Basi gani la mkoani ulipanda ukajutia?

Hii ilikuwa ni safari ya Ifakara Dar bila shaka. Bora lami ikamilike sasa ili haya mambo yabakie tu kuwa ni historia. Hiyo barabara ilikuwa inachosha sana.
 
Siyo moja kweli? Mimi nilipanda hilo Happy Africa linatoka Ludewa linapita kijiji chetu kipo mbele ya Ludewa saa 11 alfajiri.

Kwa hesabu zangu za haraka nikajua Dar tutafika mchana. Gari likasimama Makambako kama masaa manne, likaanza safari hivyo hivyo Mikumi tukafika saa 4 usiku, tukakuta Twiga wapo barabarani ikabidi tusubiri watoke.

Dar tukafika saa 7 usiku.

Next time nikiwa narudi tena Dar walivyonitajia nikawaambia sipandi hilo gari wakajibu siku hizi kachukua Luwinzo.

Sasa hapo labda nilichanganya kusikia Africa
 
Kipindi hicho nilipanda MJ safari, gari watu wanakula muda wote, sio mayai ya kuchemsha wala mahindi ya kuchoma, hawachagui hawabagui. Mmoja tunafika Morogoro akajinyea kwenye bus, harufu yake mule ndani haifai. Nilikoma kabisa siku hio.
🀣🀣🀣acha tuongeze siku za kuishi watu mnavituko 🀣🀣🀣mtu kujinyea🀣🀣🀣
 
Zakaria Trans,Mwanza -Tarime.Bus lilikuwa poa tu ila ngumi sasa.1.Dereva v/s konda 2.Konda v/s abiria 3.Abiria v/s Dereva 4 .Konda na derevav/s abiria 5.Abiria v/s Abiria.Mwisho kabisa Sister wa Kikatoliki v/s Konda.
Ntiti kwa ntiti
 
Kipindi hicho nilipanda MJ safari, gari watu wanakula muda wote, sio mayai ya kuchemsha wala mahindi ya kuchoma, hawachagui hawabagui. Mmoja tunafika Morogoro akajinyea kwenye bus, harufu yake mule ndani haifai. Nilikoma kabisa siku hio.
ChaiπŸ˜‚πŸ˜‚
 
Nikipata pesa na mimi nitapanda basi ,mnapata raha kiasi hiki? Comedy za kutosha🀣
 
Happy Africa ni Luwinzo
Sio kweli
Luwinzo ni Sweet Afrika labda Kama umechanganya.
Happy Afrika ilikuwa ya bwana mmoja hivi wa Mafinga jina lake ljnafanana na jina la miongoni mwa wanafunzi wa Yesu.
Ilikuwa bluu hivi wakati Luwinzo hata kipindi ni Stamili sidhani Kama amewahi kuwa na rangi ya bluu
 
Route ndio alichukua Luwinzo
 
Mmasai kabeba ugoro kilo 2 , gari zima anatema mate yeye tu. Mwenyew anaita "Reja"
 
Machame coach,,,nilikata tiketi ya bus la saa moja na nusu coz lilikuepo na la saa moja kamili,,,bwana weeee kumbe bus la saa moja na nusu linapita saa mbili na la saa moja kamili linapita saa moja na nusu,,ile kuzama ndani sasa nashangaa mbona siti yangu sioni nkavunga,,safari ishapamba konda kukagua tiket sio ya gari yao ambalo ilibidi nipande lipo nyuma,,wakawasiliana wanavojua wao,, safari nikaendelea.

Arusha to Dodoma.
 
Bus ya kuitwa Shukurani Dar - Dom hata kama imebaki yenyewe sipandi.
Bus ya kuitwa Fikoshi sipandi bora niahirshe safari.
Niliwahi kupanda iringa - Mwanza gari ilkuwa fikoshi au premier(nimesahau).
Ila yote yalikuwa yanaongozana halafu yote miyeyusho.
Sitasahau, nilisimama kutokea iringa mpaka nimefika Singida ndio nikapata siti.
 
Hata huyo nae ilibidi ashukie njiani na sio sababu ya kula kula basi tu bahati mbaya ilimkuta ambae hata mimi na wewe inaweza kutukuta sema ni bonge ya aibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…