Barua za Dada..Nafikiri kumtimua

kama ni msikivu mkuu,mpelekeni taratibu. fanyeni kama ambavyo mngemfanyia mdogo wenu. sheria moja muhimu,hana ruhusa ya ku-entertain mgeni yeyote wakati hampo. kama ana umri mkubwa,lay the rules down na mkubaliane.akirudi kijijini huyo ndo watammalizia na ngoma. mnaweza kumsemea kwa wazazi wake,just incase kukiwa na tatizo msilaumiane.ni muhimu akajua lakini kama mtawaambia na wazazi.mkishindwana sio mbaya kukubaliana nae hatua zitakazofuata.ukali hauisaidii sana,ushauri kama ambao ulipatiwa ww hata ukaweza kuwa mtu mzima madhubuti.
 
Du! Usimtimua kwanza, ni stage ya maisha ambayo hata mtoto wako atakuja kupitia/ashapitia. Jaribu kumchukulia kama mwanao, na 'umlee' katika hilo ili litakapokuja kuwa kwa mwanao, uwe na experience.

Umemshauri kwa busara sana...........ILA................wenzetu kusini niwajuavyo mimi...............huyo si kwamba anakua...........................wanaanza mapema sana mahusiano.............................anaweza akawa mjuzi wa mambo kuliko wife wako hapo ................usidharau udogo wake.

Nina rafiki yangu anafanya NGO fualani mambo ya kupambana na ukimwi huko kusini...............................anakwambia...............unakutana na binti ...............miaka 16 tu..........yuko kwenye ndoa ya tatu(3).................

Kama huamini...............mchunguze utakuta anatumia vidonge vya majira.......................ukimwi kwao bado kufunguka akili..................

Mfanyie kanseling ya madhara ya angono zembe na jinsi ya kujilinda ...........usitegemee ataacha ndono...................

Kaa nae chini............mkubaliane.........atimize majukumu yake vizuri kama zamani...................kama unaweza mpe off-day at least kuanzia saa6 siku ya jumapili awe huru kwenda kusalimia ndugu na jamaa.......mpangie na muda wa kurudi nyumbani.

Ukimbana sana .....................ataanza kukutega wewe baba mwenyenyumba..............(yalimtokea ndugu yangu mmoja)

Ukiona haelekei baad ya haya yote......................mrudishe kwao haraka sana.
 
SISI BINADAMU MARANYINGI TUNAPOKUWA MBALI NA TATIZO NI WEPESI SANA KUWAAMBIA WALIO KARIBU NA TATIZO KUWA VUMILIA,
WAKATI HUO HUO KUTOKA NDANI YA MIOYO YETU HATUNA HUO UVUMILIVU TUNAOTAKA WENZETU WAWE NAO......haya bwana ndiyo binadamu tulivyo, mara nyingi hatupendi kusema ukweli.

HUYO msichana kama umepitia hatua zote muhimu za,
kumwelimisha,kumwonya,kumkarilipia kwa wakati,muda na eneo husika bado hakuelewi japo anakusikia,
wala usiendee kumvumilia, mrudishe kwao kwa usalama kabisa. Ipo siku atakumbuka kile ulichokuwa ukimweleza juu ya ubaya
wa hayo mahusiano yake yasiyo na faida kwake na familia yake.

Msichana wa kazi ni msaidizi,mlinzi wa mali na familia yako kwa ujumla,
sasa kama ameanza mapepe hawezi kutimiza wajibu wake ipasavyo,
Anaweza akaleta madhara makubwa kwa watoto wako ( ksb maranyingi watoto ni wepesi kuiga yanayofanywa na watu wanaowazunguka),

Yawezekana wewe (familia yako ) imemtambua kuwa ni mmoja wa familia ,
lakin yeye hajajitambua kama ni mmoja wa familia , pia hajui nini kilichomleta hapa mjini.
KUMBADILISHA MTU TABIA NI KAZI SANA , ILA NI RAHISI SANA PALE ANAPOAMUA YEYE BINAFSI KUBADILIKA.

RAHA YA MTU UNAPOMWONA NA KUMCHULIA KUWA NI MTOTO WAKO,
BASI HATA YEYE AKUCHUKULIE KAMA MZAZI WAKE ,
AKISHAFANYA HIVYO BASI ITAKUWA RAHISI KUKUSIKILIZA NA KUZINGATIA USHAURI PINDI UNAPOMTOLEA/MPA.
 
View attachment 32181View attachment 32182View attachment 32183View attachment 32184View attachment 32185View attachment 32186View attachment 32187View attachment 32188

Haya mambo ya Dada (House Girl) kutoka kusini mwa nchi yetu. Alianza ajira shwari kabisa, baada ya muda mwenendo wake ukabadilika, pengine akienda sokoni kurejea lazima achelewe. Siku chache zilizopita, mamsapu alijaribu kuchukua simu anayoitumia kwa mawasiliano hapa nyumbani tulimnunulia kwa hilo tui, mara simu ikalia, baada ya kupiokea, sauti ya jamaa ikasikika ikikoroma "vipi we mtoto mbona huonekani buchani sasa mimi nimeweka nyama kibao uje ule??...njoo bwana tiufanye kama siku ile leo nitakupa na hela ya mtoko.." Mamsapu akashtuka na kuuliza, vipi ??? Jamaa likakata simu..badaa ya kumuuliiza dada akakataa..lakini baada ya muda akakiri anasumbuliwa na jamaa fulani ..akaahidi kuacha haya mambo. Tukamnyang'anya simu.

Aidha, katika harakati ya kujaribu kumsaidia..tuliendelea kumwonya tu ili azingatie kile ambacho kimemleta mjini asije ishia kwenye matatizo ikiwemo maradhi...lakini inaonerkana kabinti kamezoea..leo naletewa kesi hii,...eti dada anatumia daftari, karamu na rangi za watoto kuandikia barua wanaume...khaaa.

Nafikiri kutimua mtu this evening!! Naona hakuna kitu hapa!!
Mkuu hiyo miandiko mbona inafanana na wa kwako (Joking).

Mkuu, hii kitu ni kumzalilisha House girl wako, nadhani wewe ni mtu mzima na unaweza kabisa kuyamaliza haya mambo uko uko nyumbani. Just fikra zangu tu.
 
SISI BINADAMU MARANYINGI TUNAPOKUWA MBALI NA TATIZO NI WEPESI SANA KUWAAMBIA WALIO KARIBU NA TATIZO KUWA VUMILIA,
WAKATI HUO HUO KUTOKA NDANI YA MIOYO YETU HATUNA HUO UVUMILIVU TUNAOTAKA WENZETU WAWE NAO......haya bwana ndiyo binadamu tulivyo, mara nyingi hatupendi kusema ukweli.

HUYO msichana kama umepitia hatua zote muhimu za,
kumwelimisha,kumwonya,kumkarilipia kwa wakati,muda na eneo husika bado hakuelewi japo anakusikia,
wala usiendee kumvumilia, mrudishe kwao kwa usalama kabisa. Ipo siku atakumbuka kile ulichokuwa ukimweleza juu ya ubaya
wa hayo mahusiano yake yasiyo na faida kwake na familia yake.

Msichana wa kazi ni msaidizi,mlinzi wa mali na familia yako kwa ujumla,
sasa kama ameanza mapepe hawezi kutimiza wajibu wake ipasavyo,
Anaweza akaleta madhara makubwa kwa watoto wako ( ksb maranyingi watoto ni wepesi kuiga yanayofanywa na watu wanaowazunguka),

Yawezekana wewe (familia yako ) imemtambua kuwa ni mmoja wa familia ,
lakin yeye hajajitambua kama ni mmoja wa familia , pia hajui nini kilichomleta hapa mjini.
KUMBADILISHA MTU TABIA NI KAZI SANA , ILA NI RAHISI SANA PALE ANAPOAMUA YEYE BINAFSI KUBADILIKA.

RAHA YA MTU UNAPOMWONA NA KUMCHULIA KUWA NI MTOTO WAKO,
BASI HATA YEYE AKUCHUKULIE KAMA MZAZI WAKE ,
AKISHAFANYA HIVYO BASI ITAKUWA RAHISI KUKUSIKILIZA NA KUZINGATIA USHAURI PINDI UNAPOMTOLEA/MPA.

Kila jambo linahitaji utulivu katika kuamua na si papara itokanayo na jazba.............................Ukikurupuka sana na mahousegirl..............
utakuja pata mdada aliyetulia sana.....laikini mchawi au anafanya huo ushenzi na watoto wako...................lipi bora hapo............

Hayo tunayasikia kila siku kwenye vyombo vya habari.
 
Mmmmh ndugu zangu, nahisi kama wote mnaomshauri huyu bwana mmesahau kwamba msichana wa kazi nae ni binadamu kama kawaida, na ana haki ya kupenda na kupendwa kama wengine, imeandikwa wapi ukiwa msichana wa kazi hatakiwi kuwa na mpenzi??? Embu tuwe na ubinadamu kidogo, cha muhimu ni kumkumbusha majukumu yake, na kumwambia asitumie karatasi za mtoto atumie daftari lingine kuandika barua, sio kumdhalilisha kubandika barua zake hapa, na namshangaa huyo mama mwenye nyumba, anataka huyo dada akiwa anataka mahusiano sijui akuchukue wewe??? maana ashukuru yuko na amadi muuza bucha na si wewe wala mtoto wa familia au ndugu yenu yeyote....tafadhali tuwe na utu, mie na kaa na msichana wa kazi miaka mingi sana na huwa ananiaga kabisa naenda kutembea anaondoka asubuhi hasa siku ya jumapili na kurudi jioni, nampa tu wosia jinsi dunia ilivyo na ajilinde vipi
 
Yaani Gaga umeongea yaliyokuwa moyoni mwangu..............a very nice post.
Unajua kwanza wengi wako underpaid,kazi j3-j2....saa11 asubuhi mpaka saa 6usiku.........yaani hakuna kupumzika.............

Halafu akikosa kidogo unataka kumtimua kama mbwa...............nao ni binadamu kama sisi jamani............hapo ameajiriwa kama wewe ulivyoajiriwa huko ukujuako..............ukitimuliwa kwa staili hiyo huko kazini kwako utapenda?.................

Kama hana kasoro nyingine kiutendaji..................ongeeni naye.............mkeo na wewe pamoja................mpeni muda wa kupumzika like siku ya jili(Yeye mwenyewe atajua aitumiaje siku hiyo).

Mi nategemea ana umri kati ya 16-18 au zaidi......................sasa kwa mabinti hasa wa ukanda wa kusini lazima awe na mahusiano.............
 
Mie kwa kweli nashindwa kuelewa watu wanawachukuliaje hawa, wanataka akae ndani tu, amekuwa mwali huyo? mwisho wa siku mtoto wako wa miaka nane anaanza kumlazimisha alale naye na kufundishwa mambo makubwa sababu tu, gate limefungwa na mlinzi kaambiwa dada siende popote,,hapana hawa wanatakiwa waheshimiwe na wapewe haki zao
 
Du! Usimtimua kwanza, ni stage ya maisha ambayo hata mtoto wako atakuja kupitia/ashapitia. Jaribu kumchukulia kama mwanao, na 'umlee' katika hilo ili litakapokuja kuwa kwa mwanao, uwe na experience.

Nasisitiza kama wenzangu.. ushauri ndio huo hapo juu... .Jiulize kama angekuwa mtoto wako ungefanya nini?..Ni sehemu ya maisha..yeye ni binadamu..na stage ya umri wake majaribu ni mengi.kikubwa msaidie.. mpe "live" faida na hasara..mfanye ajue analofanya na achague anataka nini...mwangalie kwa muda hasa tabia na ufanisi wa kazi... baada ya muda ukweli utadhiilika amechagua nini..hapo chukua hatua kufutana yeye amechagua nini..ushauri wako au hayo mambo..
 
Hili tatizo ni alisia na ninaweza kusema hata wanashauri humu wengi wamejisahau, wamesahau ndugu zao walivyo na wamesahau wao wenyewe walivyo na hata walivyokuwa siku za nyuma, yawezekana hata humu Members wengine ni kama huyu binti tusimuhukumu bila kumsahidia jamani.

Tuwe na utu, na tujuwe kuwa kama unaishi na mtu ni ndugu yako husimchukulie kama si ndugu yako na ukamuona kama hana haki ya kushauriwa na kusaidiwa na wewe unayeishi naye; Ukimchukuli huyu kama hakuhusu ukaweka mbele ubinafsi utakuta jibu la kumfukuza ni sahihi na rahisi sana halina matatizo na ndio jibu la bei chee, lakini kama Binadamu tu wabinafsi kiasi hicho basi hata hapa JF sisi sote ni wanafki na waongo maana kama tunaongozwa na Ubinafsi tunasaidiana ushauri wa nini au tunadanganyana hapa na kwanini wengine wanapoteza muda wao kufikiria mustakabali wa Taifa badala ya kufikiria mambo yao Binafsi.

Jiweke katika nafasi ya Mzazi na huyo ni mdogo wako lolote utakalo mfanyia uwe ndani ya viatu vya mzazi, maana huyo ni mtoto ambaye anatanga na dunia anahitaji kusahidiwa kama Mtazania mwenzetu. Angalia sheria na taratibu kama kama kuna kosa amevunja au yule muuza nyama kavunja unaweza kuchua hata hatua za kisheria dhidi ya muuza nyama, lakini pia anahitaji elimu hasa ya afya na ngono kuna magonjwa hawa watoto taama zinawapereka pabaya sana wanarukia wazee kama hawana akili nzuri, hawajui kama kuna Ukimwi au la!

Kumfukuza iwe hatua ya mwisho sana lakini hakikisha wazazi wake wanapata taarifa juu ya mienendo yake, pia kuwa makini sana kama una vijana hapo nyumbani hawa mabinti wanachipukia ndio wamekuwa njia kuu ya kuambukiza Ukimwi siku hizi vijana hasa wadogo zako wasije wakarukia itakuletea balaha baadae. Wadogo zetu siku hizi wanaongozwa na tamaa zaidi sasa huyu sijui nyama choma na pesa ya huyu muuza nyama ndio inamponza; unaweza pia kuangalia hatua ya kuwaozesha kama kwakuwahusisha wazazi wake ili awe mke wake badala ya kumdanganya akaishia pabaya kwa sababu unaweza kukuta muuza nyama anao kama hao kumi hatari sana.

Pole Mkuu ndio ukubwa huo.
 
mh house girl noma ..na muuza bucha atakuwa mgogo tu huyo..
Mimi nafikiri, karibu kuwa na hakika, kuwa muuza bucha ni Mpemba, anaitwa Hamadi (amadi) kwa lafudhi ya HG.
Turudi kwenye mada, kama angekuwa mtoto wako ungefanya nini? Bila ya shaka usingemtimua kama hatua ya mwanzo au pengine daima usingeamua hivyo. Kwa hivyo, nakubaliana na walioshauri usikimbilie kumimua. Chukulia kama ni mtoto wako na jitahidi
kufunza na kumfahamisha ulimwengu.
Lakini pia kama ilivyosemwa na wachangiaji wengine, wazazi wa huyu HG wanajua kuwa mtoto wao yuko kwako na kwa sasa jukumu lote liko kwako. Kwa hivyo ninakushaurini muwajulishe wazazi wake juu ya mwenendo wake ili likitokea lolote lawama zisiangukie kwako/kwenu.
Na kama umeamua kumtimua, basi mtimue kwa kumrejesha kwao wewe mwenyewe, umkabidhi kwa wazazi wake au yeyote aliyekukabidhi wewe, na unawe mikono.
 
Hili tatizo ni alisia na ninaweza kusema hata wanashauri humu wengi wamejisahau, wamesahau ndugu zao walivyo na wamesahau wao wenyewe walivyo na hata walivyokuwa siku za nyuma, yawezekana hata humu Members wengine ni kama huyu binti tusimuhukumu bila kumsahidia jamani.

Tuwe na utu, na tujuwe kuwa kama unaishi na mtu ni ndugu yako husimchukulie kama si ndugu yako na ukamuona kama hana haki ya kushauriwa na kusaidiwa na wewe unayeishi naye; Ukimchukuli huyu kama hakuhusu ukaweka mbele ubinafsi utakuta jibu la kumfukuza ni sahihi na rahisi sana halina matatizo na ndio jibu la bei chee, lakini kama Binadamu tu wabinafsi kiasi hicho basi hata hapa JF sisi sote ni wanafki na waongo maana kama tunaongozwa na Ubinafsi tunasaidiana ushauri wa nini au tunadanganyana hapa na kwanini wengine wanapoteza muda wao kufikiria mustakabali wa Taifa badala ya kufikiria mambo yao Binafsi.

Jiweke katika nafasi ya Mzazi na huyo ni mdogo wako lolote utakalo mfanyia uwe ndani ya viatu vya mzazi, maana huyo ni mtoto ambaye anatanga na dunia anahitaji kusahidiwa kama Mtazania mwenzetu. Angalia sheria na taratibu kama kama kuna kosa amevunja au yule muuza nyama kavunja unaweza kuchua hata hatua za kisheria dhidi ya muuza nyama, lakini pia anahitaji elimu hasa ya afya na ngono kuna magonjwa hawa watoto taama zinawapereka pabaya sana wanarukia wazee kama hawana akili nzuri, hawajui kama kuna Ukimwi au la!

Kumfukuza iwe hatua ya mwisho sana lakini hakikisha wazazi wake wanapata taarifa juu ya mienendo yake, pia kuwa makini sana kama una vijana hapo nyumbani hawa mabinti wanachipukia ndio wamekuwa njia kuu ya kuambukiza Ukimwi siku hizi vijana hasa wadogo zako wasije wakarukia itakuletea balaha baadae. Wadogo zetu siku hizi wanaongozwa na tamaa zaidi sasa huyu sijui nyama choma na pesa ya huyu muuza nyama ndio inamponza; unaweza pia kuangalia hatua ya kuwaozesha kama kwakuwahusisha wazazi wake ili awe mke wake badala ya kumdanganya akaishia pabaya kwa sababu unaweza kukuta muuza nyama anao kama hao kumi hatari sana.

Pole Mkuu ndio ukubwa huo.
Hapa Mkuu umesoma mawazo yangu, najuta kwa nini nikakimbilia kuchangia bila kusoma post yako.
Uliompa ni ushauri mzuri kabisa.
 
Mimi binti akifikisha miaka 16 lazima kuna ka uhuru fulani awe nacho, hata akiwa ana date huyu sita mkaripia bali nitamwelekeza njia muhimu za kufata kwenye mahusiano ya umri kama huo, na wengi sana wanaishia kwenda kufanya mapenzi na hao wapenzi wao sababu ya walezi wao wanakuwa tu wakali bila kuwapa mwongozo, nina assume huyu ni kuanzia miaka 18.....mpe maadili mpe uhuru wake kiasi ,ssio awe kama mfungwa wako
 
Wakati fulani mwaka jana mwanzoni sikuwa na simu. Ilibidi niombe simu ya HG naweka card yangu naitumia namaliza namrudishia. Siku moja wakati nahangaika kufuta msg zangu nilizotuma, nilikuta huko msg za matusi hayaandikikii hapa amemwandikia mpenzi wake. Sikuonyesha kama nimefahamu kitu au nimezisoma! Nilimrudishia simu yake, nikanunua yangu nikakoma kutumia simu yake. HG wangu ni mdada mkubwa, ameacha mtoto nyumbani kwao, mtoto yuko darasa la 4 sasa. Sikuchukua hatua yoyote kumsema wala kumkaripia, maana majukumu anafanya vizuri, akitoka anawahi kurudi, akichelewa anatuma msg kuomba samahani na kwamba yuko njiani foleni ni kubwa. Ninae sasa huu mwaka wa 3 na anasoma VETA kozi ya House Keeping. Wakati mwingine ni kuwasaidia wajue kutenganisha mapenzi na kazi, labda kama utaona kamecharuka sana hakasikii. Umri ukifika, huna la kuzuia ila kuelekeza how to.
 
Kila jambo linahitaji utulivu katika kuamua na si papara itokanayo na jazba.............................Ukikurupuka sana na mahousegirl..............
utakuja pata mdada aliyetulia sana.....laikini mchawi au anafanya huo ushenzi na watoto wako...................lipi bora hapo............

Hayo tunayasikia kila siku kwenye vyombo vya habari.

NAKUBALIANA NA WEWE KUWA SI VIZURI KUKURUPUKA/JAZIBA WAKATI WA KUFANYA MAAMUZI,
UKISOMA POST YANGU KWA UMAKINI UTAGUNDUA KUWA NIMESEMA AMRUDISHE KWAO,
BAADA YA KUCHUKUA BAADHI YA HATUA KAMA KUMWONYA,KUMTAHADHARISHA..NK.
NILIAMUA KUSEMA HIVYO ILI KUEPUSHA HAYO MAAMUZI YA KUKURUPUKA/JAZBA KUMRUDISHA KWAO BALI
IWE NI HATUA YA MWISHO KABISA, UKIZINGATIA KUWA KILA JAMBO LINA MWISHO WAKE WA UVUMILIVU.

Suala la kupata msichana mwenye tabia nzuri au baya hilo hakuna anayelipanga,
ila linatokea ukichukulia kuwa hsegal ni binadamu kama tulivyo binadamu wote ,
tuna mazuri na mapungufu yetu,ukimpata anayelingana na vigezo vyako shukuru MUNGU,
lakin yule asiyempata asiyelingana na vigezo vyake pia asilaumiwe,pia kubadilisha hsegal siyo dhambi japo wakati mwingine siyo vizuri.
(siyo mbadilishaji wa ma hse gal naomba usinielewe hivyo Ballerina....lol ,niliyenaye ana miaka zaid ya 5 kwangu)

UNAPOISHA NA HSE GAL NI LAZIMA UVUMILIVU UTAWALE JUU YAKE,
KAMA AMBAVYO YEYE ANAVUMILIA ANAPOKUWA KATIKA HIMAYA YETU.
 
Wakati fulani mwaka jana mwanzoni sikuwa na simu. Ilibidi niombe simu ya HG naweka card yangu naitumia namaliza namrudishia. Siku moja wakati nahangaika kufuta msg zangu nilizotuma, nilikuta huko msg za matusi hayaandikikii hapa amemwandikia mpenzi wake. Sikuonyesha kama nimefahamu kitu au nimezisoma! Nilimrudishia simu yake, nikanunua yangu nikakoma kutumia simu yake. HG wangu ni mdada mkubwa, ameacha mtoto nyumbani kwao, mtoto yuko darasa la 4 sasa. Sikuchukua hatua yoyote kumsema wala kumkaripia, maana majukumu anafanya vizuri, akitoka anawahi kurudi, akichelewa anatuma msg kuomba samahani na kwamba yuko njiani foleni ni kubwa. Ninae sasa huu mwaka wa 3 na anasoma VETA kozi ya House Keeping. Wakati mwingine ni kuwasaidia wajue kutenganisha mapenzi na kazi, labda kama utaona kamecharuka sana hakasikii. Umri ukifika, huna la kuzuia ila kuelekeza how to.

Anaendeleaje?
 
mmmh, HG ni kazi inayodharauliwa na baadhi ya watu, wakati huo huo maisha ya familia yako mikononi mwao, sijajua kwa nini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom