Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,566
TAARIFA KWA UMMA
Katika utekelezaji wa agizo hilo, ni kumbi 149 tu ndizo zimetekeleza. Hivyo basi, Baraza kupitia masharti ya usajili ya Kanuni ya 59 linasitisha rasmi shughuli za Sanaa, sherehe na burudani katika kumbi 504 Tanzania Bara (Orodha ya kumbi 504 imeambatishwa) kuanzia tarehe 28 Machi, 2024 mpaka watakapolipia vibali kupitia kiungo AMIS. Baraza litashirikiana na mamlaka nyingine za Serikali wakiwemo Maafisa Utamaduni kote nchini ambao kimsingi ni Wasajili Wasaidizi kufuatilia watakaondelea kukiuka Sheria na Kanuni za BASATA.
Ofisi za BASATA zitakuwa wazi kwa siku ya Jumamosi na Sikukuu kuanzia saa tatu kamili asubuhi hadi saa sita mchana kwa ajili ya kutoa huduma.
Aidha, Baraza linawakumbusha wamiliki wa kumbi ambao hawajasajiliwa/hawanavibali HAI vya kuendesha shughuli za Sanaa, starehe na burudani wajisajili mara moja ili kuepuka usumbufu. Umuhimu wa kuwa na KIBALI cha BASATA ni pamoja na kuzitambua na kuzisimamia kumbi ili zitimize matakwa ya Kisheria ikiwemo kuzingatia usalama wa watu. Kwa msaada piga simu 0759942512.
KUSITISHA SHUGHULI ZA SANAA, SHEREHE NA BURUDANI KATIΚΑ KUMBI 504 ΤΑΝΖΑΝΙΑ BARA.
Mnamo tarehe 19 Februari, 2024 Baraza lilitoa tamko la nia ya kusitisha huduma kwa kumbi 653 ndani ya siku 14 kwa wadau wote ambao hawatatimiza vigezo vya kuhuisha vibali vya kufanya shughuli za Sanaa, Sherehe na Burudani nchini.Katika utekelezaji wa agizo hilo, ni kumbi 149 tu ndizo zimetekeleza. Hivyo basi, Baraza kupitia masharti ya usajili ya Kanuni ya 59 linasitisha rasmi shughuli za Sanaa, sherehe na burudani katika kumbi 504 Tanzania Bara (Orodha ya kumbi 504 imeambatishwa) kuanzia tarehe 28 Machi, 2024 mpaka watakapolipia vibali kupitia kiungo AMIS. Baraza litashirikiana na mamlaka nyingine za Serikali wakiwemo Maafisa Utamaduni kote nchini ambao kimsingi ni Wasajili Wasaidizi kufuatilia watakaondelea kukiuka Sheria na Kanuni za BASATA.