Barua: Zitto akataa posho za vikao

Zitto aache janja yake! Anatupiga tu wananchi changa la macho. Hii Kigoma Development Initiative(KDI) ni NGO yake mwenyewe! So hizo allowance zinamrudia yeye mwenyewe!
Sio janja bali pesa inaelekezwa kunakohitajika zaidi...ameonyesha njia ...tena kwa vitendo...big up sana !! Kila mbunge angeielekeza posho yake kwenye maeneo ya msingi ya jimboni kwake life would be a bit easier
 
Mh. Zitto kabwe (MB-Kigoma Kaskazini), kwa kutambua Makali ya bajeti Amemwandikia Barua katibu mkuu kumtaka asitishe malipo ya posho yake yatokanayo na vikao vya bunge. Kwa step aliyoipiga Zitto nadhani Kuna haja ya WABUNGE WOTE WA CDM kumuunga mkono nao kuacha posho zao ili kudhihirisha dhamila ya chadema kuleta maendeleo kwa watanzania. Hongera mh. Zitto Kabwe!
 
Zitto aache janja yake! Anatupiga tu wananchi changa la macho. Hii Kigoma Development Initiative(KDI) ni NGO yake mwenyewe! So hizo allowance zinamrudia yeye mwenyewe!

Mkuu nami nilikuwa nataka kujua hiyo KDI ni ya nani. Sasa kama ni ya Zito basi hapa anatudanganya ni kwamba anajipigia tu pasi ya hizo posho kutoka bungeni na kwenda kuzinyakulia KDI.

Pili, kama huo ndio msimamo wa CHADEMA mbona ni Zito peke yake anaandika barua kwa nini chama kisiandike barua? Maumivu ya kichwa huanza taraatibu, na mwazo wa goma ni lele pia mwanzo wa vurugu ni kuhitililafiana. Hapa kuna kitu; kwa nini Zitto peke yake na kwa nini si Chama? Tutafakari
 
Siku Lema akijotoa kupokea posho za Bunge ndio utasifia

usipende kurukia thread katikati na hoja bila kutafakari nakufuatilia tangu mwanzo wa thread .... rudia kusoma post iliyotolewa na jibu fupi nililotoa ...

angalia hii post no. 7 katika hii thread

Mw. JK Nyerere is listening to us

moral practice indeed .... well done zitto

wewe lazima ni mcharuko
 
Mhh! Kweli?
Lkn mie nadhan pamoja na kuwa kweli posho hizo ni kubwa, kwa cdm bado zinahitajika sana kwani chama bado hakina vyanzo vya kutosha vya mapato vya kutosha. Hivyo basi posho hizo pamoja na ruzuku kidogo inayopatikana itakisaidia chama kujiimarisha zaidi.
Sa wakizikataa wataanza tena kuwaomba kina Sobodo!
 
Then Amesema Budget ya sasa imejaa upotoshaji wa takwimu sana! Nadhani ktk kuchangia budget itakuwa poa, ful madata! Huyu ndio Zitto Kabwe TULIEMISS! "the Come back of Zitto Kabwe" wooow!
 
Big Up zitto Kabwe huoni mfano wa kuigwa

Lakini kwa kuongeza unge quantify matumizi ya hiyo posho Huko KDI o yafanye nini hasa. Pesa yako isije ikaishia kaishia kwenye administration. eg

  • Pesa ya bunge hili kununu vitabu kadhaa vya hesabu vya darasa la tatu na las ita kwa shule za msingi tatu zilizochaguliwa kigoma.
  • Pesa ya ikao cha bunge bunge lingine somesha walimu kumi wa secondary za kigoma 10 short course za kompyuta

BTN

serikali imetoa bajeti yao je wabunge mbona hawatoi bajeti na matumiz yao ya pesa za mfuko wa bunge. Au mfuko huo wa bunge una Kinga. Wanachi tunataka kujua mipango ya wabunge juu ya pesa a mfuko ya jimbo. Tunataka kuona Financial report.

-Ni mbunge gani kawashikisha wananchi juu ya matumizi ya pesa za mfuko wa jimbo
- Ni mbunge gani hata kama hakushirikisha wananchi atoa report za matumuzi za mfuko huo
 
Mkuu hiyo posho haingii ktk mfuko wa chama bt ktk mifuko ya wabunge, chama kina ruzuku yake. Nadhani wabunge wa chadema wafanye km vito japo kwa Bunge hili la Budget!
 
milioni saba za mshahara. mkopo wa mil 90 kwa kila mbunge. ruzuku ya chama kutokana na idadi ya wabunge wake. bado unasema hela hiyo haitoshi? labda haitoshi kweli lakini hiyo posho ya ta.ko ya mbunge inamsaidiaje mpigakura?
 
Kwakuwa chama kina vyanzo vichache vya mapato, nadhani angekuwa ametumia busara kuchukua tu hizo posho na kuzielekeza kufungua matawi na kuendeleza chama...hii inakuwa haina maana chama hakina hela kinaenda kuwaomba kina Sobodo kila siku, then mnakataa kupokea pesa ambazo zinewasaidia kugrow!
Inawezekana kweli anapalilia ndoto zake za kuwa raisin lkn anatakiwa atumie akili zaid...
Angewaza kukiimarisha chama zaidi..
 
Hata kama zinaenda KDI, kwangu hii inabaki kuwa hatua ya maana sana katika kuhakikisha hakuna pesa ya umma inayotafunwa na tumbo moja pekee. umeonesha njia Zitto
 
Mh. Zitto kabwe (MB-Kigoma Kaskazini), kwa kutambua Makali ya bajeti Amemwandikia Barua katibu mkuu kumtaka asitishe malipo ya posho yake yatokanayo na vikao vya bunge. Kwa step aliyoipiga Zitto nadhani Kuna haja ya WABUNGE WOTE WA CDM kumuunga mkono nao kuacha posho zao ili kudhihirisha dhamila ya chadema kuleta maendeleo kwa watanzania. Hongera mh. Zitto Kabwe!

Mbona Zitto tu? Wako wapi makamanda wengine? Mtema, Mnyika, Lissu, Lema, Weche, Shibuda, Kamanda Mkuu Mbowe, n.k jitokezeni basi mzikatae hizo posho. Au inawezekana Zitto amendika barua kwa niaba ya Chama kama Naibu Katibu Mkuu. Kama ni barua binafsi basi Chama kikae kione msimamo wa Chama kama Taasisi isiwe suala la mtu binafsi.
 
Mkuu Kimbunga ningependa km makamanda wote wange muunga mkono zitto, kwa mujibu wa Zitto Kabwe ile Barua ni yake binafsi, ameiandika kuelezea dhamila yake ya kutochukua posho!
 
BTN

serikali imetoa bajeti yao je wabunge mbona hawatoi bajeti na matumiz yao ya pesa za mfuko wa bunge. Au mfuko huo wa bunge una Kinga. Wanachi tunataka kujua mipango ya wabunge juu ya pesa a mfuko ya jimbo. Tunataka kuona Financial report.

-Ni mbunge gani kawashikisha wananchi juu ya matumizi ya pesa za mfuko wa jimbo
- Ni mbunge gani hata kama hakushirikisha wananchi atoa report za matumuzi za mfuko huo

Muulize Mnyika nilimsikiliza pale Mabibo External alitoa uchambuzi mzuri sana (physical evidence) kuhusu ni sh. ngapi zimetumika na kwa ajili gani.
NB: huo mfuko sio hela ya mbunge, mbunge is just mwenyekiti kwa hiyo nakushauri umkomalie mbunge wenu kisawasawa ujue ukweli husika
 
Mkuu nami nilikuwa nataka kujua hiyo KDI ni ya nani. Sasa kama ni ya Zito basi hapa anatudanganya ni kwamba anajipigia tu pasi ya hizo posho kutoka bungeni na kwenda kuzinyakulia KDI.

Pili, kama huo ndio msimamo wa CHADEMA mbona ni Zito peke yake anaandika barua kwa nini chama kisiandike barua? Maumivu ya kichwa huanza taraatibu, na mwazo wa goma ni lele pia mwanzo wa vurugu ni kuhitililafiana. Hapa kuna kitu; kwa nini Zitto peke yake na kwa nini si Chama? Tutafakari
Yaani hata mtu akifanya jambo jema still anatiliwa shaka!!
Mbona Watanzania hatuna jema!!
 
Back
Top Bottom