GAZETI
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 5,277
- 6,673
Mheshimiwa Rais, sisi wakulima wa zao la korosho ni miongoni mwa watu tusiosikilizwa na tunaopigwa danadana kwenye mambo mengi sana, Bila msaada wako hatuwezi kunusurika.
Kwa nia safi Kabisa serikali imeamua kugawa Viuatilifu kwa wakulima lakini jambo la kushangaza ni kuwa havigaiwi kwa wakati licha ya kuwa viko kwenye maghala ya vyama vya msingi vya ushirika. Ni miezi miwili na zaidi sasa toka awamu ya kwanza ya ugawaji ipite, Kwa mikorosho ni hatari kwani unavyokaa muda mrefu bila kupiga dawa inapelekea kuua maua na hivyo kusababisha uzalishaji kupungua.
Rais Samia, kinachosikitisha ni kuwa hizi pembejeo zipo kwenye maghala lakini zinashindwa kufanikiwa kutokana na kukosekana kwa vitu vinavyoitwa Vibandiko, Sasa serikali inawezeje kusafirisha mzigo mkubwa wa viuatilifu halafu ishindwe vibandiko ambavyo ni vikaratasi vidogo sana visivyo na uzito wowote Jambo la kushangaza ni kuwa tatizo hili limekuwa likijirudia kila awamu.
Muheshimiwa Rais, sisi wakulima wa korosho ni wanachi wako kama walivyo wananchi wengine, kwanini tunanyanyasika kiasi hiki? Tunaamini wewe kama kiongozi wa nchi unaweza kutatua hili ili kuokoa zao la korosho na wakulima wake na si hivyo tu bali pia korosho zinachangia pato la Taifa.
Ahsante