Kikwete mbunifu sana wa mbinu za kugonganisha vichwa halafu yeye anakaa kando akichekelea mambo yanavyoenda. Alijua fika kilichoendelea ndani ya CCM wakati Sitta, Nape na Mpendazone wakihaha kuanzisha CCJ, yeye akawatibua kwa kumpa cheo Nape kuwa mkuu wa wilaya na hivyo kuwa bizu na shughuli za serikali na papo hapo akiwa chini ya usimamizi wa vyombo vya usalama kama mkuu wa wilaya. alishinda kwa hilo. Pamoja na kukwamba kumtoa Sitta kwa vile ndani ya vikao alikuwamo basi vita vikaishia kumwengua kwenye uspika na kumweka kilaza atakayefanya kila anachotaka bungeni.
Lengo la kikwete kumnyanyua Nape kwenye nafasi nyeti Chamani ilikuwa kumthibiti, lakini undani wa Nape na Kikwete wanatofautiana kwa kiasi kikubwa, ingawa kikwete kamnyanyua Nape ili kumthibiti lakini kiitikadi wanatofautiana. Matokeo yake ndio haya vijembe vya Nape kwa mwenyekiti wake vimeanza. Na kinachomlinda Kikwete ni kinga ya Urais vinginevyo yangeshampata mambo zaidi ya hawa mapacha watatu.
Kujiengua kwa Rostam Aziz madhara yake ni makubwa ndani ya CCM maana huyu anajua siri nyingi na udhaifu mwingi wa viongozi wengi wa CCM kuanzia ngazi ya juu. Sitashangaa CCM sasa kutengeneza maadui wengi ndani ya chama chao wenyewe kutokana na itikadi za makundi, na makundi ndiyo yanayozidi kukidhoofisha chama.
Yanayotokea kujivua magamba kwa kunyoosheana vidole majukwaani na kwenye vyombo vya habari ni dalili za wazi mmommonyoko wa hekima na busara ndani ya CCM iliyojengeka miaka mingi. Ububu wa mwenyekiti wa chama nao ndio umesababisha ufa mkubwa ambao kuzibika kwake ni ziada isiyofikirika kwa urahisi. Uadui ndani ya CCM pamoja na uroho wa vyoe ambao umeonyesha dhahiri kuwepo na cheo ni njia rahisi ya kujichotea mapesa ya wavuja jasho sasa vinapelekesha CCM mchakamchaka ambao hauonyesha dalili za lini wataweka kituo cha kurushiana makonde.
Biashara na Siasa haviendani, na kama Rostam alivyoamua kuachia yote kwa ajili ya biashara zake nampongea ni uamuzi mgumu unaotakiwa kwa manufaa yake binafsi, familia yake na taifa kwajumla. Maana kwa mazingira yaliyokuwepo kila lililofanywa na ye yote Rostam alionekana kama ndiye mbunifu. Tusubiri mengine yaja. Na kosa kubwa la CCM kuweka vuvuzela lisilotumia hekima na busara, na afadhali Mkama angekuwepo vinginevyo mambo yangezidi kuharibika na huyu kijana motomoto Nauye Nape.