😅😅 Chawaaa mnaumaaaa Dr Bashiru mwenye amesha puliza dawa... Mtakufa kimya kimya...Friends and Our Enemies,
Kuna msemo wa wanazuoni unaosema kwamba chochote kinamchomfaa mamba Kwa kuliwa either kiwe kimetumbukia mtoni au kimekaa kihasara hasara kwenye kingo za mto mamba hatafanya ajizi,atakifanya kuwa ni chakula tuh.
Nimebahatika kuwa ni miongoni ambao nimepata kumshuhudia BASHIRU akiwa mwanaharakati enzi zile Yuko Chuo Kikuu huku akisimama Kawa hoja za weledi pamoja na sisi walalahoi, Kisha akiwa ni kiongozi mwenye Mamlaka makubwa ndani ya Chama na Serikali enzi ya Magufuli, na kipindi hiki ambacho hana mamlaka yoyote zaidi tu ya huu ubunge wa kuteuliwa, Kwa hakika na pasipo na shaka yoyote naweza kusema ya kwamba BASHIRU halisi ni yule ambae alikuwa ni Katibu Mkuu wa CCM na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Magufuli.
Kwa kifupi kabisa huyu ni mamba tuh mwenye njaa, haijalishi anasimama kueleza ukweli au kukemea uovu mtu huyu anakosa kabisa kabisa justification ya kusimama na kusema chochote labda kama ni kuomba radhi kwa matendo ambayo alishiriki ya kukandamiza demokrasia na uhuru wa habari kipindi hiko akiwa anaogelea kwenye mto wenye kila neema maishani mwake.
Anasimama Leo kutetea wakulima, na kuwaambia WAWE wakali ili waweze kusaidiwa sawa, yuko sahihi, alikuwa wapi kusimama na sisi kipindi korosho zetu zinachukuliwa na Serikali ambayo alikuwa anaisimamia huku wengine tukiambiwa hatulipwi pesa zetu hadi tuoneshe wapi yalipo mashamba ya hizo korosho?
Hivi anafahamu ni kwa kiasi gani amegharimu maisha na matumaini ya wakulima kipindi kile hadi kufikia kuwa watu omba omba had hivi Leo?
Kusimama Leo BASHIRU na kusema kwamba anachukizwa na kauli ya kusema kwamba Samia anaupiga mwingi ni dalili ya Mamba mwenye Njaa tuh, kipindi Magufuli yupo hai na watu tunalalamika vyuma vimekaza ni yeye na wenzake ndiyo walikuwa wanaimba hii nyimbo ya kwamba Magufuli anaupiga mwingi, kipi sasa kinachomshangaza?
BASHIRU alifikia hatua ya kusema kwamba wao ndiyo wenye Dola, kwa hiyo atatumia vyombo vya Dola kubakia kwenye Dola kwani siku akiacha kutumia vyombo vya Dola akatoka madarakani basi hawezi Tena kurudi kwenye Dola, na suala la Katiba Mpya na tume huru ya uchaguzi hataki kusikia.
Hakuna tofauti baina ya BASHIRU na Ndugai, ni wale wale Mamba waliotufikisha sehemu mbaya katika awamu Yao, kabla ya hawa kusimama na kukosoa wanatakiwa kwanza kusimama na kuomba radhi na wajutie matendo Yao, hadi tutapokubaliana kuwa tumewasamehe kisha wakae kando na waache watu wengine waendelee kufanya kazi na kutekeleza maono yao ya kiutawala na uongozi.