Waziri Dkt. Ndumbaro Azitaka Taasisi Kuongeza Wadau wa Ushirikiano

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

WAZIRI DKT. NDUMBARO AZITAKA TAASISI KUONGEZA WADAU WA USHIRIKIANO

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameziagiza Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kuongeza wadau wa ushirikiano nje ya Serikali ili kutimiza mahitaji ya wananchi katika Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Mhe. Dkt. Ndumbaro ametoa maagizo hayo Septemba 7, 2023 jijini Dodoma wakati wa kikao chake na Wakuu wa Taasisi za Wizara kilicholenga kufahamiana na kujua majukumu ya Taasisi tisa kilichohudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Hamis Mwinjuma.

"Watanzania wanataka mabadiliko kwenye Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo, ni lazima mfahamu Ilani imeelekeza nini kwenye maeneo yenu pamoja na kutafuta wadau wa ushirikiano nje ya Serikali. Na kwa Taasisi ambazo wadau wenu wanafanana lazima mshirikiane". Amesisitiza Mhe. Dkt. Ndumbaro.

Awali akizungumza katika Kikao hicho, Naibu Waziri Mhe. Hamis Mwinjuma amesema Taasisi za Wizara hiyo zina mchango mkubwa katika kutoa furaha kwa Watanzania na kwa sasa Watanzania wanazielewa, hivyo zinahitajika kuongeza ubunifu na kuwa karibu na Wadau wake

Taasisi hizo ambazo zimewasilisha taarifa kuhusu majukumu yao kwa Mhe. Waziri ni Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bodi ya Filamu Tanzania, Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA), Kituo cha Ukombozi wa Bara la Afrika, Mfuko wa Utamaduni na Sanaa pamoja na Chuo cha Michezo Malya.

F5b6w7uXwAEkEPO.jpg

F5b6yADXwAQrrgS.jpg

F5b6yaQXwAES-Bx.jpg
 

Attachments

  • F5b6w7uXwAEkEPO.jpg
    F5b6w7uXwAEkEPO.jpg
    99.4 KB · Views: 1
Back
Top Bottom