, Ucraine, Ugiriki n.k na kwa africa zinaonekana Ghana, Kenya, Uganda, Namibia, Msumbiji, Tanzania n.k
Kwa hakika hii ni kazi nzuri ya John Heche kama Mwenyekiti wa BAVICHA na Deogratias Munishi kama Katibu Mkuu wa BAVICHA ambao wamejenga hoja na mazingira ya vijana hawa kuwa hapa Tanzania. Huu ni ufanisi wa hali ya juu kwa siasa za kimataifa zinazofanywa na BAVICHA ukiacha zile za ndani ambapo kwa kwa kiasi kikubwa wamevunja unazi wa vijana wa chama cha kijamaa kutawala ulimwengu wa siasa za Vijana Tanzania.
Welldone BAVICHA, Bravoo CHADEMA kwa kuwa na Vijana Mahiri kama Heche na Munishi.
MA CCM WANAONA GELE