Basi la sabina lapata Ajali tabora

Keagan

Member
Aug 6, 2012
40
11
Wakuu,
Kwa masikitiko makubwa nawataarifu ajali ya basi la sabina, ilotokea tabora kwenda mbeya baada ya basi kupinduka.Tbc wameizungumzia pia kwny jambo alfajiri hii.

Tatizo wameeleza kifupi sana. Sie tuna kaka yetu alikuwepo kwnyw hilo basi Hadi sasa hatuelewi fate take hasa ukizingatia imeua watu kadhaa,maana hapatikani kwny simu hadi sasa.

Tunaendelea kusubiri updates.
 
Poleni wahanga wote wa ajali hiyo. Mtoa taarifa barabara hiyo ya TBR to MBY kuna sehemu hazina mawasiliano kabisa. Halafu jina la basi nadhani ni SABENA si SABINA.
 
Sheria za usafiri zisiporekebishwa kuendana na zile za kimataifa Tanzania itaendelea kuwa kaburi na machinjio ya watu wasio na hatia. Hili laweza kulaumiwa kwa uwekezaji wa kipumbavu ambapo wenye magari wameruhusiwa kudai kiwango cha pesa watakacho kiasi cha kuhatarisha maisha ya abiria. Magari mengi yamo barabarani lakini ni mikangafu ambayo hafanyiwi services kama sheria itakavyo. Rushwa kwa matrafiki ndiyo usiseme. Ingawa ni mapema kusema chanzo cha ajali ni nini, kuna uwezekano moja ya niliyotaja hapo juu kuwa sababu.
 
Wanauwa reli ili mabasi yaendelee kumaliza watu!! Reli ndiyo usafiri uliomzuri zaidi kutokana na ukweli kuwa nchi nyingi duniani mabasi huwa ni kama back-ups!! Lakini serikali haiko madarakani kwa ajili ya wananchi, ipo kwa ajili ya genge fulani lenye nia ya kujitajirisha mpaka tulitoe ndiyo tutaanza kuona matunda ya kuwa na viongozi wa watu!
 
Mkuu
Poleni kwa taarifa hii nzito yenye utata mwingu kwenu.
Fanyeni kila liwezekanalo kujua hatima yake na km ameumia afanyiwe mipango mizuri ya tiba.
Tuko pamoja mdogo wangu, na Mungu anaendelea na kazi yake.
 
Daaah taarifa zilizopatikana sasa ni kwamba bro nae ni kati ya 16 walofariki kwenye ajali,so hatunaye tena!
 
Wanauwa reli ili mabasi yaendelee kumaliza watu!! Reli ndiyo usafiri uliomzuri zaidi kutokana na ukweli kuwa nchi nyingi duniani mabasi huwa ni kama back-ups!! Lakini serikali haiko madarakani kwa ajili ya wananchi, ipo kwa ajili ya genge fulani lenye nia ya kujitajirisha mpaka tulitoe ndiyo tutaanza kuona matunda ya kuwa na viongozi wa watu!

Kwa speed ambayo ma bus yao yanatuchinja nadhani siyo muda mrefu watakosa abiria wa kusadfirisha!!!! SOTE TUTAKWISHA AU TUTAKUWA WALEMAVU TISOWEZA KUSAFIRI TENA!!
 
Back
Top Bottom