Bashungwa: Mitambo Yote na Wataalamu Wawe Site Ndani ya Mwezi Mmoja - Mlimba

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,899
944

BASHUNGWA: MITAMBO YOTE NA WATAALAM WAWE ‘SITE’ NDANI YA MWEZI MMOJA - MLIMBA

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ametoa mwezi mmoja kwa Mkandarasi wa Kampuni ya M/s Henan Highway Engineering Group Co. Ltd, inayojenga barabara ya Ifakara-Kihansi (km 124) Sehemu ya kwanza Ifakara-Mbingu (km 62.5) kwa kiwango cha lami kuhakikisha analeta mitambo yote na wataalam eneo la mradi.

Waziri Bashungwa ametoa agizo hilo wilayani Mlimba mkoani Morogoro mara baada ya kukagua kambi na mitambo na kutoridhishwa na idadi ya mitambo na wataalam waliopo eneo la Mradi.

“Mkandarasi huyu amekabidhiwa site tangu mwezi Novemba 2023 lakini bado mitambo na wataalam hawajafika site, nataka ndani ya mwezi mmoja TANROADS mniletee taarifa kuwa mitambo yote na wataalam wako hapa", amesisitiza Bashungwa.

Bashungwa ameitaka Wakala wa Barabara (TANROADS) kusimamia ipasavyo Wakandarasi wote wenye miradi mikubwa na midogo na kuhakikisha wanakuwa na Wataalam na Mitambo yote iloyobainishwa kwenye mikataba ili kuwezesha miradi hiyo kukamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa.

Aidha, Bashungwa amesema atakutana na uongozi wa juu wa Kampuni ya M/s Henan Highway Engineering Group Co. Ltd ili kujua namna gani watakavyojipanga kukamilisha miradi mitatu wanayoitekeleza nchini ndani ya muda wa mikataba.

Amesema atakutana na Balozi wa China nchini Tanzania ili kuzungumza naye juu ya Makampuni ambayo yamepewa zabuni ya kujenga miundombinu ya barabara na madaraja nchini lakini yamekuwa yakifanya kazi kwa kusua sua na kutokamilisha miradi hiyo kwa wakati

Kwa upande wake, Kaimu Msimamizi wa Miradi kutoka TANROADS, Mhandisi Malima Kasesa ameeleza kuwa kulingana na mkataba Mkandarasi alitakiwa kuwa na mitambo 137 katika eneo la mradi lakini hadi sasa ana mitambo 14.

Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Alinanuswe Kyamba amesema Mkandarasi alitakiwa kuwa ameleta wataalam tisa katika eneo la mradi lakini mpaka sasa wameshafika wataalam watatu na kati ya hao mmoja ndo ameidhinishwa kukidhi vigezo.

Naye, Mbunge wa Mlimba Godwin Kunambi amesema kilio kikubwa cha wananchi wa maeneo hayo ni kupata barabara ya lami na matumaini yao ni kuona mradi unakamilika kwa wakati na wameahidi kutoa ushirikiano mkubwa kwa Mkandarasi.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-02-24 at 13.19.29.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-24 at 13.19.29.jpeg
    622.6 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-02-24 at 13.19.30.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-24 at 13.19.30.jpeg
    639.2 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-02-24 at 13.19.30(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-24 at 13.19.30(1).jpeg
    381.5 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-02-24 at 13.19.31.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-24 at 13.19.31.jpeg
    550.3 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-02-24 at 13.19.31(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-24 at 13.19.31(1).jpeg
    645.7 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-02-24 at 13.19.32.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-24 at 13.19.32.jpeg
    666.5 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-02-24 at 13.19.32(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-24 at 13.19.32(1).jpeg
    821 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-02-24 at 13.19.33.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-24 at 13.19.33.jpeg
    909 KB · Views: 2
Henan kunani pale ? Shida mnawapa miradi mingi sana....pia hamuwapi pesa kuanzia....watumie zao
 
Diplomasia haijawahi kufanya kazi kwenye umasikini na unyonge!

Ingekuwa hivyo, njiwa wenu wasingekuwa wanadakwa hovyo uko duniani!
 
Back
Top Bottom