Barua ya wazi kwa Mh.John Mnyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua ya wazi kwa Mh.John Mnyika

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pengo, Jun 19, 2010.

 1. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ndugu John Mnyika,naandika barua hii kuwakilisha mawazo na vilio vya wana Ubungo kuhusu matatizo ya miundombinu hususani ubovu wa barabara zao.
  Wana Ubungo wengi wamenituma niwasiliane nawe ili kuweza kujaribu kutatua matatizo ya siku nyingi wayapatayo katika barabara zao kwavile wana imani na wanaamini kuwa wewe ndiye uliyeshinda ubunge mwaka 2005 kabla ya kupokwa na wenye nchi yao na pia wana imani kuwa kwa uwezo wa muumba mwaka 2010 utaweza kuteuliwa na chama chako(chochote kile) na kuweza kushinda ubunge katika jimbo sugu la matatizo licha ya kuwa ni kiunganishi na miji mikubwa barani Afrika.
  Mh.Mnyika wana ubungo wanakuomba fanya ziara ya mara kwa mara katika maeneo yanayozunguka jimbo lako kama Ubungo kibangu,kimara temboni,kimara golani,king'ongo,mbezi msumi,malamba mawili na kwingineko.Hayo maeneo hayapitiki kirahisi kwa gari na kusababisha adha kubwa ya usafiri na haswa wakati wa kwenda na kurudi makazini.Wakina mama wajawazito inakuwa mtihani pale uchungu unapowafika na wengi wameshawahi kujifungulia barabarani kwa hali ilivyo.
  Mh.Mnyika,kutokana na mateso wanayoyapata wanaubungo wameona ni bora ya lawama kuliko fedheha,kwani kulaumiwa kwa kumchagua Mnyika na kuwa mwakilishi wao bungeni ni bora mara milioni kuliko karaha wanayopata wananchi kwa kukosa mahitaji muhimu ya maisha yao kwavile barabara hazipitiki.
  Mh.Mnyika unaombwa tembea na wanahabari ukianzia barabara ya Suka kwenda Golani utaona hali halisi ya wanaubungo na haswa pale mvua kidogo inaponyesha basi mawasiliano ndio ukatika kabisa.Nenda maeneo hayo na mengine ukiambatana na waandishi ili ikiwezekana hayo maeneo yapigwe na picha kabisa.Baada ya hapo utafute suluhisho la matatizo ya wananchi wako wakati ukijiandaa kutinga mjengoni.
  Mwisho wana ubungo wanasema kwavile umeonyesha nia ya kuwakomboa na matatizo yanayowakera kwa muda mrefu,jiandae kutinga Dodoma kwa kishindo kwani safari hii hawana imani tena na hao waliokuwa wanawafanya 'vibatari' ambavyo hutumika pale umeme unapokatika na umeme ukiwaka haviitajiki tena na utupwa na kusahauliwa.
  Mungu Ibariki Tanzania,mungu ibariki Ubungo,Mungu mbariki John Mnyika.
   
 2. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,841
  Likes Received: 1,101
  Trophy Points: 280
  hahahaha! no comment.
   
 3. P

  Paul S.S Verified User

  #3
  Jun 19, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Naamini amekusikia
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mi kura yangu nampa Mnyika bahati nzuri nitapigia huko huko Ubungo
   
 5. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,402
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  Nyie subirini tuu muone vibweka uchaguzi huu kama hamjapewa mteule mwingine kutoka kule kule!!Hii system ni corrupt hata Mwl.J.K alishasema sanaa!!
   
 6. Kibukuasili

  Kibukuasili JF-Expert Member

  #6
  Jun 19, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 858
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Miaka yote mkuu ulikua wapi barua unaandika leo? Kampeni tu hamna cho chote!
   
 7. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #7
  Jun 19, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Ufumbuzi kwenye vitendawili vifutavyo pia Mkuu:.
  1. Maji safi na salama
  2. Umeme usion na uhakika (japo mitambo ya Tanesco imefungwa hapo)
  3. Ungufu wa walimu na vitendea kazi mashuleni
  4. Ukosefu wa Zahanati, wataalamu na madawa katika zile chache zilizopo
  5. Kukosekana kwa maeneo ya kupumzikia (Kumbi za Burudani, viwanja vya michezo nk)
  6. Usafiri wa uhakika
  7. Uhamasishaji wa vikundi vya vijana kujikwamua kiuchumi
  8. Matatizo ya ardhi
  9. Ujenzi holela
  10. Mazingira machafu
   
 8. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #8
  Jun 19, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Pole mkuu, lakini Mnyika hana mafungu ya kujengea barabara. Tunaamini atajitahidi kupiga kelele, pengine hao walioweka pamba masikioni wataweza kusikia. Lakini vinginevyo, si kazi ya mbunge kujenga barabara, bali ni kazi yake kuwakumbusha TANROADS na wizara ya miundombinu kufanya hivyo. Na kama siyo kipaumbele cha wizara imekula kwenu.
   
 9. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  kila la heri Mnyika
   
 10. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #10
  Jun 19, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Pamoja na hizo rushwa zao,mwaka huu jimbo letu!
   
 11. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #11
  Jun 19, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Na wewe(Mgombea Ubunge Mtarajiwa) unagombea jimbo gani?????????????????
   
 12. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #12
  Jun 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Balantanda kwa uchokozi:bump2:
   
 13. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #13
  Jun 19, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Hapana si uchokozi mkuu......Ni bora akawa wazi tili tuangalie tutamuunga vipi mkono(maana kaomba tumuunge mkono)...........Afanye kama alivofanya Mtanzania ambaye ana mpango wa kugombea Kyela
   
 14. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #14
  Jun 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Lakini si kila wanalofanya wale wavaa kijani lazima lifanywe na wavaa kombati siyo? Wao naona hawana papala ya kujitangazia majimbo kabla ya muda. We vuta subira tu mkuu wangu. Utajua si punde kuwa Gender sensitive anagombea.....................
   
 15. M

  MC JF-Expert Member

  #15
  Jun 20, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  My vote is for you Mnyika,

  I'm from King'ongo, Alichosema Mkuu hapo juu ni kweli kabisa matatizo ni kibao kuliko maelezo.


  MC
   
Loading...