Pengo
JF-Expert Member
- Oct 15, 2009
- 579
- 10
Ndugu John Mnyika,naandika barua hii kuwakilisha mawazo na vilio vya wana Ubungo kuhusu matatizo ya miundombinu hususani ubovu wa barabara zao.
Wana Ubungo wengi wamenituma niwasiliane nawe ili kuweza kujaribu kutatua matatizo ya siku nyingi wayapatayo katika barabara zao kwavile wana imani na wanaamini kuwa wewe ndiye uliyeshinda ubunge mwaka 2005 kabla ya kupokwa na wenye nchi yao na pia wana imani kuwa kwa uwezo wa muumba mwaka 2010 utaweza kuteuliwa na chama chako(chochote kile) na kuweza kushinda ubunge katika jimbo sugu la matatizo licha ya kuwa ni kiunganishi na miji mikubwa barani Afrika.
Mh.Mnyika wana ubungo wanakuomba fanya ziara ya mara kwa mara katika maeneo yanayozunguka jimbo lako kama Ubungo kibangu,kimara temboni,kimara golani,king'ongo,mbezi msumi,malamba mawili na kwingineko.Hayo maeneo hayapitiki kirahisi kwa gari na kusababisha adha kubwa ya usafiri na haswa wakati wa kwenda na kurudi makazini.Wakina mama wajawazito inakuwa mtihani pale uchungu unapowafika na wengi wameshawahi kujifungulia barabarani kwa hali ilivyo.
Mh.Mnyika,kutokana na mateso wanayoyapata wanaubungo wameona ni bora ya lawama kuliko fedheha,kwani kulaumiwa kwa kumchagua Mnyika na kuwa mwakilishi wao bungeni ni bora mara milioni kuliko karaha wanayopata wananchi kwa kukosa mahitaji muhimu ya maisha yao kwavile barabara hazipitiki.
Mh.Mnyika unaombwa tembea na wanahabari ukianzia barabara ya Suka kwenda Golani utaona hali halisi ya wanaubungo na haswa pale mvua kidogo inaponyesha basi mawasiliano ndio ukatika kabisa.Nenda maeneo hayo na mengine ukiambatana na waandishi ili ikiwezekana hayo maeneo yapigwe na picha kabisa.Baada ya hapo utafute suluhisho la matatizo ya wananchi wako wakati ukijiandaa kutinga mjengoni.
Mwisho wana ubungo wanasema kwavile umeonyesha nia ya kuwakomboa na matatizo yanayowakera kwa muda mrefu,jiandae kutinga Dodoma kwa kishindo kwani safari hii hawana imani tena na hao waliokuwa wanawafanya 'vibatari' ambavyo hutumika pale umeme unapokatika na umeme ukiwaka haviitajiki tena na utupwa na kusahauliwa.
Mungu Ibariki Tanzania,mungu ibariki Ubungo,Mungu mbariki John Mnyika.