Ni vita down town Baton Rouge.
Update: Watu wawili wenye silaha ndio waliohusika kuwafyatulia risasi askari polisi na inasemwa mmoja wao ni mwenye matatizo ya akili. Bado kujulikana kama ni kitendo cha kigaidi au namna ya kuwasilisha ujumbe fulani.
Update: Baton Rouge ndipo alipouwawa mmarekani mweusi Alton Sterling.
Update: Msemaji wa polisi Casey Rayborn Hicks kutoka kituo cha polisi cha East Baton Rouge Sheriff’s Office anasema eneo la Airline Highway limefungwa na watu watafute utaratibu mwingine wa usafiri.
Update: Polisi wametanda eneo kubwa la Baton Rouge ambapo watu wenye silaha wanadaikiwa kuwa wamejificha.
Update: Idadi ya askari waliokufa sasa ni watatu, na waliopigwa risasi ni saba.
Askari polisi wawili wameuwawa baada ya kubadilishana risasi na kikundi cha watu katika mji wa baron Rouge.
Habari zaidi kuendelea kuja, lakini polisi wengine watatu wamejeruhiwa vibaya na hali zao si nzuri.