ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,279
- 7,681
Haki, usawa na utawala bora haviwezi kuwepo midomoni tu. Ni lazima vionekane kwa vitendo.
Bavicha iko wapi?
Hivi karibuni kuna vijana walifukuzwa uanachama Bavicha na Kamati Tendaji kwa kosa la kuwachafua viongozi wa chama kwenye mitandao ya kijamii.
Hata hivyo, kijana Ben Saanane aliyehusika na kuwachafua viongozi kwenye mitandao ya jamii alisamehewa. Walioadhibiwa ni wale waliomchafua Dr. Slaa. Huyu Ben Saanane alimchafua Zitto Kabwe.
Msamaha huo wa Bavicha ulitolewa sababu mbalimbali, lakini wapo walioamini kuwa ni msamaha wa upendeleo unaokiuka misingi ya haki, usawa na utawala bora.
Cha kushangaza ni kwamba kupitia mitandao ya facebook na JamiiForums kijana Ben Saanane anaendelea kumchafua Zitto Kabwe, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, kwa kumhusisha na kesi za ugaidi!
Viongozi wa Bavicha wako kimya wakitabasamu kuona Zitto anachafuliwa.
Bavicha iko wapi?
Je, kuchafua viongozi kwenye mitandao ya jamii sio kosa tena?
Je, kiongozi asiyepaswa kuchafuliwa ni Dr. Slaa peke yake?
Je, ni lini Bavicha itaanza kumtendea haki Zitto Kabwe, kiongozi aliyejitolea kuiimarisha Bavicha kwa nguvu zake zote?