BASATA: Diamond amekosea kumjibu Naibu Waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo, Julianza Shonza

Si lazima kumuandikia barua msanii? Huu ni utendajikazi mpya wa serekali. Hiyo mahakama yenyewe tu inaandika samaz itakua basata!!?
 
Katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania Godfrey Mngereza amefunguka na kusema kuwa anachofanya diamond cha kujibishana na naibu waziri wa habari sio kizuri na kukifananisha kitendo hicho na kitendo cha kuitukana serikali .Diamond na naibuwaziri waliingia katika mgogoro wa kurushiana maneno baada y naibu waziri kufunga nyimbo zaidi ya 15 huku nyimbo mbili zikiwa ni nyimbo za msanii Diamond.

Mngereza anasema kuwa jambo analofanya Diamond kwa sasa ni sawa na kuitusi serikali jambo ambalo kama atashitakiwa na serikali pia ni kosa la kimtandao.ameongezea na kusema kuwa sio lazima mtu anapofanya kosa lazima aandikiwe barua kama yeye anavyodai.

Mngerza anasema kuwa amesikitshwa sana na maneno ya diamond , kwa sababu kama angekuwa na maalalmiko angepaswa kuandika barua ili kutoa malalamiko yake na sio kwenda katika mitandao ya kijamii.

Katika kumjibu diamond, mh juliana shonza alisema kuwa hana mamlaka ya kumjibu diamond tena kwa sababu maamuzi anayoyafanya sio yake ila ni kazi ya serikali na kama ana malalamiko aandike barua, ndipo diamond alipoamua kumjibu kuwa kama yeye alianza kuyapeleka radion na kwenye mitandao na yeye hatokaa aandike barua.
 
Mimi nacheki tuu hadi mwisho, hili li muvi linapoenda, ukiwa na pesa/madaraka ni lazima ujione mungu mtu.
 
Hapo Diamond ni geresha tu, vita halisi ni Clouds Media,Mwakyembe,Shonza,Mngereza dhidi ya 'Mungu wa Dar'. Lakini tukumbuke huyu Mungu wa Dar anababa yake asiyeshindwa kamwe
 
Wenzenu wanawatengenezea muvi kuwatoa kwenye maandamano

Tumieni akili ninyi mampunga
Sikutaka kugusia hiyo ndio maana nimeishia nilipo ishia mkuu, muda ndio hakimu. Uwezekano wa hilo ni mdogo saaana.

Ungeniambia zile ajira 10000 za bomba ningekuelewa
 
Back
Top Bottom