Bashe: Vyombo vya ulinzi na usalama vimlinde mgombea wa CHADEMA jimbo la Ukonga

Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe, amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kutoa ulinzi wa kutosha kwa mgombea ubunge wa Jimbo la Ukonga kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Asia Msangi ili kuondoa uzushi kuwa mgombea huyo anataka kutekwa.

Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni za jimbo hilo uliofanyika Mziga Mwanagati, jijini Dar es Salaam jana Jumatatu Septemba 10, Bashe alisema kuna taarifa zimetolewa na watu wa Chadema wakidai wamepata taarifa kuwa mgombea wao atatekwa, hivyo ni vyema vyombo vya ulinzi na usalama vikahakikisha vinamlinda.

Bashe alisema si vema kupuuza maneno hayo kwani wakati wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kinondoni walipuuza yakatokea maafa.

“Nimesikia wakitoa hoja kuwa CCM wanataka kumteka mgombea wao, vyombo vya ulinzi naomba mtoe ulinzi huyu dada alindwe kuanzia nyumbani kwake, kwenye gari na kwenye kampeni ili isije ikafika mahali wakaanza kusema ametekwa,” alisema Bashe.

Pamoja na mambo mengine, Bashe amesema chama chao kimejipanga hivyo ni vyema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakatenda haki.

“Naiomba NEC itende haki ili ikifika siku ya uchaguzi Septemba 16 upinzani wasipate sababu ya kufanya vurugu,” alisema.

Aidha, Bashe amewataka viongozi wa upinzani kuacha kusema kuwa wanaohamia CCM wamenunuliwa kwani kuna wengi wamehama chama tawala na kwenda upinzani lakini lakini hakuna aliyesema amenunuliwa.

“Kati ya waliowahi kuhama upinzani ni pamoja na Mgombea wa CCM wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara, Mgombea wao wa Monduli, Julius Kalanga na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa. Naomba wapinzani watuambie waliwapa Sh ngapi hawa?

“Vyama vya siasa ni sawa na gari unapanda likupeleke mahali, ukiona halikufikishi unashuka, ndivyo alivyofanya Waitara,” alisema Bashe.

Alisema kwa sasa CCM ndiyo chama pekee chenye demokrasia ambapo kinaruhusu kukosoana, kuzungumza na Waziri Mkuu yupo, jambo ambalo Chadema hawawezi.

“Huko kwao hakuna hayo mambo, ni zidumu fikra za mwenyekiti kwa hiyo naomba waangalie nyumba yao waache haya mambo ya kusema watu wamenunuliwa,” alisema Bashe.

Source : MPEKUZI |Tanzania Entertainment News,Politics News ,Celebrity Gossip and Live Updates
 
Bashe anauma na kupulizia, ila ni muadilifu sana na mpenda haki , na laiti kama angekuwa mwekiti wa NEC Nina hakika angeweza kutenda haki.
 
Wajaribu kufanya hivyo ili tuone uhalisia
 
Siku hizi Ccm ni wepesi sana kama pamba,na wenyewe wanajua bila msaada wa wakurugenzi na polisi hawachomoki
 
Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe, amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kutoa ulinzi wa kutosha kwa mgombea ubunge wa Jimbo la Ukonga kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Asia Msangi ili kuondoa uzushi kuwa mgombea huyo anataka kutekwa.

Ameyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni za jimbo hilo uliofanyika Mziga Mwanagati, jijini Dar es Salaam, ambapo Bashe amesema kuwa kuna taarifa zimetolewa na watu wa Chadema wakidai wamepata taarifa kuwa mgombea wao atatekwa, hivyo ni vyema vyombo vya ulinzi na usalama vikahakikisha vinamlinda.

Amesema kuwa si vyema kupuuza maneno hayo kwani wakati wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kinondoni walipuuza yakatokea maafa.

“Nimesikia wakitoa hoja kuwa CCM wanataka kumteka mgombea wao, vyombo vya ulinzi naomba mtoe ulinzi kwa huyu dada alindwe kuanzia nyumbani kwake, kwenye gari na kwenye kampeni ili isije ikafika mahali wakaanza kusema ametekwa,” amesema Bashe.

Pamoja na mambo mengine, Bashe amesema chama chao kimejipanga hivyo ni vyema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakatenda haki.

Aidha, Bashe amewataka viongozi wa upinzani kuacha kusema kuwa wanaohamia CCM wamenunuliwa kwani kuna wengi wamehama chama tawala na kwenda upinzani lakini hakuna aliyesema amenunuliwa.

Hata hivyo, kwa upande wake Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde, amesema tatizo la upinzani wakipelekewa ulinzi wanasema CCM imewapelekea mashushushu
Huyu mso ... nae kasikia udaku anakuja mbio na udaku wake,akamlinde yeye
 
Sina chama lakini, siungi mkono Waitara kupewa nafasi ya kugombea pale pale na jimbo lile lile alilolitwaa kwa CDM.
Kulitokea nini hadi ang'atuke?? Kumetokea nini arudi kivile?? Ni maswali ambayo hadi sasa bado hajayajibu.
 
Bashe naye kaanza kufikili kwa kutumia makalio ........

wakina nasari wana ushahidi mpaka wa video .....

lakini bado mnaongea siasa....................

kweli ukiwa ccm lazima ujitoe ufahamu.
 
Back
Top Bottom