Bashe: Tumeanza Utafiti wa Mbegu za GMO

Bashe: Tumeanza Utafiti wa Mbegu za GMO

Mbegu za GMO ni kweli kila utafiti khs madhara na faida zake ya hizi mbegu duniani....Faida zake ni ndogo sn na madhara yake ni makubwa. Tubaki na mbegu zetu za asili. Mh Bashe kwa hili tafakari sana. Maamuzi yetu ya sasa yanaweza kutuletea madhara ya vizazi vijavyo..
 
Madhara ya mbegu za GMO ni yapi??
 
Naamini unaelewa vizuri jinsi mbolea flani na dawa za kuulia wadudu zinavyoifanya ardhi iwe tasa...Sasa kikubwa kuna watu kama bill gates wengi hawamjui kwamba ni mbwa alievaa ngozi ya kondoo...Anatamani aone kila mwanaume ni shoga kutokana na mutation inayotokana na chanjo na mazao ya kinafki anayojidai ni ya msaada...Viongozi wa tanzania wasiojali watu wake wanamkaribisha panya mharibifu bill gates kuja kuwekeza tanzania...Kwa nini hizo mbegu za kinafki asibadilishe mazao ya biashara tu kama pamba na mkonge,,,anakimbilia kwenye chakula tu huyo sheytwani kaona nini???
Hakuna mbolea au dawa za wadudu zinazosababisha ardhi kuwa tasa, kwanza kufikiria tu kwamba ardhi inaweza kuwa tasa ni ufinyu akili.
Halafu Bill Gates atafaidika nini wanaume wote mkiwa mashoga?? Ujinga mtupu
 
My Take
Nilitarajia Nguvu kubwa iwekezwe kwenye Benki ya mbegu za asili za mazao mbalimbali ambazo ziko hatarini kutoweka na kuzibiresha hizo badala ya hizi za GMO.

Ni vyema tukajua kama huu ndio msimamo wa Serikali.

Soungi mkono hoja hata kidogo .Pia soma Bill Gates "Afrika kuna njaa na Utapiamlo, Mazao ya GMO yatawasaidia. Je, hii si kauli ya dharau kwa Waafrika?

SERIKALI imetangaza rasmi kuanza kuvitumia Vituo vya Utafiti vya Mikocheni cha Jijini Dar es Salaam na Makutupora cha Jijini Dodoma kwaajili ya kufanya majaribio na utafiti wa mbegu zenye vinasaba vya uhandisi jeni maarufu kama GMO.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema hayo leo Oktoba 16,2024 wakati akizungumza na wanajumuiya wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA.

Wanajumuiya hao ni wanataaluma, wadau waliowahi kusoma na kufanya kazi katika chuo hicho katika halfa iliyotanguliwa awali na utoaji wa zawadi kwa wanafunzi na wahadhiri waliofanya vizuri kitaaluma.

Waziri Bashe amesema serikali wameridhia uamuzi huo licha ya kwanza teknolojia hiyo haijaruhusiwa rasmi matumizi yake nchini kwa lengo la kujiweka tayari kwa kuwa na wataalamu watakaokuwa tayari wakati wowote.

Nipashe
Shida ya waafrika kutaka kujaribu kila kitu. Huko zilipoanzia hawazitaki. Kwani mbegu sasa hivi zina tatizo gani hadi serikali ianze majaribio ya mbegu za GMO.
 
Unafikiri punda walikuwa na tatizo gani watu wakahamia kwenye magari?
Magari yalikuwa na shinda gani watu wakahamia kwenye ndege?
Umeme wa diezel ulikuwa na shida gani watu wakahamia kwenye maji, solar na nuclear?
Kuni zilikuwa na shida gani watu wakahamia kwenye gesi??
 
Wewe mwenyewe mbona unapigwa Sindano tangu unazaliwa mpaka utakapoingia kaburini.

Kwani umeambiwa kuna mtu anataka kukunyang'anya mbegu zako za asili??
Wewe si uendelee kuzitumia, na wanaotaka kutumia nyingine nao waachwe watumie.
Wewe unataka kubugia chungwa la GMO?
 
Hatari sana...
Ardhi yetu wala haitaji GMO...

Cc: Mahondaw
Mkuu no place to hide,jirani yetu Uganda amefanya utafiti kupitia taasisi zake kitambo,anachosubiri rasmi kutumia hiyo GMO ni idhini ya Bunge.

Kenya nako alipoingia madarakani Raisi Ruto alitamani kulima mahindi ya GMO ili kukabili njaa inayowaandama kila wakati.
Nchi yetu yenye uzembe,uvivu,ulaghai uliokubuu una uhakika gani katika usimamizi wa kuzui mbegu za GMO au labda ipo sokoni bila kujitambua?

GMO sio rocket science zipo kitabo sana katika nchi kubwa kiuchumi. Ni bora tafiti za kina zikapewa nafasi ili kugundua ubaya na ubora wake nchini kwetu.
 
Huwezi kumkuta samia au bashe anabugia CHUNGWA LA GMO.

Wao wanakula vitu nachuro, ila haya MAGMO ndio wanatusukumia sisi.

We Bashe UTUKOME na MACHUNGWA YAKO YA PLASTIKI.

Khaaaa.... CHUNGWA linadungwa SINDANO, una wazimu?

Cc: Yoda Extrovert
 
Mkuu no place to hide,jirani yetu Uganda amefanya utafiti kupitia taasisi zake kitambo,anachosubiri rasmi kutumia hiyo GMO ni idhini ya Bunge.

Kenya nako alipoingia madarakani Raisi Ruto alitamani kulima mahindi ya GMO ili kukabili njaa inayowaandama kila wakati.
Nchi yetu yenye uzembe,uvivu,ulaghai uliokubuu una uhakika gani katika usimamizi wa kuzui mbegu za GMO au labda ipo sokoni bila kujitambua?

GMO sio rocket science zipo kitabo sana katika nchi kubwa kiuchumi. Ni bora tafiti za kina zikapewa nafasi ili kugundua ubaya na ubora wake nchini kwetu.
Acha uvivu KALIME.

Usipende DEZO LA MAGMO
 
GMO zina madhara kiafya,kwani wizara ya afya inasemaje?wizara ya kilimo na ya afya zishirikiane kabla ya kuruhusu?wataalamu wa afya wanajua watatusaidia kuona kama tuko tayari kukabiliana na madhara yatakayotokana na hizo GMO.
 
GMO zina madhara gani?
 
My Take
Nilitarajia Nguvu kubwa iwekezwe kwenye Benki ya mbegu za asili za mazao mbalimbali ambazo ziko hatarini kutoweka na kuzibiresha hizo badala ya hizi za GMO.

Ni vyema tukajua kama huu ndio msimamo wa Serikali.

Soungi mkono hoja hata kidogo .Pia soma Bill Gates "Afrika kuna njaa na Utapiamlo, Mazao ya GMO yatawasaidia. Je, hii si kauli ya dharau kwa Waafrika?

SERIKALI imetangaza rasmi kuanza kuvitumia Vituo vya Utafiti vya Mikocheni cha Jijini Dar es Salaam na Makutupora cha Jijini Dodoma kwaajili ya kufanya majaribio na utafiti wa mbegu zenye vinasaba vya uhandisi jeni maarufu kama GMO.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema hayo leo Oktoba 16,2024 wakati akizungumza na wanajumuiya wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA.

Wanajumuiya hao ni wanataaluma, wadau waliowahi kusoma na kufanya kazi katika chuo hicho katika halfa iliyotanguliwa awali na utoaji wa zawadi kwa wanafunzi na wahadhiri waliofanya vizuri kitaaluma.

Waziri Bashe amesema serikali wameridhia uamuzi huo licha ya kwanza teknolojia hiyo haijaruhusiwa rasmi matumizi yake nchini kwa lengo la kujiweka tayari kwa kuwa na wataalamu watakaokuwa tayari wakati wowote.

Nipashe
My Take
Nilitarajia Nguvu kubwa iwekezwe kwenye Benki ya mbegu za asili za mazao mbalimbali ambazo ziko hatarini kutoweka na kuzibiresha hizo badala ya hizi za GMO.📌📌
 
GMO zina madhara gani?
 
Back
Top Bottom