Bashiru Ally: Nilitamani kujiuzulu Ukatibu Mkuu wa CCM

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Dk Bashiru Ally amesema wadhifa alionao ulikuwa mzigo kwake na ilifikia wakati alitaka kujiuzulu lakini alipewa moyo na mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli na watu wake wa karibu.

Dk Bashiru ametoa kauli hiyo jana Jumatano Agosti 28, 2019 katika Shule ya Msingi Ubungo Kisiwani katika siku ya pili ya ziara yake jimbo la Ubungo.

“Siasa za kiutendaji na usimamizi wa chama kikubwa kama hiki nina umri wa mwaka mmoja, nilikejeliwa sana nikaitwa majina ya uonevu wakati mwingine nampigia mwenyekiti (Magufuli) hii kazi uliyonipa vipi.”

“Mtoto wangu mkubwa alisema kama angekuwa na hiari kuamua kazi inayonifaa angeniambia baba achana na kazi hii (ya ukatibu mkuu), Magufuli alinishauri maana anajua misukosuko ya uongozi,” amesema Dk Bashiru.

Pia, aliwataja mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na wa Mbeya, Albert Chalamila kwamba wanatakiwa kurejea shule kusoma somo la uongozi.
 
Hao wanaompa misukosuko na kumkejeli amesema ni wa ndani ya chama au nje? Maana kama ni wa ndani basi inaonyesha kuna watu hawamkubali
 
Kwake sahihi ni chuoni akafundishe siasa,siasa zake zilifaa zama za kina makamba baba,hizi za mwendo kasi heri akalinde heshima yake,komborela likifunguliwa watu waanze kutema nyongo hatoweza.

CCM mpya haiamini kwenye siasa safi za Hoja za kuuza Sera inaamini kwenye matumizi ya nguvu na kubebwa na dola.Yeye ni Muumini wa siasa safi za Hoja atoweza kwendana na ccm ya mwendokasi.
 
SIASA YA MWENDOKASI,SIASA YA KUBEBWA NA DOLA,Bashiru alizoea siasa ya hoja,hi ya mwendokasi yakina ngosha haiwezi,yeye na polepole wanapaswa kukaa nje ya ulingo wanajivunjia heshma zao bure
 
Kwa kitendo chake cha kuwataka Makonda na Chalamila kurudi shule kusomea somo la uongozi, kinahitaji mjadala mpana sana! Mtu mwingine anaweza akahisi Katibu Mkuu anamkosoa Mwenyekiti wake 'indirectly' kwa kuteua watu ambao kimsingi hawana sifa ya uongozi bila shaka.

Na pia kwa aina hii ya vyeo, nadhani hatuna budi kama Taifa kuendelea kuipigia kelele Rasimu Ya Katiba ya Jaji Warioba, ijadiliwe upya ili tuwe na katiba sahihi isiyompa mamlaka mtu mmoja tu kuteua watu anaowapenda yeye hata kama hawana tija/faida kwa Taifa.
 
Kwa mazingira ya sasa yeyote akipewa nafasi hiyo atapata msongo na shida. Kitatu cha ukatibu mkuu ccm ni oversize xxx. Tatizo cheo hicho sio compatible with either the top or the bottom now.... So a stable and confinent one hatakuwa na kosa kuamua.
Hao wanaompa misukosuko na kumkejeli amesema ni wa ndani ya chama au nje? Maana kama ni wa ndani basi inaonyesha kuna watu hawamkubali
 
Naona umemwelewa vizuri sana. anamlaumu mkuu wake indirectly. Kwamba kimsingi anashindwa kufanya kazi naye maana kile anachoona ni tatizo mkuu anaona kinafaaa. Hao wakuu angekuwa na mamlaka angewaondoa lakini mkuu anawakubali kwa hiyo ni mengi kama hayo. Yeye sio compatible with his boss.
Kwa kitendo chake cha kuwataka Makonda na Chalamila kurudi shule kusomea somo la uongozi, kinahitaji mjadala mpana sana! Mtu mwingine anaweza akahisi Katibu Mkuu anamkosoa Mwenyekiti wake 'indirectly' kwa kuteua watu ambao kimsingi hawana sifa ya uongozi bila shaka.

Na pia kwa aina hii ya vyeo, nadhani hatuna budi kama Taifa kuendelea kuipigia kelele Rasimu Ya Katiba ya Jaji Warioba, ijadiliwe upya ili tuwe na katiba sahihi isiyompa mamlaka mtu mmoja tu kuteua watu anaowapenda yeye hata kama hawana tija/faida kwa Taifa.
 
Anachotafuta atakipata, nafasi hiyo ataachishwa muda sio mrefu. Anapingana indirectly na aliyemteua? Jukwaa LA walimu wakereketwa Wa ccm analianzisha Polepole yeye analikataza. Walimu wakereketwa wamesema wataendelea , ajue hayo ni maagizo kutoka Juu walimu waendelee.

Raha sana, kumbe hata awamu ya tano wachezaji hawachezi ngoma moja. Mimi nilidhani ni awamu zilizopita tu ndio watendaji wanatofautiana hivyo? Boss atatumbua hadi achoke.

Lakini hata wanaounga mkono wajue awamu ya NNE toka inaingia hadi inatoka wafanyakazi walipanda mishahara kila mwaka na ukiangalia salary slip za wafanyakazi JK kama aliingia ukuwa na mshahara unapata 400,000/_ ameondoka unapata 1,600,000/_ kama ulikuwa Mwalimu.

Sasa hii awamu haijaongeza ngazi, wala nyongeza ya mwaka. Sasa walimu mnaokiuka katiba kwa kuunga juhudi ni faida gani mumepata, tuelezeni na sisi tuunge juhudi.

Kama ni barabara za mkoa hadi mkoa , zote kaanzisha JK , awamu ya tano hata viporo vilivyobaki wameshindwa kumalizia.

Haya tuone hiyo Stiegler Umeme, na train ya SGR kama watazimaliza itakuwa sio haba, ila nchi itakuwa hoi kwa deni LA taifa linavyopaa.

Halafu tuache kujigamba eti tunajenga kwa pesa yetu ya ndani wakati tunakopa mabenki ya biashara. Na wahanga ni wananchi ambao mzunguko wa pesa umedorora.
 
Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Dk Bashiru Ally amesema wadhifa alionao ulikuwa mzigo kwake na ilifikia wakati alitaka kujiuzulu lakini alipewa moyo na mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli na watu wake wa karibu.

Dk Bashiru ametoa kauli hiyo jana Jumatano Agosti 28, 2019 katika Shule ya Msingi Ubungo Kisiwani katika siku ya pili ya ziara yake jimbo la Ubungo.

“Siasa za kiutendaji na usimamizi wa chama kikubwa kama hiki nina umri wa mwaka mmoja, nilikejeliwa sana nikaitwa majina ya uonevu wakati mwingine nampigia mwenyekiti (Magufuli) hii kazi uliyonipa vipi.”

“Mtoto wangu mkubwa alisema kama angekuwa na hiari kuamua kazi inayonifaa angeniambia baba achana na kazi hii (ya ukatibu mkuu), Magufuli alinishauri maana anajua misukosuko ya uongozi,” amesema Dk Bashiru.

Pia, aliwataja mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na wa Mbeya, Albert Chalamila kwamba wanatakiwa kurejea shule kusoma somo la uongozi.

Bashiri ni dhaifu sana, na hana maamuzi yoyote ya maana!! CCM ni chama kilichokufa tayari, yeye analazimishwa kukifanya hai na imekuwa kazi ngumu kweli kweli!! Jambo la maana ambalo ningeweza kumsaidia ni kujizulu aendelee na mambo yake, sio kupiga tararira kuwa amechoka! Kwani ukatibu ni pumzi useme ukiuacha utakufa??!!
 
Back
Top Bottom