Basi gani luxury barabara ya Dar-Arusha?

Basi gani luxury barabara ya Dar-Arusha?

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2014
Posts
4,050
Reaction score
12,966
Wakuu habari.

Nina safari ya kwenda Arusha siku ya Jumatano ama Alhamisi. Sasa naomba kujua basi ambalo ni luxury au basi semi luxury zuri lenye uhakika. Ni muda sijasafiri hiyo barabara, hivyo naomba kujua ni basi gari zuri na lenye huduma nzuri na zenye uhakika.

Ahsante.
 
Ukipata Kilimanjaro sio mbaya na ni uhakika. Ukiulizia luxury watakuambia ni saa ngapi inaondoka dsm.
 
Eti milele. Hatuishi milele mkuu.
Hajui maisha ya binadamu yeyote yule muda wa kuishi duniani ni mfupi, hata uwe tajiri,masikini,mzuri,mbaya,mwema, maarufu n.k utayaacha yote watu wakitumbua na kugombania wakati unaumia kuyatafuta wao walikuona mpuuzi.

Hahahahahaa!!!

Tusipotoshane!!!
 
Dar Lux baba lao
Mabasi mbovu, huduma mbovu. Nina experience ya hayo mabasi njia ya Mwanza.

Wameandika huduma za uongo ambazo hazipo ila kwenye nauli zimewekwa kama wi-fi. Kila ukiuliza utaambiwa imeharibika.

Wana kuhoteli chao pale Dodoma kabla ya kufika Singida, chakula kina mwezi mzima au wiki kadhaa. Ukila wali pale au chakula chochote cha maji maji hufiki Singida unahisi uharo.

Hii route ya Arusha yamekua yakiharibika njiani mara kwa mara watu wanalalamika.

Darlux hata bure sipandi.
 
Back
Top Bottom