Barua: Zitto akataa posho za vikao

Kweli kabisa!! Na hicho ndichi Zitto alichofanya. Halafu hpa ndani mijitu inampongeza tu bila hata kuthink big

Ukweli zitto kathubutu kuna tofauti ya zitto kupokea pesa zake na zitto kusema pesa hizo mpe muhasibu wa NGO yangu . Zikishaingia KDI ni pesa ni ya NGO. Na NGO zinakuwa audited na zinakuwa accountable.

Sina uhakika kama kweli NGO hiyo ni yake lakini hata kama myonge myongeni haki yake mpeni

Kimbunga shirikisha ubongo unapoandika. KDI ni kigoma Devp Initiative na sio Zito Devp Initiative. Zito yeye ni founder member tu wa hiyo NGO kwa hiyo anakuwa ni Board members na sio mtendaji mkuu. Siku zote wanayefaidi katika NGO ni watendaji na walengwa na sio Board members na hata kama hiyo NGO ni ya Zito Kama vission na mission zake ni kuleta maendeleo kwa watu wa kigoma kwa vitendo na yakatelezeka we hv no querry abt him. Congrat Zito

Mwanaharakat unazijua vizuri NGO za nchi hii? Unajua NGO za nchi hii zinavyoendeshwa? Unajua utitiri wa NGO viwavi hapa nchini? Nimeshirikisha ubongo wangu.
 
very good. Hatutaki maneno maneno tu.
Kiongozi huonyesha njia na Zitto umeonyesha na kuifuata.
big-up
 
Tall order for CDM MPs to follow suit! Hongera Mkuu, ila naona umewatega wenzako wakina Mbowe.....watakuwa wanakulaani chinichini!
Umepiga bao la kisigino! Tuone wafuasi wao watasema nini leo!
hamna cha wafuasi wa nani na nani (hapa pana wafuasi wa hoja na si mtu) hapa ni kwamba Zitto anastahili pongezi.Binafsi namtiliaga sana Zitto ila kwa hili kanikosha
 
Jamani Wabunge wengine wa CHADEMA vipi? Jitokezeni basi mziteme hizo posho? Mbona mnamtupa mkono Zitto?
 
Hapa nakumbuka msimamo wa Chama wa kutoka nje wakati JK anahutubia Bunge, ZZK akaja na msimamo wake wa kupingana na Chama. Acha kuturudisha nyuma Zito ni binadamu kama wengine aliona mapungufu na sasa ameamua kurudi kwenye dhamira yake ya kweli na chama pia ya kumpigania mtz mnyonge na ndio kama umesoma vizuri amesema huo ni uamuzi wake binafsi na chama pia.kuna tofauti kubwa sana kati ya magamba na Cdm.
 
Sioni mantiki yoyote kwa hili. Posho ni haki yake. Jimbo kwake kuna matatizo kibao ya huduma za wananchi. Angeweza kutangaza kuwa anaelekeza posho hizo kwenye huduma za jamii jimboni kwake. Hivi kumgekuwa na ubaya gani kama angeeleza posho hizo hospitali ya jimbo lake? Asilewe sifa ingawa ana ubora.

Usi-comment kabla hujaelewa, soma vizuri uelewe ndo utoe maoni yako... Shame on you!?
 
Hapa nakumbuka msimamo wa Chama wa kutoka nje wakati JK anahutubia Bunge, ZZK akaja na msimamo wake wa kupingana na Chama. Acha kuturudisha nyuma Zito ni binadamu kama wengine aliona mapungufu na sasa ameamua kurudi kwenye dhamira yake ya kweli na chama pia ya kumpigania mtz mnyonge na ndio kama umesoma vizuri amesema huo ni uamuzi wake binafsi na chama pia.kuna tofauti kubwa sana kati ya magamba na Cdm.
CDM na magamba vimetoka wapi tena hapa wakati tunajadili hoja ya kukataa posho. Hapa ndipo huwa watu humu ndani mnapotoka. Badala ya kujadili hoja unakimbilia kulinganisha vyama. Jadili hoja Mwanaharakat. Msimamo wa Chama uko wapi? Mapendekezo ya Budget ya CHADEMA ni kuondoa posho.

Au yalikuwa ni mapendekezo ya Zitto manake ndio yeye ameanza kuyatekeleza.?
 
Kimbunga shirikisha ubongo unapoandika. KDI ni kigoma Devp Initiative na sio Zito Devp Initiative. Zito yeye ni founder member tu wa hiyo NGO kwa hiyo anakuwa ni Board members na sio mtendaji mkuu. Siku zote wanayefaidi katika NGO ni watendaji na walengwa na sio Board members na hata kama hiyo NGO ni ya Zito Kama vission na mission zake ni kuleta maendeleo kwa watu wa kigoma kwa vitendo na yakatelezeka we hv no querry abt him. Congrat Zito
Mwanaharakati Mwanamapinduzi;
Big -up kwa saaana!. Your reasoning is very correct as well as rational. Endelea kuturekebisha kimawazo. Yaani mtu anafikiria Zitto akishiriki kuanzisha NGO ndiyo imekuwa ya nyumbani kwake?
 
Vi NGO uchwara vya nchi hii ni wizi mtupu!! Sheria zipo lakini Muanzishaji wa NGO ndiye huwa mmiliki na mwenye maamuzi ya mwisho. Huenda hiyo KDI ikawa ya Zitto na ndugu zake kama ambavyo kampuni inaweza kuwa ya mke na mume!
 
Zito ameshakuwa na uhusiano wa karibu sana na akina rostam aziz pewsa ya kula anayo na hizi na ccm campaign ndani ya zitto, pesa hizo angechukua ila angeongea na wananchi wake jimboini kwake waseme kuwa hizo pesa zifanye nini, kuchukua achukue. Kuacha mshahara wako au posho unazostahili ni ujinga tu wala haisaidii...... kwa sababu kama kweli wewe ni mbunge fanya kazi unachopata ni unachostahili kutokana na sheria
 
Mwanaharakat unazijua vizuri NGO za nchi hii? Unajua NGO za nchi hii zinavyoendeshwa? Unajua utitiri wa NGO viwavi hapa nchini? Nimeshirikisha ubongo wangu.
Kimbunga ni vyema ukafahamu kuna aina mbili za nyuki wapo wanaouma na wasiouma ijapokuwa wote wanatoa asali. mpango wa kuanzisha NGO na DF ni dhamira ya kweli ya wabunge wa CDM ili kuleta maendeleo katika majimbo yao na sio KDI tu ipo pia ArDF ya Arusha ambayo mpaka sasa inasomesha wanafunzi 400 wasiojiweza.
 
Tatizo la Magamba wao hupenda kujifananisha na CDM that why hata katika mjadala huu waposho nao wsmejipenyeza. CCM wameisha kataa kutokatwa kwa posho zao so sidhan kama kuna haja ya sisi kuwajumuisha ktk mjadala huu, they are conservative and i'm so glad that majority of tanzanians are aware of their behaviour. Mpaka 2015 ifike watakoma!
 
Mwanaharakat unazijua vizuri NGO za nchi hii? Unajua NGO za nchi hii zinavyoendeshwa? Unajua utitiri wa NGO viwavi hapa nchini? Nimeshirikisha ubongo wangu.
Kimbunga Tufani;
This NGO must be different. Kumbuka inakuwa injected funds amabazo ilikuwa ni posho ya Mbunge ambaye kaona kwa uzalendo wake hawezi kula pesa ya serikali visivyo halali. Akaamua kuichukua na kuwarudishia serikali kwa njia mbadala, akawapelekea wananchi wa-Tanzania maskini. Aisee hakuna mkono mrefu wa mtu unaoweza kugusa mbesa ile aisee. ZZK ataua mtu. Hivi umnamjua aisee?
 
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ameiandikia barua Ofisi ya Bunge kuiomba isimamishe kumlipa posho zake zinazotokana na vikao vya Bunge kuanzia juzi. Zitto ametoa ombi hilo kwa barua rasmi aliyoiwakilisha kwa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah Juni 7 mwaka huu.

Kweli kamanda Zitto UNATISHA!... Kwanza uliweka kama mapendekezo ya budget ya upinzani, halafu ile wenzio wanasuasua we umefanya kweli,...
Ungekuja kugombea ubunge jimboni kwangu, kura yangu ungeiweka mkononi kwa mwendo huu!
 
Kimbunga ni vyema ukafahamu kuna aina mbili za nyuki wapo wanaouma na wasiouma ijapokuwa wote wanatoa asali. mpango wa kuanzisha NGO na DF ni dhamira ya kweli ya wabunge wa CDM ili kuleta maendeleo katika majimbo yao na sio KDI tu ipo pia ArDF ya Arusha ambayo mpaka sasa inasomesha wanafunzi 400 wasiojiweza.

Huenda ArDF ni nyuki asiyeuma na KDI ni nyuki anayeuma!!! Nitajuaje kama sijui uongozi wa KDI na sijasikia ikisomesha wanafunzi 400 kama unavyoniambia hapa kuhusu ArDF?
 
Tatizo la Magamba wao hupenda kujifananisha na CDM that why hata katika mjadala huu waposho nao wsmejipenyeza. CCM wameisha kataa kutokatwa kwa posho zao so sidhan kama kuna haja ya sisi kuwajumuisha ktk mjadala huu, they are conservative and i'm so glad that majority of tanzanians are aware of their behaviour. Mpaka 2015 ifike watakoma, SIO WABUNIFU NA WANAIGA MAMBO SANA!
 
Kuna kazi sana kwa Watanzania kubadirika, na ndio maana Dowans , symbion, michezo michafu bado tu inaendelea wanachofanya ni kutwist akili za watu kidogo sana. Mimi ya Zitto siyaamini kwa kuwa najua system zilivyo na yeye Zitto yukoje kwa sasa, hapa kila mtu anapiga campaign kwa style ambayo yeye anadhani ata win kuwa rais mbeleni. I know kuwa hawa politicians wameajiri consultants ambao day to day anakuwa amempa series ya activities ili aweze kuwin mass na kupata uongozi.

Poleni zetu including me.
 
BINAFSI NATOA PONGEZI ZANGU STAHILI.......(ANGALIZO) KAMA ALIPOELEKEZA ZIPELEKWE KWELI IKAWA NI NGO YAKE BINAFSI (hiyo ni sarkasi katuchezea) SI SAHIHI SANA.....! BALI NINGEMWELEWA ANGEPELEKA KATIKA TAASISI AMBAZO HANA MKONO WAKE KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE!
TUHESHIMU MCHANGO WAKE NA PIA LOLOTE AMBALO AENDA KINYUME TUWE KINYUME NALO

Mkuu mahesabu ungetoka kidogo tu nje ya box ungegundua kuna kina Bill & Belinda Gates Foundation wanaopata ruzuku toka Microsoft ya Bill Gates. Hivi unatambua kuwa Mandela alipeleka mkwanja aliopata as co-winner Nobel Prize kwenye NGO yake??

Kumbuka kuna separation kati ya owners na kampuni/NGO aliyoanzisha. Hivi kabla hajasema kuwa posho zake ziende KDI mbona hatukuhoji integrity the NGO hiyo?? Kuwa na NGO uchwara Tanzania haimaanishi kuwa NGO zote ni mchumia tumbo.

Zitto apongezwe kwa hili na wala tusiwe wataalam wakutoa maangalizo.
What have we done to our communities anyway before telling others what ought to be done?
 
Back
Top Bottom