Bashe achangia 500,000 “Join the Chain”

Bashe achangia 500,000 “Join the Chain”

Ni jambo jema sana kuwahabarisha watanzania ili wajue tunaelekea wapi.
Ukombozi unaotafutwa na watanzania si wa kificho....................... mambo yote unaweka hadharani watu wapime wenyewe....................... isitoshe function nzima ilihudhuriwa na waandishi wengi kutoka vyombo mbali mbali vya habari isipokuwa tbc
Tunge wakimbiza....
 
Siku zote wachangiaji wakubwa wa CCM ni wahindi na pesa zao safi kama theluji!, kama fedha za Kagoda zilikuwa safi, hizi za hawa wafanya biashara ni safi kabisa. Mpaka kesho, wahindi ndio most generous kuchangia CCM ukiondoa tule tumichango twa wale waarabu na tule tujisuti, michango tegemewa ni ya wafanyabiasha hawa wenzetu!.
P

michango ya M4C join the chain ilichangwa na watu kutoka kada mbalimbali bila kujali ni mfanyabiashara ama mfanyakazi...................... tena kwa mtazamo wangu nilishuhudia waliochangia 50 au 30 zao mostly ni wafanyakazi na wafanyabiashara wadogo waliochoka na mfumo mbovu wa utawala wa tanzania chini kiongozi dhaifu ambaye most of his time ame spend maisha yake kwenye ndege
 
Usiku wa kuamkia leo Kauthary Bashe aliiwakilisha familiaya Bashe kwenye fundraise ya "Join the Chain" ya M4C iliyofanyika jana SNOWCREST HOTEL Arusha na kufanikiwa kwa kiwango cha juu sana kwani ilifanikiwa kupata pesa za vifaa vya matangazo na kupelea kiasi cha milioni 5 kuweza kununua gariaina Canter itakayotumika kubebea vifaa hivyo pamoja na majiko pale kazi rasmi ya ukombozi itakapo anza mapema kabisamwakani itakayo kuwa kijiji kwa kijijijumla ya pesa zilizopatikana ni TZS 42,3000,000 huku yeye na familia Basheakitoa TZS 500,000, kamanda Godbless Lema akiongea na wageni waalikwa alisemaawali alijua familia ya Bashe ni CCM ndiyo maana alienda kuweka kambi pale UDOMkuhakikisha Abubakari Bashe mdogowake na Hussein Bashe anashindwa lakini baada ya uchaguzi na chadema ikiibukakinara, Abubakari Bashe alimfata na kumlaumu kwanini amemfanyia hivyowakati yeye ni chadema na familia yao nichadema.
Baada ya habari hizi nilianza kupitia matamko Hussein Bashenikagundua alishaanza kitambo kupasha bado maamzi mazito kuya chukua au pepeo CCM bado amemwingia ndiyo maanabado mguu ndani mguu nje


Pata moja ya habari aliyoitoa 09/2012

=======================================================

MJUMBE wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama ChaMapinduzi (UVCCM), Hussein Bashe, ameonya kuwa iwapo CCM hakitajadili matatizoya wananchi sasa, kitarajie kupoteza dola mwaka 2015, kama ilivyotokea kwachama tawala Zambia.

Akizungumza katika Kata ya Kasamwa wilayani Geita katikamaadhimisho ya miaka 33 ya kuanzishwa kwa UVCCM, Bashe alisema kuwa uchaguzi waZambia umemalizika na chama kilichoongoza kwa zaidi ya miaka 20 kimeondolewamadarakani, tukio linalopaswa kuwa funzo kwa CCM.

Alisema katika mazingira ya sasa ambayo wapiga kura wengi nivijana, CCM kinapaswa kuwasikiliza, kujadili matatizo yao na kuyapatiaufumbuzi, vinginevyo kitangoka madarakani muda mfupi ujao.

CCM kianze kujiandaa leo kwa kutoa majibu ya matatizo yavijana kinaowaongoza ikiwa ni pamoja na viongozi wake kuepuka kukaa ofisini naumangimeza kwani bila hivyo, mwaka 2015 wataanza kutafuta mchawi, alisemaBashe na kuendelea:

Kiache kutafuta mchawi mmoja mmoja, kiache kujadili watukijadili matatizo ya watu tujadili watu wanapata wapi maji, watu wanapata wapiajira, wanapata wapi zahanati na fedha zinazotengwa katika halmashauri yawilaya kwenda kwa wananchi zinawafikia haya ndiyo mambo ya msingi kabisa kamayakifanyiwa kazi CCM kitaendelea kushika dola.

Alisema wakati UVCCM leo ukisherehekea miaka 33 tangukuanzishwa kwake, viongozi wanatakiwa kujiuliza ni kwa nini watu wengihawajaichagua CCM na ni vipi vijana wengi ndiyo wanaoonekana hawataki kuiungamkono CCM. Alisema hii ndiyo changamoto kubwa inayokikabili chama hicho tawalakwa sasa.

Bashe alisema vijana wa Tanzania leo watapenda CCM kama tukitawahakikisha elimu bora, afya bora, fursa ya kufanya kazi na kujiajiri nauchumi ulio imara.

Taifa linakwenda kwenye uchaguzi mwaka 2015, kipindi hichokitakuwa na wapiga kura wapya zaidi ya milioni sita ambao wengi watakuwa niwale wenye umri wa miaka 30. Vijana hawajui habari za uhuru na amani wala nini,wanataka kusikia wamepata zahanati, elimu bora na wamepata fursa za kufanyakazi basi, hapo ndipo chama kitakuwa kimejibu matatizo yao.

Alisema CCM ya leo siyo ile ya miaka 10 iliyopita na kwambandani yake kumejaa migawanyiko mingi aliyoieleza kuwa haina maslahi kwa watuwanaowaongoza huku, akisema kumejaa mizengwe mingi na matokeo yake watu wamekuwawakikimbilia upinzani.

Lazima tujiulize maswali kulikoni hali hii? Lakini majibutunayo ni kwa sababu UVCCM imeshindwa kufikia mahitaji ya vijana wengi na sasawanakichukia chama hiki.

Alisema vijana wengi wamezaliwa na kukua na kuukuta uhuruambao leo, unasherehekewa na taifa kutimiza miaka 50. Wakati huo vijana wa CCMnao wakisherehekea miaka 33 ya kuzaliwa umoja wao, uhuru huo umetokana jitihadabinafsi za wazee na vijana wa wakati ule, vijana wa sasa hawana habari nauhuru.

Nimeambiwa CCM tulishindwa uchaguzi katika Kata ya Kasamwatuliyopo ambayo tunaadhimisha miaka 33 ya umoja wetu. Kata ipo chini ya Chademana nimeambiwa hapa kumewahi kutokea vurugu. Labda niseme jambo moja kuwaambiaKasamwa uamuzi mlioyafanya wa kuchagua kutoka Chadema ni wenu na ndiyodemokrasia. Mmempa udiwani mbaye hatokani na CCM, lakini niwaombe tofauti zakisiasa zisiwagawe kufikia hatua ya kushambuliana.

Nilipata taarifa kwamba mlifikia hatua ya kuchomeana nyumbahapa Kasamwa. Niwaombe vijana wenzangu haya maslahi ya kisiasa yasitugawevijana wenzangu, tutofautiane kwa sera na itikadi, lakini tusivurugane,haisaidii mtu yeyote ikitokea vurugu hapa na vijana ndiyo watakuwa wa kwanzakuathirika.

Alisema viongozi wa UVCCM wanapaswa kuepuka Ndiyo mzeebali kuhakikisha wanazibana halmashauri za wilaya zifanye kazi ambayo itasaidiakuleta maendeleo kwa wananchi na vijana kwa ujumla na alionya kuwa CCMkinapaswa kuhakikisha kuwa maeneo yaliyochukuliwa na upinzani hayaachwi kwakuhakikisha kinafikisha maendeleo.

42,3000,000
 
Abubakar Bashe kijana shupavu na mwenye weledi mkubwa katika siasa safi,alama ya viongozi bora katika taifa letu siku za mbeleni,nimemfahamu vizuri nikiwa pale chuoni UDOM na hasa pale alipogombea urais serikali ya Wanafunzi Udom ijapokuwa Mungu hakupenda riziki iwe upande wake ila naamini ipo siku atakuwa msaada mkubwa kwa nchi yetu ya Tanzania.
 
Abubakar Bashe kijana shupavu na mwenye weledi mkubwa katika siasa safi,alama ya viongozi bora katika taifa letu siku za mbeleni,nimemfahamu vizuri nikiwa pale chuoni UDOM na hasa pale alipogombea urais serikali ya Wanafunzi Udom ijapokuwa Mungu hakupenda riziki iwe upande wake ila naamini ipo siku atakuwa msaada mkubwa kwa nchi yetu ya Tanzania.

Alipigwa chini na historia......................... kumbe jamaa mwenyewe ni kamanda
 
Kesho Hussein Bashe, atatoa press release yake, kwenye gazeti la Mtanzania, kukanusha kuhusika na huo mchango wa 500,000 toka familia ya Bashe kwenda Chadema!. Atakacho fanya ni kuji disassociate na huo mchango hata kama at the end of the day, hizo fedha zote katoa yeye!. That is politics!.

Angalau Sabodo ndiye kada wa CCM pekee aliye bold enough kutoa fedha Chadema publically!. yule Tajiri mwingine ambaye yuko CCM nae pia ni mfadhili mzuri tuu wa Chadema on low profile!. That is politics!.

Chadema wakijipanga vizuri kuonyesha seriousness kuingia Ikulu 2015, wafanya biashara wengi tuu haswa wahindi watatuma michango yako mapema ili kujiposition vizuri kabla, maana you never know with politics!.
P.

Pasco,
Bandiko lako hili linaleta picha siyo nzuri kisiasa kwa CHADEMA.

Unataka kuuaminisha umma kuwa CHADEMA nao ni walewale kama CCM kwa sababu kama mpenzi au mfanyabiashara hajitokezi hadharani kukichangia chama cha upinzani badala yake anafanya kwa kupitia chini ya meza basi huyo ana uwalakini katika maisha na biashara zake. Pia kama mfanyabiashara anasubiri mpaka aone chama kimekuwa na mtaji mkubwa wa kisiasa ndiyo akichangia pia huyo naye ana uwalakini katika mienendo yake.

Kuna maana gani basi kwa CHADEMA kupiga kelele kwa hili wakati hata wao wanapenda iwe hivyo pindi mtaji wao wa kisiasa utakapokuwa mkubwa zaidi. Huu unakuwa ni unafiki kisiasa wa kupindukia kama ndivyo wanapenda au wanafanya hivyo.

CCM imefika hapa ilipo kwa sababu pesa imekuwa ndiyo sauti katika chama na serikali yake.

Bandiko lako hili lina maana moja tu, unaiambia jamii kuwa CHADEMA siyo chama mbadala kwa sasa matendo yake pindi wanakapokuwa na mtaji hasa wa kisiasa yatakuwa kama ya CCM.

Kumbe siasa safi ni maneno matupu. Ama kweli siasa za Tanzania siyo kama tuzijuavyo.
 
Crashwise; Mungi

Nilitegemea tutapata habari hii kama tulivyopata kwani hakika muwapo mahala Mi mwenyewe nafarijika tu!

Crashwise; Mi binafsi nashukuru kwa kutupia thread hii! Asante sana kamanda!

Hakika hata Bashe ni kati ya koo ya ccm inayohitaji mabadiliko kwa sasa!
 
Last edited by a moderator:
Tarajieni kumuona Nape akiichangia Chadema kwa njia yoyote ile ilimrada asiharibu kibarua chake huko ccm
 
Tarajieni kumuona Nape akiichangia Chadema kwa njia yoyote ile ilimrada asiharibu kibarua chake huko ccm
Nnauye Jr ukimwona tu utajua anahitaji mabadiliko.................... tatizo kazi aliyopewa inabidi aropoke hata upuuzi
 
Last edited by a moderator:

......kubebea vifaa hivyo pamoja na majiko pale.... kazi rasmi ya ukombozi.... itakapo anza mapema kabisa mwakani itakayo kwa kijiji kwa kijiji...nyumba hadi nyumba...


....Crashwise....

hii imetulia sana big Excellent
makamanda!! ...inanikumbusha kule kwa Dogo janja..chakaza majangili mpaka wakasepa usiku...usiku....

.....waambie makamanda wasihofu huku vijijini tutachangia mpaka chakula....


....nakala kwa wanafiki wote wasioitakia mema chadema....
 
Familia ya bashe ni familia yenye itikaddi tofauti kuna mwanachama wa CUF Ismail Bashe ni mwanachama wa CUF anaishi Nzega, wadogo zake 3 Kaustha Bashe ,Ibrahim Bashe na Abubakar ni wanachama wa Chadema , Hussein Bashe na familia yake ni wanachama wa CCM kwahiyo ni familia yenye mitizamo tofauti kama ya nyerere mwaka 1995 Makongoro Nyerere alikuwa na mitizamo tofauti na mwl Nyerere akagombea ubunge wa Arusha mjini wa tiketi ya NCCR na akashinda, madaraka Nyerere ni mwanachama wa CDM,Mbunge wa musoma mjini ambaye pia ni mwanafamilia wa mwl Nyerere ni mwanachama wa Chadema ,katika hali ya kawaida kaustha anapotoa mchango sio kwa niamba ya bashe anatoa kwa utashi wake mwenyewe ni mtu mzima mwenye maamuzi yake leo Easter wasira anapotoa both moral and financial suport haimaanishi ni wasira katoa .
 
Pasco,
Bandiko lako hili linaleta picha siyo nzuri kisiasa kwa CHADEMA.

Unataka kuuaminisha umma kuwa CHADEMA nao ni walewale kama CCM kwa sababu kama mpenzi au mfanyabiashara hajitokezi hadharani kukichangia chama cha upinzani badala yake anafanya kwa kupitia chini ya meza basi huyo ana uwalakini katika maisha na biashara zake. Pia kama mfanyabiashara anasubiri mpaka aone chama kimekuwa na mtaji mkubwa wa kisiasa ndiyo akichangia pia huyo naye ana uwalakini katika mienendo yake.

Kuna maana gani basi kwa CHADEMA kupiga kelele kwa hili wakati hata wao wanapenda iwe hivyo pindi mtaji wao wa kisiasa utakapokuwa mkubwa zaidi. Huu unakuwa ni unafiki kisiasa wa kupindukia kama ndivyo wanapenda au wanafanya hivyo.

CCM imefika hapa ilipo kwa sababu pesa imekuwa ndiyo sauti katika chama na serikali yake.

Bandiko lako hili lina maana moja tu, unaiambia jamii kuwa CHADEMA siyo chama mbadala kwa sasa matendo yake pindi wanakapokuwa na mtaji hasa wa kisiasa yatakuwa kama ya CCM.

Kumbe siasa safi ni maneno matupu. Ama kweli siasa za Tanzania siyo kama tuzijuavyo.
Ulidhani ni tofauti?.
Katika katiba mpya, tutalazimisha mapato na matumizi ya vyama yachapishwe na kubandikwa mbao za matangazo ili kila kitu kiwe transparent!.
 
mkuu AL sadat naona umeamua kuingia mwenyewe, mtoaji alisema kwaniamba ya familia ya Bashe..lakini mwambie bashe achukue maamzi mapema gari likishaondoka asije akajuta..
 
Last edited by a moderator:
42,3000,000

vipi umeshituka ni mil 42.3 naona ni makosa ya kiuandishi.. lakini mwakani hamponi kesheni hapa jf sisi tunaingia vijiji na sembe letu na dagaa mwaka 2014 kitaeleweka tu..
 
Ulidhani ni tofauti?.
Katika katiba mpya, tutalazimisha mapato na matumizi ya vyama yachapishwe na kubandikwa mbao za matangazo ili kila kitu kiwe transparent!.

Hapa umenipiga kofi la uso.


Hapa ndiyo nimeamini Pasco wa jf hana chama lakini ni mfuasi wa siasa zenye misingi ya personality baada ya kugundua kuwa vyama vyote ni sawa, unfortunately, hizi siasa zimeanza kuitafuna CHADEMA baada ya kuzaa ubinafsi ndani ya chama.

I'm not optimistic kwa hili la kubandika mapato na matumizi ya chama kwa sababu dalili zinaonyesha kama vyama vikubwa nchini viko tayari kuwa pamoja (concoct) ili mapato na matumizi yaendelee kuwa siyo wazi. Refer, ile issue ya Nape Nnauye na Dr. Wilbroad Slaa kuhusu kupata pesa za wafadhili. Hata kwa nchi za magharibi ambazo ni magwiji wa demokrasia, bado kuna hot debate kuhusu political party donor. Kwa Tanzania itawezekana kweli wakati hata hizo pesa donor haijulikani anazitoa wapi achilia mbali matumizi ya vyama.
 
Back
Top Bottom