Basi la Mtei lachomwa moto

Basi la Mtei lachomwa moto

Wadau nimepita hapa Singida nikitokea Arusha nimekutana na basi la Abiria mali ya kampuni ya Mtei. Chanzo ni kwamba gari hilo limemgonga bodaboda aliyekuwa amebeba watoto wawili waliofikwa na mauti.Hakika inasikitisha sana kwa upande wa wafiwa na kwa kuchomwa basi hili kwani mabegi na mali za abiria zilizokuwamo ndani ya gari vyote vimeteketezwa.

Abiria hawajajeruhiwa?
 
Acha kujifanya unajua wewe sio kila kitu lazima ujifanye na wewe upo mtei ni ukoo mkubwa sana na umegawanyika edwin mtei wa cdm hahusiki na hii kampuni wala hana shea.

Ndo huyo bwana unatoka povu la nini! Ndo huyo alokuwa gavana wa bank kuu wa kwanza tz/ cjui waziri wa mshiko tz
 
Mwenye mabasi keshatangulia mbele ya haki yanasimamiwa na vijana wake na mja alifariki mwaka jana.

Mungu akusamehe maana mwenye mabasi yuko hai; anashirikiana na watoto wake anaishi kijiji cha Kiranyi, barabara ya silent inn, juu kidogo ya tank la maji.
 
Polen wafiwa,polen abilia mlioalibikiwa na mali zenu!!nafikil ingekuwa busara zaidi kama wangemwazibu dereva.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

duu hii kali sasa gari linachomwa dreva anaachwa duu..

...ndio ubaya wa mob justice.....juzi juzi dar kauliwa mtu......haijulikani kama ni kichaa au mchawi....the question is ....kwanini mtu asiye na kosa auliwe au aharibiwe mali yake kwa sababu ya watu wengine kujichukulia sheria mkononi?.........na hata kama ana kosa basi achukuliwe hatua za kisheria.....kwani tumejiwekea sisi wenyewe sheria hizo ili zitulinde na tuwe wastaarabu kuzifuata.......

Poleni wafiwa na poleni abiria mliopoteza mali zenu.........

Ikumbukwe pia kuwa sheria barabarani zina-apply kwa wote......waenda kwa miguu, waendesha pikipiki na magari.......tujifunze sheria za barabarani tunamopita kila siku ili tuzitumie barabara zetu salama.......kitendo kilichotokea kule singida kinaondoa dhamira ya werevu wa kujua/kufuata sheria....ili iwe fundisho kwetu sote....na ili jambo lile lisitokee tena..........
 
Back
Top Bottom