MGOGOHALISI
JF-Expert Member
- Apr 16, 2011
- 4,479
- 6,532
Wanatafiti au wanazileta tu 🤣🤣🤣🤣🤣My Take
Nilitarajia Nguvu kubwa iwekezwe kwenye Benki ya mbegu za asili za mazao mbalimbali ambazo ziko hatarini kutoweka na kuzibiresha hizo badala ya hizi za GMO.
Ni vyema tukajua kama huu ndio msimamo wa Serikali.
Soungi mkono hoja hata kidogo 👇👇
SERIKALI imetangaza rasmi kuanza kuvitumia Vituo vya Utafiti vya Mikocheni cha Jijini Dar es Salaam na Makutupora cha Jijini Dodoma kwaajili ya kufanya majaribio na utafiti wa mbegu zenye vinasaba vya uhandisi jeni maarufu kama GMO.
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema hayo leo Oktoba 16,2024 wakati akizungumza na wanajumuiya wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA.
Wanajumuiya hao ni wanataaluma, wadau waliowahi kusoma na kufanya kazi katika chuo hicho katika halfa iliyotanguliwa awali na utoaji wa zawadi kwa wanafunzi na wahadhiri waliofanya vizuri kitaaluma.
Waziri Bashe amesema serikali wameridhia uamuzi huo licha ya kwanza teknolojia hiyo haijaruhusiwa rasmi matumizi yake nchini kwa lengo la kujiweka tayari kwa kuwa na wataalamu watakaokuwa tayari wakati wowote.
Nipashe