Bashungwa ambana mkandarasi AVIC, atoa wiki tatu mitambo na wataalamu kufika site

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,909
946

BASHUNGWA AMBANA MKANDARASI AVIC, ATOA WIKI TATU MITAMBO NA WATALAAM KUFIKA ‘SITE’

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ametoa wiki tatu kwa Mkandarasi wa kampuni ya China National Aero-Technology International Engineering Corporation (AVIC) anayetekeleza ujenzi wa barabara ya Isyonje - Kitondo - Makete sehemu ya Kitulo - Iniho (km36.3) kwa kiwango cha lami kufikisha vifaa, mitambo na wataalamu wote katika eneo la mradi ili kazi ifanyike kwa haraka.

Waziri Bashungwa ametoa agizo hilo leo Januari 22, 2024 wilayani Makete mkoani Njombe katika ziara ya kikazi na kukagua utekelezaji wa mradi huo ambao upo nyuma kwa mujibu wa mkataba.

“Natoa wiki tatu kuanzia sasa vifaa na mitambo yote inayohitajika pamoja na wataalaam wa usimamizi wa mradi wawe hapa, hawa wananchi hawawezi kusubiri wataalamu wapo likizo China wakati sisi shida yetu ni barabara”, amesema Bashungwa.

Aidha, Bashungwa ameahidi kuendelea kushughulika na Wakandarasi ambao wanasuasua katika utekelezaji wa miradi na wanaofanya kazi kinyume na mikataba

“Tunaposaini mikataba, nataka mikataba isimamiwe, namuagiza Mtendaji Mkuu wa TANROADS kusimamia kitengo kinachoshughulikia mikataba na kama wameshindwa kufanya kazi basi fukuzeni wote”, amesisitiza Bashungwa.

Kadhalika Bashungwa ameutaka Wakala wa Barabara (TANROADS) kumsimamia Mkandarasi huyo kwa karibu na kuhakikisha anafanya kazi usiku na mchana.

Ameeleza kuwa Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameleta Bilioni 82 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo kutokana na umuhimu wa wananchi wa Wilaya ya Makete na Mkoa wa Njombe katika kuleta maendeleo na kuinua uchumi wa wananchi.

Aidha, Bashungwa ameeleza kuwa amepokea maombi ya kuunganisha Wilaya ya Makete na Busokelo mkoani Mbeya na tayari usanifu unakwenda kuanza kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha changarawe.

Naye, Mbunge wa Makete, Festo Sanga ameiomba Serikali kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwani ni kiungo muhimu kiuchumi kati ya mkoa wa Njombe na Mbeya

Akitoa taarifa ya mradi, Kaimu Mkurugenzi wa Miradi kutoka TANROADS, Mhandisi Jephason Nko, ameeleza kuwa mradi huo mpaka sasa umefikia asilimia 4.2 ambapo unasimamiwa na Kitengo cha TECU kutoka wakala huo huku ukitarajiwa kukamilika ifikapo Julai 2026.
WhatsApp Image 2024-01-22 at 16.47.35.jpeg
WhatsApp Image 2024-01-22 at 16.47.36.jpeg
WhatsApp Image 2024-01-22 at 16.47.36(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-01-22 at 16.47.36(2).jpeg
WhatsApp Image 2024-01-22 at 16.47.37.jpeg
WhatsApp Image 2024-01-22 at 16.47.37(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-01-22 at 16.47.38.jpeg
 
Back
Top Bottom