Basi la Hekima Laanguka na kuua Tanangozi

Habari nilizozipata muda huu kutoka kwa abiria aliyemo katika basi la Superfeo ni kwamba basi la kampuni ya Hekima limeanguka katika kitongoji cha Tanangozi Iringa na kuua abiria wengi idadi ambayo bado kujulikana, kwa vile kuna wengine bado wamelaliwa na bodi la basi hilo.

Kuna majeruhi wengi sana na tayari akina mama wawili wameonekana wamekatika mikono yao vibaya, hali za majeruhi ni mbaya sana.

Jamani mwe!
 
binafsi ajali ya basi hilo niliitegemea siku nyingi saana, naamini ilikawia maana Mungu alitaka wenye mamlaka watimize wajibu wao.
ajali ya basi la Airforce liendalo Mbeya , Kyela na Tunduma nayo naisubiria kwa hamu kama wenye mamlaka wataendelea kula kuku bila kuchukua hatua.
Nasema hayo kwa sababu moja kuu.......hayo mabasi ambayo nimeyataja hapo juu ni sawa na madaladala hapa mjini kwa namna yanavyoendeshwa na madereva wahovyo mno.
kwamfano ukiwa unaenda Mbeya, ukivuka Makambako tu, hicho kisehemu kilichobaki hakinaga Trafiki, hivyo madereva wa mabasi hayo huamua kufidia muda ambao husimamishwa na matrafiki njiani.
kwakweli nawapa pole majerui woote, ila ajali ya airforce Bus naitegemea muda ama siku yoyote.....kama hatua hazitachukuliwa.
 
niliwahi panda hili basi toka mbeya mpaka dar,kwakweli ilikua ni hatari sishangai likipinduka na kuua wengi,spidi jamaa alikua anaenda nayo ni hatari,nasikia alitoka lusaka zambia saa 12 asubuhi,tumefika dar saa tisa na nusu likiwa ni basi la kwanza kuingia,nilishikilia roho toka mbeya hadi dar,maana hiyo spidi mmh,poleni majeruhi na marehemu.

Wandugu this is too much for one to bear.
We should distinguish hearsay from fact,Lusaka -Mbeya is separated by 1200km, Mbeya Dar is about 880km.
2000km by bus in 9 and a half hours?
Thats too much for me to bear
 
Lole INAWEZEKANA KWENDA KWA MWENDO HUO, kama Kiswele alikua anatoka Songea Mjini saa 12 asubuhi anatua Dar saa kumi jioni umbali wa KM 1100 HIVI, hiyo ni mid 1990s Sembuse kizazi hiki cha mabaasi.
Gwakisa unapaswa utambue hilo ni Hekima bado yupo pacha wake mwingine anaitwa Airforce one ana route ya DAR-KYELA, DAR-TUNDUMA na DAR-MBEYA CITY.
huyu hana muda mrefu kama hatadhibitiwa ataua tena kwa kishindo kikuu. huu si utabiri ila ni matokeo ya kufuatilia mbio zao.
sasa Hekima atajifunza huenda.
hawana chakuogapa maana waziri mwenye dhamana mwenyewe ameenda likizo ya kampeni tangu mwezi wa sita mwaka jana.
 
niliwahi panda hili basi toka mbeya mpaka dar,kwakweli ilikua ni hatari sishangai likipinduka na kuua wengi,spidi jamaa alikua anaenda nayo ni hatari,nasikia alitoka lusaka zambia saa 12 asubuhi,tumefika dar saa tisa na nusu likiwa ni basi la kwanza kuingia,nilishikilia roho toka mbeya hadi dar,maana hiyo spidi mmh,poleni majeruhi na marehemu.

, acha uongo
 
binafsi ajali ya basi hilo niliitegemea siku nyingi saana, naamini ilikawia maana Mungu alitaka wenye mamlaka watimize wajibu wao.
ajali ya basi la Airforce liendalo Mbeya , Kyela na Tunduma nayo naisubiria kwa hamu kama wenye mamlaka wataendelea kula kuku bila kuchukua hatua.
Nasema hayo kwa sababu moja kuu.......hayo mabasi ambayo nimeyataja hapo juu ni sawa na madaladala hapa mjini kwa namna yanavyoendeshwa na madereva wahovyo mno.
kwamfano ukiwa unaenda Mbeya, ukivuka Makambako tu, hicho kisehemu kilichobaki hakinaga Trafiki, hivyo madereva wa mabasi hayo huamua kufidia muda ambao husimamishwa na matrafiki njiani.
kwakweli nawapa pole majerui woote, ila ajali ya airforce Bus naitegemea muda ama siku yoyote.....kama hatua hazitachukuliwa.

Chukueni hatua haraka nyie wenye mamlaka, mmekaa kupokea rushwa tu ala!!!! Mnapewa taarifa mnataka ushahidi, sasa tukiwaletea ninyi mtafanya kazi gani? Fuatilieni hii taarifa.
 
Si juzi juzi tuu apa wamesema basi zote speed 80 na wakaguzi watakwea kuhakikisha ilo.
I reserve my comment mpaka nipate sababu za ajari kutokea
 
Wakati mwingine abiria ndio wanachochea madereva waende kasi kubwa

Achana na simple conclusion, go to the real causes. Hivi akija mtu akuchochee kubaka utabaka? Dereva ukiambiwa uende kasi na abiria kwani anaushikilia mguu wako kwenye accelerator.

Acheneni na propaganda za watu walioshindwa kutimiza wajibu wao (Serikali na POLICE)
 
Eeh mungu wangu, ajali tena! inasikitisha. poleni sana wafiwa na mliopata majeraha tunawatakia uponaji wa haraka. mimi nadhani serikali yetu haijawa serious katika kuchukua hatua mathubuti. imefika wakati sasa watanzania tuseme 'sasa basi'. taifa linaangamia kwa ajali. walemavu wanaongezeka. jamani mpaka lini? hao trafiki wa barabarani kwa mtizamo wangu hawafai na waondolewe! wanachojali ni manufaa yao. ni mara ngapi tunaona magari mabovu yako b-barani lakini hayachukuliwi hatua yoyote? ni mara ngapi magari ya mkaa yamesababisha ajali kwa kutokuwa na reflectors na kupaki kando ya b-bara? hata reflectors nazo ghali kununua?

pendekezo langu- bus lolote litakalohusika na ajali mmiliki alazimishwe kulipa fidia kwa ndugu wa marehemu na kuwalipa majeruhi kwa kiwango cha majeraha na dereva pia kufungwa jela. mtaniambia, kwani hakuna mmiliki atakayekubali kupata hasara kwenye biashara yake. akishindwa kulipa then bus au mabasi yake yapigwe mnada kulipa fidia.
 
Wandugu this is too much for one to bear.
We should distinguish hearsay from fact,Lusaka -Mbeya is separated by 1200km, Mbeya Dar is about 880km.
2000km by bus in 9 and a half hours?
Thats too much for me to bear
mkuu nilipandia mwanjelwa basi lilitoka zambia abiria ndani ndio walinisimulia walikotoka,na nasikia hilo basi wao wafanyabiashara zambia wengi ndio abiria kwani wanawahi dar na kupiga shoping wakifika asubuhi wanaondoka nalo tena.
 
, acha uongo
Joji, Hekima kwenda mwendo wa kasi kweli ndio sifa yao, siku ambazo hakuna Trafiki wengi njiani linauwezo wakufika Tukuyu saa kumi na nusu, kweli linauwezo wakumia hata masaa 9 likiamua.
mbona ukitumia usafiri binafsi unauwezo wa kutumia masaa nane na nusu kutoka Mbeya mjini, kumbuka hizi basi zina engine kubwa sana, na zina madereva wasio waoga, kuna mtu ananitonya ni gari zenye bodi za kichina.....pamoja na ndugu yake airforce
 
Terrible. Lakini why Tz things like these are daily on the increase?

ni wakati sasa wa kufufua mabasi ya kamata na railway, hakukuwa na hizi ajali kwa kampuni hizi, wenye mabasi wamejaa tamaa ya pesa bila kujali wateja wao
 
Joji, Hekima kwenda mwendo wa kasi kweli ndio sifa yao, siku ambazo hakuna Trafiki wengi njiani linauwezo wakufika Tukuyu saa kumi na nusu, kweli linauwezo wakumia hata masaa 9 likiamua.
mbona ukitumia usafiri binafsi unauwezo wa kutumia masaa nane na nusu kutoka Mbeya mjini, kumbuka hizi basi zina engine kubwa sana, na zina madereva wasio waoga, kuna mtu ananitonya ni gari zenye bodi za kichina.....pamoja na ndugu yake airforce
mi nilipoingia ndani jamaa hiyo spidi yake aliyoanza chomoka nayo toka uyole,ndiyo ilifanya niulize maana nilishangaa na ndio abiria kuniambia nisishangae ni kawaida wao wametoka zambia saa 12 asubuhi,na nakwambia basi zote mpaka zilizoondoka mbeya na zingine tunduma saa 11 alfajiri tumezipita njiani kama zimesimama.
 
ni wakati sasa wa kufufua mabasi ya kamata na railway, hakukuwa na hizi ajali kwa kampuni hizi, wenye mabasi wamejaa tamaa ya pesa bila kujali wateja wao

Yaani kama ulijua ninachowaza.
Railways ifufuliwe by hooks or crooks but not by Indians
 
Wandugu this is too much for one to bear.
We should distinguish hearsay from fact,Lusaka -Mbeya is separated by 1200km, Mbeya Dar is about 880km.
2000km by bus in 9 and a half hours?
Thats too much for me to bear

that means 2000km/9.5hrs=210km/hr...kwa barabara gani?hio nyoka ya dar-mbeya,jamani tuongee vitu vya uhakika.mind you kuna sehemu atakuwa anapunguza mwendo kama kitonga hivyo hio 210km/hr ni average speed so kuna sehemu anakanya over 210km/hr
Hakuna basi linaweza kwenda mwendo huu,tushasafiri na hayo mabasi sana, wanaenda speed but not 200km/hr.
 
hao wajinga wa mabasi ni kwamba wanaendesha rough,kama speed wengi tunakwenda speed ila unakuwa sensible,hao wajinga wanaenda kama nyati,overtaking kwenye kona,hills na mashindano yasikuwa na msingi,ukijumlisha na hizo barabara kama nyoka hata 100km/hr inaoneka speed kali.
 
Back
Top Bottom