Bashe: Vyombo vya ulinzi na usalama vimlinde mgombea wa CHADEMA jimbo la Ukonga

Ketoka

JF-Expert Member
Sep 23, 2015
1,087
1,913
Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe, amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kutoa ulinzi wa kutosha kwa mgombea ubunge wa Jimbo la Ukonga kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Asia Msangi ili kuondoa uzushi kuwa mgombea huyo anataka kutekwa.

Ameyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni za jimbo hilo uliofanyika Mziga Mwanagati, jijini Dar es Salaam, ambapo Bashe amesema kuwa kuna taarifa zimetolewa na watu wa Chadema wakidai wamepata taarifa kuwa mgombea wao atatekwa, hivyo ni vyema vyombo vya ulinzi na usalama vikahakikisha vinamlinda.

Amesema kuwa si vyema kupuuza maneno hayo kwani wakati wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kinondoni walipuuza yakatokea maafa.

“Nimesikia wakitoa hoja kuwa CCM wanataka kumteka mgombea wao, vyombo vya ulinzi naomba mtoe ulinzi kwa huyu dada alindwe kuanzia nyumbani kwake, kwenye gari na kwenye kampeni ili isije ikafika mahali wakaanza kusema ametekwa,” amesema Bashe.

Pamoja na mambo mengine, Bashe amesema chama chao kimejipanga hivyo ni vyema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakatenda haki.

Aidha, Bashe amewataka viongozi wa upinzani kuacha kusema kuwa wanaohamia CCM wamenunuliwa kwani kuna wengi wamehama chama tawala na kwenda upinzani lakini hakuna aliyesema amenunuliwa.

Hata hivyo, kwa upande wake Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde, amesema tatizo la upinzani wakipelekewa ulinzi wanasema CCM imewapelekea mashushushu
 
Bora uwe kichaa na kaelimu angalau kidogo
Kichaa ni kichaa tu, tena bora kichaa ambaye hajasoma kuliko kichaa aliyepita shule kidogo, fanya uchunguzi wa vichaa unaowajua hawajasoma uone na ulinganishe na waliopita shule kidogo
 
Mwenye digiriiiii ni afadhali kuliko darasa la saba
 
Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe, amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kutoa ulinzi wa kutosha kwa mgombea ubunge wa Jimbo la Ukonga kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Asia Msangi ili kuondoa uzushi kuwa mgombea huyo anataka kutekwa.

Ameyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni za jimbo hilo uliofanyika Mziga Mwanagati, jijini Dar es Salaam, ambapo Bashe amesema kuwa kuna taarifa zimetolewa na watu wa Chadema wakidai wamepata taarifa kuwa mgombea wao atatekwa, hivyo ni vyema vyombo vya ulinzi na usalama vikahakikisha vinamlinda.

Amesema kuwa si vyema kupuuza maneno hayo kwani wakati wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kinondoni walipuuza yakatokea maafa.

“Nimesikia wakitoa hoja kuwa CCM wanataka kumteka mgombea wao, vyombo vya ulinzi naomba mtoe ulinzi kwa huyu dada alindwe kuanzia nyumbani kwake, kwenye gari na kwenye kampeni ili isije ikafika mahali wakaanza kusema ametekwa,” amesema Bashe.

Pamoja na mambo mengine, Bashe amesema chama chao kimejipanga hivyo ni vyema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakatenda haki.

Aidha, Bashe amewataka viongozi wa upinzani kuacha kusema kuwa wanaohamia CCM wamenunuliwa kwani kuna wengi wamehama chama tawala na kwenda upinzani lakini hakuna aliyesema amenunuliwa.

Hata hivyo, kwa upande wake Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde, amesema tatizo la upinzani wakipelekewa ulinzi wanasema CCM imewapelekea mashushushu
Hana lolote kwani kuna uchaguzi hapo? Ni wizi tu wa kura ili mradi msaliti apite
 
kumsimamisha mgombea yuleyule aliyejiuzulu ubunge agombee tena nafasi hiyo kwa chama tofauti sio tu ni dharau kwa wapiga kura bali ni ushamba wa kisiasa wa hali ya juu sana. ni dharau na kiburi kilichopitiliza kwamba watatufanya nni?
Sio jambo geni katika siasa za dunia Vladmir Putin baada ya kushindwa uraisi akagombania uwaziri mkuu
 
alijiuzulu kumuunga mkono nani? acha uzuzu wewe! mwita waitara alikuwa mbunge hapo ukonga akashindwa kabisa kufanya lolote leo kahama chama mnamsimamisha agombee hapohapo SIO TU NI USHAMBA WA KISIASA BALI NI DHARAU KUBWA SANA KWA WALIOMCHAGUA.
 
Back
Top Bottom