BASATA: Diamond amekosea kumjibu Naibu Waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo, Julianza Shonza

Hadi tusahau 26042018 daadeki, tukienda hollywood na hizi script zetu lazima tutoboe!
 
Kuitukana serikali ndio kusemaje?
Nchi hii inataka watu wawe waoga kujieleza .....

Fyonza amesthili
 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Godfrey Mngereza amesema mwanamuziki Nassib Abdul maarufu Diamond amefanya makosa kumjibu Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza akifananisha kitendo hicho na kuitukana Serikali.


Diamond Platnumz na naibu waziri huyo waliingia katika vita ya maneno baada ya Serikali kufungia nyimbo 15 mwezi uliopita, zikiwemo mbili za mwanamuziki huyo.



Akizungumza na MCL Digital leo Jumatano Machi 21, 2018, Mngereza amesema Diamond anapaswa kuelewa kwamba maneno machafu anayoyatoa dhidi ya waziri huyo ni sawa na kuitusi serikali jambo ambalo hata ukienda katika sheria za kimtandao anaweza kujikuta anaingia matatizoni.



Diamond, naibu waziri ni vuta nikuvute
Mngereza amesema wamesikitishwa na kauli ya Diamond na kusisitiza kwamba ni vyema akafuata taratibu katika kulalamikia suala hilo ikiwemo kuandika barua kama alivyomuelekeza Waziri Shonza.



Ameongeza kuwa si lazima msanii aandikiwe barua pale anapokosa kama ambavyo Diamond ameeleza katika ukurasa wake wa Twitter, kwamba Shonza angemwandikia barua kabla ya kumfungia.
Amebainisha kuwa si kila mwanamuziki anayefanya makosa huwa anaandikiwa barua.



Katika malalamiko yake, Diamond amesema naibu waziri huyo amekuwa akikurupuka kufungia nyimbo na pia kutowaandikia barua rasmi ndio maana ameamua kuyazungumza kwenye redio na mitandao ya kijamii.



Jana Waziri Shonza alisema hawezi kujibizana na Diamond kwa sababu alichofanya si maamuzi yake binafsi na kwamba kama anaona ameonewa apeleke malalamiko yake kwa maandishi.
 
Hata kama Diamondi ameonewa lakini kitendo cha kujibizana na Naibu Waziri kiudaku namna ile ni utomvu wa nidhamu kabisa.

Hata kama Mungu mtu ndio mlezi wake, angetumia busara kumjibu.
 
Huyu katibu wa BASATA sijui msomi wa wapi. Serikali inafanya Kazi kwa matamko siku izi bila maandishi nilikuwa sijui
 
BASATA wanafikiri bila kodi za akina Nasibu na wenzake watakula wapi?
Serikali haina shamba la fedha!!!!
BASATA wasimamie taratibu friendly waache ushenzi wa TRA kuwa "hapa ni kazi tu"!
 
matatizo ya kulewa sifa ndo hayo mondi shuka kuwa na wafuasi wengi si kigezo cha kuwa juu ya sheria.
 
Hata kama Diamondi ameonewa lakini kitendo cha kujibizana na Naibu Waziri kiudaku namna ile ni utomvu wa nidhamu kabisa.

Hata kama Mungu mtu ndio mlezi wake, angetumia busara kumjibu.
Wao mbona awatumii kauli za kiungwana kwa wasanii au mwananchi kiujumla ifikie kipindi lazima tukubariane hii nchi yetu sote wote tuna haki sawa wasilete hbr za kikaburu hapa...
 
Serikali hii inaongozwa hovyo sana.

Shonza mwenyewe alidai kwamba serikali haifanyi kazi na mambo ya mtandao

Hawa basi tu bora siku zisonge maisha yaendelee.

Imefika wakati haijulikani ni kipi nchi inataka ili iendelee kila mwenye mamlaka yake akiamka ni maneno tu
 
Back
Top Bottom