Tabora: Basi la Kampuni ya Coast Line lapata ajali ya kupinduka, abiria kadhaa wajeruhiwa

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Basi linalomilikiwa na Kampuni ya Coast Line lililokuwa likitoka mkoani Katavi kuelekea jijini Arusha lilipata ajali ya kupinduka Jana maeneo ya wilaya ya Sikonge mkoani Tabora

Taarifa zinasema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni utelezi wa barabara uliotokana na mvua zinazoendelea kunyesha baadhi ya sehemu nchini Tanzania.

Kuhusu hali ya abiria, taarifa zinadai kwamba hakuna vifo, isipokuwa kuna abiria kadhaa walijeruhiwa na walikimbizwa kwenye hospitali ya wilaya ya Sikonge kwa matibabu.
IMG_20190222_083211_590.jpeg
IMG_20190222_083227_253.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi inakuawaje miaka yote hiyo baada ya uhuru inakuwaje bado tunasikia habari za barabara za vumbi? Halafu hilo jina la kampuni mbona haliendani na route yake- coast wakati route yake ipo inland.
 
Back
Top Bottom