Barua ya wazi kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa JMT

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Naomba kuchukua fursa hii kukupongeza kwa kuapishwa kuwa Rais- wa JMT. Nikupe pole kwa kupata nafasi hii ukiwa katika hali ya majonzi na nikuombe usitetereke, umepokea kijiti angali nchi inakimbia kiuchumi nawe usikubali kwa namna yoyote kwenda speed ndogo kuliko mtangulizi wako, kanyaga mafuta.

Nimepnda kuchukua nafasi kukupa changamoto za maeneo kadhaa yakuboresha ili hatimaye utakapo kanyaga mafuta basi gari liongeze speed. Mambo ninayoweza kukushauri ni haya yafuatayo;

1. Pamoja na ugumu uliopo, nakuomba utusaidie kutenganisha majukumu ya chama na majukumu ya serikali. Tunaomba utumishi wa Umma uachwe uwe utumishi wa Umma. Nashauri hivi kwa sababu usipokuwa na watumishi wenye hari na moyo hata ukanyage mafuta vipi gari haitakimbia kwa kiwango ulichopanga. Kwa kuanza mwondoe Katibu mkuu Kiongozi aliyepo si kwa sababu siyo mchapakazi bali historia yake kwa nchi hii na msimamo wake kwa chama hautamwezesha kutenda haki kwa watu wote. He will never be neutral person even if he will commit himself to neutral no one will evaluate and consider him as neutral person. Katibu wa chama Cha siasa hawezi kusimamia utumishi wa Umma kwa haki na Bashiru anajua hivyo na hata kwenye katiba mpya alisimamia hoja yakutenganisha madaraka ya utumishi na siasa, wewe una nafasi yakumpangia kazi nyingine na watumishi wa Umma watakusikiliza na watafanya kwa moyo.

2. Tusaidie kutenganisha dola na siasa. Nikushauri, lisaidie Taifa kujiondoa kwenye mfumo wa dola kuwa sehemu ya mikakati ya chama chetu Cha mapinduzi. Viongozi wa chama Cha mapinduzi wa sasa wamekuwa wategemezi wa fikra kutokana na wakati wote kuamini hata wasiposhinda kwa hoja watashinda kwa nguvu ya dola. Kirejeshee chama nguvu yake ya kisiasa kwa kukitenganisha na dola.

3. Wawezeshe dola kufanya ujasusi wa kiuchumi nje ya mipaka yetu nakulinda soko la ndani. Mapambano Kati ya dola na Wafanyabiashara wa ndani nimakubwa sana na yameua biashara nyingi nchini. Tengeneza Uhuru na misingi imara yakuwalinda Wafanyabiashara wa ndani kupitia dola huku ukiwawezesha wananchi kuziona fursa nje ya mipaka yetu. Endapo dola itazidi kukita mizizi ndani bila kufanya ujasusi wa fursa nje ya Tanzania utawala wako utakuwa mgumu kwa sababu kundi la wataka ajira na fursa limekuwa kubwa. Fungua milango watu wqtawanyike Duniani na Balozi zetu zisimamie ilo.

4. Miradi yote aliyoanzisha mtangulizi wako isisimame, Bora ukope lakini ikamilike kuepusha hasara. Lakini miradi hi Ni moyo wa Taifa linalopanga kujitegemea.

5. Wape watumishi motisha na stahiki zao kikatiba.

6. Liponye Taifa, fanya maridhiano hata Kama chama chako hakitaki.

7. Lipatie Taifa katiba mpya

8. Usijipange kugombea urais 2025 endapo utatekeleza agenda ya kulipatiwa Taifa katiba mpya. Jipange kustaafu siasa ili uwe netral wakati wa mchakato wa katiba. Endapo unajipanga kugombea na kuanzisha harakati za katiba mpya hautatuachia katiba mpya kwa sababu utataka kutupa katiba yakukuakikishia ushindi na usalama uwapo madakani. Mfano.wakipendekeza Rais ashtakiwe wewe utopenda kukiona kipengele Kama hicho.

9. Usikubali kuwa Mwenyekiti wa CCM kwa Sasa, kubali kuwa Mwenyekiti endapo tu unampango wakugombea 2025 nafasi ya urais. Kwa hapa Taifa lilipo na miradi iliyopo mbele yako pamoja na mategemeo ya Watanzania pls usiongeze mzigo.

10. Safisha ofisi ya DPP uweke watu wanaoheahimu utu na taaluma. Ofisi hiyo inasemwa vibaya sana hasa na viongozi wanaoisimamia katika ngazi ya kitaifa na wizara husika.

11. Usiwatoe waliopo mahabusu bali elekeza mahakama ziwasikilize na wapelelezi wakamilishe uchunguzi. Ukiamuru watolewe utaonekana umeingilia mahakama, ila ukiruhusu wasikilizwe na mahakama naamini DPP atawasomea mashtaka na Kama bado ana uchunguzi wataachiwa kwa dhamana waungane na familia zao wakati wakisubiri hukumu. Nadhani unaelewe ni watu wangapi wapo mahabusu kwa miaka kadhaa bila kusikilizwa. Nadhani unajua ni namna gani DPP qmekuwa akitumia rungu la sheria kunyima watu dhamana....we live once if God wishes, give them freedom

12. Usitumbue sana, tymbua pale ambapo uchunguzi na ripoti iliyopo mezani mwako inakupa ushahidi wakutumbua. Ukitumbua sana watu watakuogopa na utadhani kazi zinaenda ila haziendi.

13. Sikiliza sana, sikiliza wote- chambua then toa maamuzi.

14. Ruhusu Uhuru wakutoa maoni na kusema kusikovunja sheria.

15. Dhibiti wasiojulikana

16. Jenga miundombinu mizuri kwenye mipaka yetu hasa ya nchi kavu kuruhusu baishara, Kodi na usalama...mifumo ya Tehama ikusaidie kukusanya Kodi na kudhibiti wasiotakia mema uchumi wetu na Tqifa letu.

17. Rudisha mahusiano na jumuhia zakimataifa ikiwemo Sadec na EAC

18. Usiruhusu mabeberu wakaingia Tena jikoni kwa uchochoro wa diplomasia, tuendele kujijenga kwa kutokuwa na rafiki wakudumu wala adui wakudumu.

19. Tuondolee viongozi wote wa kisiasa na kiutumishi wanaolalamikiwa na walioshindwa kuheshimu wakubwa kipindi wewe ukiwa siyo Rais. Naamini unawajua, Wapo viongozi walitumiwa usuluishi Hadi wa PM lakini waliendelea kuwa shingo ngumu, walitumwa akina Mzee mkuchika wakashindwa kusikilizwa.. tuondolee unatachables na nchi itakuwa salama

20. Tuongoze kumtegemea Mungu nakulisafisha Taisha na damu zilizomwagika ambazo badala yakuleta ukombozi zimezalisha mafarakano. Liponye Tqifa, tuongoze kupata toba ya kweli kwa kuzika yakale.

Nikitakie kazi njema na Mwenyenzi Mungu akubariki.
 
Barua za wazi zimekuwa nyingi sana, zingine Fanyeni ziwe confidential
 
Kila mtu anamshauri mama yetu,is not a bad thing,lakini mtamchanganya mama wa watu,ashinde asilale usiku akipitia ushauri wenu,,,lol
 
Ushauri mzuri sana kama utapokelewa. No 18...tafadhali naomba ufafanuzi kidunchu(Japo mm sio raisi)
 
Barua za wazi zimekuwa nyingi sana, zingine Fanyeni ziwe confidential
Barua za wazi zimekuwa nyingi kwa sababu kuna mambo mengi Serikalini hayaendi sawa kutokana na confidentiality ya Serikali yenyewe imejifanya hard to find ili kuficha yasiyo lazima kufichwa ikiwa ni pamoja na ugonjwa, vifo, mauaji na vyombo vya Dola, wizi mali za umma nk. Serikali iwe wazi, ifiche siri zake!
 
Namba 9 akiikubali atafanya kazi katika mazingira magumu sana. Wanaccm wanawwza kumzidi nguvu wakati wowote.

Namba tano akifanikisha hata kelele za mitandaoni zitapungua kwasababu wanyonge aliokuwa anadili nao magufuli wengi si wapiga kelele mitandaoni.
 
Wingi wa barua ni dhahiri utawala wa awamu ya tano maoni mengi yalipuuzwa.

Barua hii makini sana,pamoja na barua zingine Mama azifanyie kazi.Maudhui yanafanana kwa kiasi kikubwa
 
Beatrice Kamugisha ingawa naona jinsi wahaya mnavyopigana vita unlike wachagga, namba 4. Utakuwa umemfurahisha JK maana Hiyo ndiyo fursa ya kuingiza ufisadi katika hasa miradi mikubwa yenye manufaa kwa nchi kiuchumi kuliko mingine; wa umeme kama hautakuwa na ufisadi, tunategemea unit ya umeme ishuke. Ikishuka, jua gharama za uzalishaji bidhaa viwandani zitashuka Hivyo Kuvutia uwekezaji nchini; wengi wenu mtapata ajira.

Mradi wa pili ni SGR kama hakutakuwa na ufisadi basi naamini usafishaji wa mizigo na abiria utakuwa na unafuu na wa haraka. Hivyo gharama za kusafirisha bidhaa mfano toka Dar hadi Kigoma utakuwa nafuu na wakazi wa Kigoma watanunua bidhaa kwa bei nafuu. Ila ufisadi ukiingia hapo tumeliwa.

namba 8. Nakuunga mkono Kwani ili kupata katiba mpya, lazima muwe na kifungu kinachowakataza wote watakaohusika kutogombea cheo chochote kwa angalau miaka 20. La sivyo itakuwa kama JK alivyovuruga mchakato wa hiari kwa kuharibu draft ya Warioba kwa kuuliza wabunge kama hawataki uwaziri. Kuhusu mwenyekiti wa ccm naona humpendi Samia, watakuondoa kesho asubuhi. Lazima agangamale awe mwenyekiti ila aangalie makundi yaccm maslahi na ccm mpya. Akina Kinana, makamba, nape, January etc ni ccm maslahi
 
Nasema Amina kwa namba 3 na 15,
Pale TISS,Mh Raisi weka Mkurugenzi mwingine,hazina,Doto James mpangie kazi nyingine,Waziri wa fedha,mpumzishe,DPP weka mwingine,.
 
1 Masheikh wa UAMSHO wasikilizwe, Mama samia naomba ulisimamie wewe kama Mama yangu na Rais wangu kipenzi..usipofanya hivyo utabeba dhima kubwa na utaulizwa , kumbuka hao ni Waislamu wenzio,, المسلم أخو المسلم kikwete mpaka anastaafu hakuzungumzia chochote, sasa anakula bata na familia yake, wenzie huko wanateseka gerezani. Allah awaongoze na awafanyie wepesi ndugu zetu.

2 Wafanyabiashara wapunguziwe kodi n.k
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom