Bashe achangia 500,000 “Join the Chain”

Bashe achangia 500,000 “Join the Chain”

Crashwise

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
22,227
Reaction score
8,761
Usiku wa kuamkia leo Kauthary Bashe aliiwakilisha familiaya Bashe kwenye fundraise ya "Join the Chain" ya M4C iliyofanyika jana SNOWCREST HOTEL Arusha na kufanikiwa kwa kiwango cha juu sana kwani ilifanikiwa kupata pesa za vifaa vya matangazo na kupelea kiasi cha milioni 5 kuweza kununua gariaina Canter itakayotumika kubebea vifaa hivyo pamoja na majiko pale kazi rasmi ya ukombozi itakapo anza mapema kabisamwakani itakayo kuwa kijiji kwa kijijijumla ya pesa zilizopatikana ni TZS 42,3000,000 huku yeye na familia Basheakitoa TZS 500,000, kamanda Godbless Lema akiongea na wageni waalikwa alisemaawali alijua familia ya Bashe ni CCM ndiyo maana alienda kuweka kambi pale UDOMkuhakikisha Abubakari Bashe mdogowake na Hussein Bashe anashindwa lakini baada ya uchaguzi na chadema ikiibukakinara, Abubakari Bashe alimfata na kumlaumu kwanini amemfanyia hivyowakati yeye ni chadema na familia yao nichadema.

Baada ya habari hizi nilianza kupitia matamko Hussein Bashenikagundua alishaanza kitambo kupasha bado maamzi mazito kuya chukua au pepeo CCM bado amemwingia ndiyo maanabado mguu ndani mguu nje…

Pata moja ya habari aliyoitoa 09/2012

=======================================================

MJUMBE wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama ChaMapinduzi (UVCCM), Hussein Bashe, ameonya kuwa iwapo CCM hakitajadili matatizoya wananchi sasa, kitarajie kupoteza dola mwaka 2015, kama ilivyotokea kwachama tawala Zambia.

Akizungumza katika Kata ya Kasamwa wilayani Geita katikamaadhimisho ya miaka 33 ya kuanzishwa kwa UVCCM, Bashe alisema kuwa uchaguzi waZambia umemalizika na chama kilichoongoza kwa zaidi ya miaka 20 kimeondolewamadarakani, tukio linalopaswa kuwa funzo kwa CCM.

Alisema katika mazingira ya sasa ambayo wapiga kura wengi nivijana, CCM kinapaswa kuwasikiliza, kujadili matatizo yao na kuyapatiaufumbuzi, vinginevyo kitang'oka madarakani muda mfupi ujao.

"CCM kianze kujiandaa leo kwa kutoa majibu ya matatizo yavijana kinaowaongoza ikiwa ni pamoja na viongozi wake kuepuka kukaa ofisini naumangimeza kwani bila hivyo, mwaka 2015 wataanza kutafuta mchawi," alisemaBashe na kuendelea:

"Kiache kutafuta mchawi mmoja mmoja, kiache kujadili watukijadili matatizo ya watu tujadili watu wanapata wapi maji, watu wanapata wapiajira, wanapata wapi zahanati na fedha zinazotengwa katika halmashauri yawilaya kwenda kwa wananchi zinawafikia… haya ndiyo mambo ya msingi kabisa kamayakifanyiwa kazi CCM kitaendelea kushika dola."

Alisema wakati UVCCM leo ukisherehekea miaka 33 tangukuanzishwa kwake, viongozi wanatakiwa kujiuliza ni kwa nini watu wengihawajaichagua CCM na ni vipi vijana wengi ndiyo wanaoonekana hawataki kuiungamkono CCM. Alisema hii ndiyo changamoto kubwa inayokikabili chama hicho tawalakwa sasa.

Bashe alisema vijana wa Tanzania leo watapenda CCM kama tukitawahakikisha elimu bora, afya bora, fursa ya kufanya kazi na kujiajiri nauchumi ulio imara.

"Taifa linakwenda kwenye uchaguzi mwaka 2015, kipindi hichokitakuwa na wapiga kura wapya zaidi ya milioni sita ambao wengi watakuwa niwale wenye umri wa miaka 30. Vijana hawajui habari za uhuru na amani wala nini,wanataka kusikia wamepata zahanati, elimu bora na wamepata fursa za kufanyakazi basi, hapo ndipo chama kitakuwa kimejibu matatizo yao."

Alisema CCM ya leo siyo ile ya miaka 10 iliyopita na kwambandani yake kumejaa migawanyiko mingi aliyoieleza kuwa haina maslahi kwa watuwanaowaongoza huku, akisema kumejaa mizengwe mingi na matokeo yake watu wamekuwawakikimbilia upinzani.

"Lazima tujiulize maswali kulikoni hali hii? Lakini majibutunayo ni kwa sababu UVCCM imeshindwa kufikia mahitaji ya vijana wengi na sasawanakichukia chama hiki."

Alisema vijana wengi wamezaliwa na kukua na kuukuta uhuruambao leo, unasherehekewa na taifa kutimiza miaka 50. Wakati huo vijana wa CCMnao wakisherehekea miaka 33 ya kuzaliwa umoja wao, uhuru huo umetokana jitihadabinafsi za wazee na vijana wa wakati ule, vijana wa sasa hawana habari nauhuru.

"Nimeambiwa CCM tulishindwa uchaguzi katika Kata ya Kasamwatuliyopo ambayo tunaadhimisha miaka 33 ya umoja wetu. Kata ipo chini ya Chademana nimeambiwa hapa kumewahi kutokea vurugu. Labda niseme jambo moja kuwaambiaKasamwa uamuzi mlioyafanya wa kuchagua kutoka Chadema ni wenu na ndiyodemokrasia. Mmempa udiwani mbaye hatokani na CCM, lakini niwaombe tofauti zakisiasa zisiwagawe kufikia hatua ya kushambuliana."

"Nilipata taarifa kwamba mlifikia hatua ya kuchomeana nyumbahapa Kasamwa. Niwaombe vijana wenzangu haya maslahi ya kisiasa yasitugawevijana wenzangu, tutofautiane kwa sera na itikadi, lakini tusivurugane,haisaidii mtu yeyote ikitokea vurugu hapa na vijana ndiyo watakuwa wa kwanzakuathirika."

Alisema viongozi wa UVCCM wanapaswa kuepuka ‘Ndiyo mzee'bali kuhakikisha wanazibana halmashauri za wilaya zifanye kazi ambayo itasaidiakuleta maendeleo kwa wananchi na vijana kwa ujumla na alionya kuwa CCMkinapaswa kuhakikisha kuwa maeneo yaliyochukuliwa na upinzani hayaachwi kwakuhakikisha kinafikisha maendeleo.
 
ni vyema kupata waungaji mkono kutoka ccm katika kuelekea kutwaa dola mwaka 2015.lakini ni makosa makubwa kama tukiwaza kuwa huo ndio msingi haswa wa kutwaa dola.cha msingi hapa ni kuwaeleza wanachi na waelewe kwanini tunataka kubadili dola 2015.tukibakia kupokea majina na kuyashangilia huku watu wetu hawajui kwanini mabadiliko ni laima tutakwama.
 
Hakuna shida ila zisiwe ni zile hela zao za wizi na dhuluma , kwanza wameisharekebisha lile swala lao la uraia ?
 
Mkuu wanachama wa CCM wananafasi kubwa sana kutuwezesha kuingia ikulu hawa ndiyo wapiga kura wetu kwa hiyo tunapo wapata na ukijumlisha na wale ambao hawana chama kitaeleweka tu....
 
Hakuna shida ila zisiwe ni zile hela zao za wizi na dhuluma , kwanza wameisharekebisha lile swala lao la uraia ?
Mkuu CCM hata leo wewe ukigombea ubalozi wa nyumba 10 watakuambia wewe siyo raia lakini uchukuaji wa form ukisha pita hutojua hiyo kesi imeishia wapi?
 
Kumbe Lema alishiriki ktk siasa chafu Udom.
 
Kesho Hussein Bashe, atatoa press release yake, kwenye gazeti la Mtanzania, kukanusha kuhusika na huo mchango wa 500,000 toka familia ya Bashe kwenda Chadema!. Atakacho fanya ni kuji disassociate na huo mchango hata kama at the end of the day, hizo fedha zote katoa yeye!. That is politics!.

Angalau Sabodo ndiye kada wa CCM pekee aliye bold enough kutoa fedha Chadema publically!. yule Tajiri mwingine ambaye yuko CCM nae pia ni mfadhili mzuri tuu wa Chadema on low profile!. That is politics!.

Chadema wakijipanga vizuri kuonyesha seriousness kuingia Ikulu 2015, wafanya biashara wengi tuu haswa wahindi watatuma michango yako mapema ili kujiposition vizuri kabla, maana you never know with politics!.
P.
 
  • Thanks
Reactions: ral

Kama wanapesa safi zitapokelewa lakini kama zina wa lakini baadae zitatuletea matatizo kama ya CCMabwepande hasa ukipata kiongozi asie na msimomo kama tulie nae angalau Mkapa alikuwa anaweza kuweka wa mee hatakama anakujua..
 
Nimekusoma mkuu lakini ilikuwa inarushwa moja kwamoja na vyombo vya habari kilichokuwa kikiendelea kwa hiyo hata nisiposema mimi kesho au mwakani utaiona kwenye magazeti hata hivyo CCM siyo watu wa kuongopwa pale ni bogus tupu yaani unaweza kuwapa mtihani na majibu lakini bado watachemka na wanapaswa wajue mwakani ni kazi kazikuna makamanda zaidi ya 20 wako tayari vyombo viko tayari bado Canter tu, harafu waendelee na propaganda za kijinga mwaka 2014 - 2015 watashangaa tuko magogoni kudadadeki zao...
Askari wa na hasa kikosi cha INtelijensia huwa hakitangazwi kuwa tayari kimefikia hapa......ama kina taarifa hii na mhusika mkuu kwa sasa amefikia kwenye eneo hili nk, naamini umenielewa .
 
.....pesa za vifaa vya matangazo kuweza kununua gari aina Canter itakayotumika kubebea vifaa hivyo pamoja na majiko pale kazi rasmi ya ukombozi itakapo anza mapema kabisa mwakani itakayokuwa kijiji kwa kijiji.

Hapa mambo yamekaa vizuri barikiweni sana wakuu!
 
Kama wanapesa safi zitapokelewa lakini kama zina wa lakini baadae zitatuletea matatizo kama ya CCMabwepande hasa ukipata kiongozi asie na msimomo kama tulie nae angalau Mkapa alikuwa anaweza kuweka wa mee hatakama anakujua..
Siku zote wachangiaji wakubwa wa CCM ni wahindi na pesa zao safi kama theluji!, kama fedha za Kagoda zilikuwa safi, hizi za hawa wafanya biashara ni safi kabisa. Mpaka kesho, wahindi ndio most generous kuchangia CCM ukiondoa tule tumichango twa wale waarabu na tule tujisuti, michango tegemewa ni ya wafanyabiasha hawa wenzetu!.
P
 
.....pesa za vifaa vya matangazo kuweza kununua gari aina Canter itakayotumika kubebea vifaa hivyo pamoja na majiko pale kazi rasmi ya ukombozi itakapo anza mapema kabisa mwakani itakayokuwa kijiji kwa kijiji.

Hapa mambo yamekaa vizuri barikiweni sana wakuu!
Pamoja mkuu, vita hii siyo ya viongozi tu shiriki hata kwa dua....
 
Siku zote wachangiaji wakubwa wa CCM ni wahindi na pesa zao safi kama theluji!, kama fedha za Kagoda zilikuwa safi, hizi za hawa wafanya biashara ni safi kabisa. Mpaka kesho, wahindi ndio most generous kuchangia CCM ukiondoa tule tumichango twa wale waarabu na tule tujisuti, michango tegemewa ni ya wafanyabiasha hawa wenzetu!.
P

Leo jumapili PAsco unakunywa nini hapo ulipo?
 
Askari wa na hasa kikosi cha INtelijensia huwa hakitangazwi kuwa tayari kimefikia hapa......ama kina taarifa hii na mhusika mkuu kwa sasa amefikia kwenye eneo hili nk, naamini umenielewa .

Ni jambo jema sana kuwahabarisha watanzania ili wajue tunaelekea wapi.
Ukombozi unaotafutwa na watanzania si wa kificho....................... mambo yote unaweka hadharani watu wapime wenyewe....................... isitoshe function nzima ilihudhuriwa na waandishi wengi kutoka vyombo mbali mbali vya habari isipokuwa tbc
 
Siku zote wachangiaji wakubwa wa CCM ni wahindi na pesa zao safi kama theluji!, kama fedha za Kagoda zilikuwa safi, hizi za hawa wafanya biashara ni safi kabisa. Mpaka kesho, wahindi ndio most generous kuchangia CCM ukiondoa tule tumichango twa wale waarabu na tule tujisuti, michango tegemewa ni ya wafanyabiasha hawa wenzetu!.
P
Yaani kweli kwasasa wanajiunga kwenye chama kwa wingi ingawa bado waoga kujiweka huru, hapo kwenye nyekundu nimecheka sana mzee mzima alilambisshwa suti watu wakachuku walichokitaka...kweli lazima tuingie kwenye kumbukumbu kama watanzania tuko salama...
 
Back
Top Bottom