Basi la Abood lapata ajali asubuhi hii Aprili 23, 2023, Dereva akimbia

Boran Jakutay

Senior Member
Apr 8, 2023
110
255
IMG_20230423_093135.jpg
IMG_20230423_093310.jpg

Taarifa za hivi punde zinasema kwamba Basi la Kampuni ya Abood lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es Salaam limepata ajali maeneo ya Mswiswi.

Mtoa taarifa amesema: "Abood kutoka Mbeya kwenda Dar asubuhi ya Leo maeneo ya Mswiswi.

"Poleni sana aisee, taarifa kamili itakuja baadae na itatolewa na mamlaka husika."

Mungu awanusuru wote.

----------- ----------------
Updates...

POLISI WAFIKA SEHEMU YA TUKIO
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema “Ni kweli ajali imetokea na basi limelalia ubavu mmoja, kuna majeruhi kadhaa ambao wamepelekwa hospitali.”

“Inavyoonekana chanzo cha ajali ni dereva kukosa umakini wakati akiwa katika mwendo kasi, bahati mbaya dereva amekimbia na hatujui alipo, abiria wengine wameondoka kwa usafiri mwingine.

“Tunaendelea kulifanyia uchunguzi basi kisha tutatoa taarifa kamili baadaye.”
 
View attachment 2596889View attachment 2596891

Taarifa za hivi punde zinasema kwamba Basi la Kampuni ya Abood lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es Salaam limepata ajali maeneo ya Mswiswi.

Mtoa taarifa amesema: "Abood kutoka Mbeya kwenda Dar asubuhi ya Leo maeneo ya Mswiswi.

"Poleni sana aisee, taarifa kamili itakuja baadae na itatolewa na mamlaka husika."

Mungu awanusuru wote.

Tumeamua kuukimbia ukweli na hadi akili zitakapokuja kutukaa sawa, bado tupo tupo sana:

Ajali: Tuambiane ukweli dhahama hili lituepuke
 
Mungu awaponye haraka majeruhi, Police wawe wawazi kwenye hili maana abood wanafigusu kwenye taarifa za ajali
 
Back
Top Bottom